PENIELA
SEASON 4
EPISODE 5
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Narudia tena kukuhakikishia Jacob kwamba endapo mpango huu utafanikiwa basi tutaingia katika orodha ya mabilionea kwa hiyo nakuomba usije ukabadili mawazo” akasema Dr Kigomba
“ Only a fool can do that.Nakuhakikishia Kigomba siwezi kubadili mawazo.Nimekuwa mtiifu katika kazi yangu lakini hakuna chochote cha maana nilichokipata zaidi ya kujenga maadui wengi.Nadhani ni wakati wangu na mimi kufanya mambo ambayo wengine wanafanya yaani kujitengenezea maisha mazuri baada ya kustaafu” akasema Jacob
“ Ahsante Jacob kwa kuwa na muono huo.Muda wa uzalendo umepita na sasa ni wakati wa kujijengea maisha mazuri baada ya kustaafu.Tutaongea vizuri zaidi na kwa kirefu kesho.” Akasema Dr Kigomba na kisha wakaagana na Dr Kigomba akaondoka kuelekea nyumbani kwake
“ Kama ulifikiri una akili sana,ulikuwa unajidanganya Dr Joshua .Sasa nitakuonyesha kwamba kuna watu wana akili zaidi yako” akawaza Dr Kigomba wakati akielekea nyumbani kwake kupumzika.
ENDELEA………………..
Kumekucha Tanzania .Taarifa ,kubwa iliyoliamsha taifa asubuhi hii ni tukio la polisi kupambana na majambazi wenye silaha katika msitu wa Makenge na kufanikiwa kuwaua majambazi wanne.Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kanda ya Dare s salaam aliyehojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya tukio lile kutokea ni kwamba walipokea taarifa kuhusu kuwapo kwa kambi ya majambazi katika msitu wa Makenge kutoka kwa jaji Eibariki.
Kamanda Yule aliendelea kusema kwamba jaji huyo wa mahakama kuu ambayealikuwa anatuhumiwa kwa mauaji ya mke wake ambaye ni mtoto wa rais,alikuwa ametekwa na watu hao siku kadhaa zilizopita na alipelekwa katika msitu wa Makenge ambako alifichwa katika pango
“ Akiwa mafichoni“ akaendelea mkuu wa polisi kanda ya Dare s salaam
“ Watu wale walimtaka jaji Elibariki ampigie simu mke wake na kumtaka afike mahala walikopanga.Lengo lao lilikuwa ni kumteka Flaviana mtoto wa rais na kudai kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa rais ili wamuachie.
Jaji Elibariki alifanya kama alivyoelekezwa na Flaviana alipofika sehemu walikopanga wakutane majambazi wale walijitokeza na kutaka kumteka lakini kwa bahati nzuri alikuwa ameongozana na walinzi na hapo ndipo walipoanza kushambuliana na katika tukio hilo Flaviana alijeruhiwa kwa risasi akafariki akiwa katika matibabu nchini Afrika ya kusini.
Jaji Elibariki ,alifanikiwa kutoroka toka mafichoni alikokuwa anashikiliwa na majambazi hayo na kunipigia simu akanifahamisha kila kitu na kutuelekeza mahala wanakojificha majambazio hao .Usiku wa kuamkia leo polisi walivamia maficho ya majambazi hayo na pakatokea majibizano ya risasi kwa zaidi ya nusu saa lakini polisi walifanikiwa kuwadhibiti .
Majambazi wanne waliuawa na wawili walifanikiwa kutoroka.Katika eneo walilotumia majambazi hayo kama maficho yao kulikutwa na silaha mbili aina ya smg , na risasi mia moja na kumi.Kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na msako mkali kuwatafuta majambazi waliotoroka pamoja na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Mathew ambaye inasemekana ndiye anayeshirikiana na majambazi hayo na kuwasaidia katika kufanikisha mipango yao ya kihalifu”
Hii ilikuwa ni taarifa fupi iliyotolewa na kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam kwa baadhi ya waandishi wa habari,muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio lile la majambazi na polisi kushambuliana kwa risasi katika msitu wa Makenge tukio lililotokea mida ya saa kumi na moja za alfajiri.
Dr Joshua ambaye kwa kawaida huwa hakosi kutazama taarifa ya habari .Aliitazama taarifa hii iliyopewa umuhimu mkubwa akatabasamu
“ he did it…!! Akasema kwa furaha
“ hawa ndio watu ninaopenda kufanya nao kazi.Ukimpa maelekezo yanafanyika kama unavyotaka.Nimeongea naye jana usiku na usiku huo huo akatafuta namna ya kulimaliza suala ambalo lilikuwa linanila sana akili yangu.I’m very Impressed .
Kabla ya uongozi wangu kumalizika lazima na huyu kamanda wa kanda ya Dare s salaam nimuache katika nafasi nzuri.” Akawaza Dr Joshua na kuchukua simu akazitafuta namba za kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam akampigia
“ hallow mzee.” Akasema Kamanda wa polisi baada ya kupokea simu
“ Habari yako Kamanda”
“ Habari nzuri sana mzee.Samahani nimechelewa kukupigia simu kukutaarifu kuhusiana na kukamilika kwa ile kazi uliyonipa”
“ Usijali kuhusu hilo kamanda,nimeona katika taarifa ya habari muda mfupi uliopita.Thank you so much”
“ Mzee,jana baada ya kumaliza kuzungumza nawe ,nilianza kuchekecha akili namna ya kufanya nikakumbuka niliwahi kupewa taarifa za kuwapo kwa majambazi wanaotumia msitu wa Makenge kama maficho yao .Taarifa hii haikuwa imefanyiwa kazi bado kwa hiyo nilikuwa nayo mimi pekee hivyo niliwaandaa vijana na kuwapa maelekezo na mimi mwenyewe nikaongozana nao hadi katika msitu wa Makenge na kweli tulifanikiwa kuwakuta majambazi hao tukawavamia na kushambuliana nao tukawaua wanne, wawili wakatoroka.
Hiyo ilikuwa ni njia nyepesi niliyoweza kuifanya ya kumsafisha tena Elibariki na kumuondoa katika zile tuhuma zilizokuwa zinamkabili.Kwa sasa mpira umerushwa kwa huyu Mathew na Elibariki amesafishika na hahusiki tena katika tuko lolote.
Nitaonana naye na kumpa maelekezo ya namna ya kuzungumza na waandishi wa habari ambao watapenda kumuhoji au mtu yeyote atakayemuuliza kuhusuana na tukio hili lakini hadi hapo nitakapokuwa nimeongea naye naomba asihojiwe na mtu yeyote Yule au chombo chochote cha habari”
“ Kamanda nimefurahi sana kwa namna ulivyo mbunifu.Sitaki nikuahidi chochote kwa sasa ila naomba unisubiri kwa kama wiki mbili hivi na utaona nitakachokufanyia.Watu watiifu kama ninyi mnastahili pongezi ya kiwango cha juu mo” akasema Dr Joshua
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais” akasema Kamanda wa polisi
“ Hata mimi nashukuru sana na kwa kuwa hivi sasa bado nimebanwa na mambo mengi nitakuita hivi karibuni ili tujadili kuhusiana na huyu Mathew.”
“ Hakuna shaka mzee.Muda wowote ukinihitaji utanipa taarifa”
“ Ahsante kamanda .Nakukumbusha vile vile kuwa leo ni siku ya mazishi ya mwanangu na kutakuwepo na wageni mbali mbali marafiki zangu wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo naomba suala la ulinzi lipewe kipaumbele kikubwa.”
“ Tayari nimekwisha toa maelekezo ya kuwepo kwa ulinzi wa kutosha eneo hilo kwa hiyo usihofu mheshimiwa “ akasema kamanda wa polis Dar es salaam wakaagana Dr Joshua akakata simu.
“ Lazima nimfanyie mambo makubwa huyu kamanda kwa namna alivyonisaidia katika suala hili.Kitakachofuata baada ya Elibariki kusafishika ni kuanza kumuandaa kwa ajili ya kushika madaraka makubwa.Najua kuna taratibu zake kwa mtu kama Elibariki ambaye ni jaji wa mahakama kuu kuingia katika mambo ya siasa lakini hilo si tatizo litakalonisumbua.
Elibariki kwa sasa tayari jina lake linafahamika,kwanza kama mhalifu na sasa anajulikana kama shujaa.Nitawaita wanamtandao wangu ili kwa pamoja tuanze kulijadili suala hili la kumuandaa Elibariki kwa nafasi ya urais” akawaza Dr Joshua.
“ Ngoja kwanza niachane na mambo haya ya jaji Elibariki,leo ni siku ndefu na ngumu.Ninamzika mwanangu Flaviana” akanyamaza na kuinamana na kuzama katika mawazo
“ Sikutegemea kama suala hili lingenifikisha hapa.Sikujua kama jambo hili lingewapoteza mke na wanangu.Hakuna wa kumlaumu kwa haya yote yaliyotokea,kwani ilikuwa ni lazima yatokee.Ninachopaswa kukifanya kwa sasa ni kuhakikisha lengo langu halikwami na ninafanikiwa kulimaliza suala la package .
Siko tayari kuyakosa mabilioni yale ya fedha ambayo tayari yametua mikononi mwangu.” Akawaza Dr Joshua halafu akaanza kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo.Wakati akijiandaa mara mlango ukagongwa,akatoka na kukutana na mwanae Anna
“ Anna,how are you my princess??
“ I’m fine dady” akajibu Anna na kuingia akateti sofani
“ Nashukuru umekuja Anna kwani nilikuwa natazamia kukuita asubuhi hii ili tuongee kuhusiana na siku ya leo” akasema Dr Joshua halafu akanyamaza kidogo akamtazama Anna aliyekuwa amesawajika sana na kuendelea
“ Leo ni siku nyingine ngumu kwetu kama familia.Tunakwenda kumpumzisha dada yako Flaviana.Its hard but we have to be strong.Anna nakuomba sana uwe jasiri siku ya leo”
“ I’m trying dady.Najaribu sana kuwa jasiri lakini najikuta nashindwa .Why this is happening to us? Why always us” Anna akasema huku akilia
“ Usilie Anna.Kila jambo hutokea kwa sababu maalum na kifo ni mapenzi ya Mungu.Hatuwezi kujua Mungu ana makusudi gani kutuchukulia wapendwa wetu wawili ndani ya kipindi kifupi.Hata kabla ya arobaini ya mama yako haijawadia,ametutoka tena dada yako.
Japo ni mapenzi ya Mungu na yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa lakini inauma sana” akasema Dr Joshua na kuinama akionyesha majonzi makubwa.Sekunde kadhaa za ukimya zikapita Anna akainua kichwa na kusema
“ Who will be next??.
Swali lile likamstua Dr Joshua
“ Umesemaje Anna?
“ Nimeuliza nani atafuata kati yetu? Alianza mama ,akafuata Flaviana na sasa tumebaki wawili mimi na wewe kwa hiyo nani atakayefuata? Akauliza Anna.Dr Joshua akamtazama mwanae kwa sekunde kadhaa akashidwa ampe jibu gani
“ kwa nini umeuliza hivyo Anna?
“ kwa sababu naona kama kuna kitu kinaiandama familia yetu na ndiyo maana najiuliza hivyo”
Ukimya ukatanda mle ndani.Baada ya muda Anna akasema
“ Anyway dady forget what I said. Mambo haya yaliyotokea yamenichanganya mno akili yangu.Kitu kikubwa kilichonileta hapa kwako asubuhi hii ni kutaka kufahamu kuhusu jaji Elibariki.Nimemuona uko naye jana usiku.What is he doing here? Kwa nini hakamatwi? Akauliza Anna
“ Mimi ndiye ninayepaswa kulaumiwa kwa kutokukufahamisha mapema kuhusu jaji Elibariki.There is an explanation” akasema Dr Joshua
“ Explanation? What explanation dady?? He killed my sister so what can you explain to me? Akauliza Anna
“ Calm down Anna.Umetazama taarifa ya habari leo asubuhi?
“ Hapana sijaitazama.Kuna nini ?
“ Basi kama ungekuwa umetazama tayari ungekuwa na jibu Elibariki siye aliyemuua Flaviana”
“ What ???!! Anna akashangaa
“ Ndiyo Anna,Elibariki siye aliyemuua Flaviana”
“ Dady I don’t understand what you are talking about. Jeshi la polisi walilithibitisha hilo na wakaanzisha msako wa kumsaka Elibariki ,nini kimetokea ?
“ Ukweli umebainika kwamba Elibariki alitekwa na watu wasiojulikana na kwenda kufichwa katika msitu wa Makenge.Lengo kuu la watu hao ni kujipatia fedha na ndiyo maana wakamtumia ili awasiliane na Flaviana wakapanga wakutane sehemu ambako wale majambazi walikuwa wamejipanga ili wamteke Flaviana.
Kwa bahati nzuri kulikuwa na walinzi wa siri ambao walikuwa wanamlinda Flaviana ambao walipambana vilivyo na majambazi hao na katika mapambano hayo Flaviana akajeruhiwa kwa risasi.Jana Elibariki alifanikiwa kuwaponyoka majambazi wale na kukimbia na mtu wakwanza kumpigia simu baada ya kutoroka alikuwa ni mimi.
Alinieleza kila kitu na mahala alipo nikampiga simu kamanda wa polisi kanda ya Dare s salaam nikamtaarifu kuhusu suala hili na usiku wa kuamkia leo polisi walivamia maficho ya majambazi hao na kufanikiwa kuwaua watatu na wawili wakakimbia.
Kwa sasa jeshi la plisi linawasaka majambazi yaliyokimbia pamoja na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Mathew ambaye ndiye mfadhili wao.Kwa maana hiyo basi jaji Elibariki hahusiki kabisa na kifo cha dada yako.” Akasema Dr Joshua wakabaki wanatamana.Anna akataka kusema kitu lakini mlango ukafunguliwa akaingia mlinzi wa rais
“ Mzee kuna mgeni wako amefika anakusubiri pindi ukimaliza maongezi”
“ Ni nani? Akauliza Dr Joshua
“ Abel mkokasule”
Dr Joshua hakutaka kupoteza muda akamtaka Anna aende akajiandae ili yeye apate muda wa kuongea na mgeni wake .Anna akatoka japo kwa shingo upande.
“ hallow Abel,karibu sana “ akasema Dr Joshua
“ Ahsante sana mzee.Samahani kwa kukuvamia asubuhi asubuhi namna hii.
“ Bila samahani Abel.I hope you have something for me this morning”
“ Ndiyo mzee” akajibu Abel
“ Tell me good news Abel..” akasema Dr Joshua huku akitabasamu
“ Tulipoachana jana usiku niliwapanga vijana wangu na tukaanza kazi mara moja.Kama ulivyoelekeza ,usiku huo huo tulianza kumfuatilia Dr Kigomba.Alipotoka hapa kwako,aliekea moja kwa moja kwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa Jacob kateka” akasema Abel.
“ Alikwenda kuonana na Jacob Kateka?..Dr Joshua akashangaa
“ Ndiyo mzee”
“ Alikwenda kumueleza kitu gani? Mlifanikiwa kunasa maongezi yao?
“ Hapana mzee hatukufaikiwa kunasa maongezi yao”
Taarifa ile ikaonekana kumchanganya kidogo Dr Joshua
“ Kama baada ya kutoka hapa alikwenda kuonana na Jacob basi lazima kuna jambo alikwenda kumueleza.Waliongea mambo gani? Naanza kuhisi lazima Kigomba atakuwa amemueleza Jacob kuhusiana na mpango wetu.Kigomba anaanza kudhihirisha ni kwa namna gani alivyo hatari kwangu.
Anafahamu mambo yangu mengi na anafahamu mipango yangu yote na ninahisi atakuwa na mipango ya siri ya kunivurugia mipango yangu.Natakiwa kufahamu kitu ambacho wawili hawa wanakipanga na kikubwa zaidi natakiwa kumshughulikia Kigomba haraka iwezekanavyo .
Endapo nitamuacha huyu jamaa basi lazima kuna jambo anapanga kulifanya.Na kama amemweleza Jacob basi lazima wawili hawa watakuwa wameungana na kupanga njama za kunihujumu.I’m going to deal with them “
“ Mr President..!!” Abel Mkosasule akamstua Dr Joshua toka mawazoni
“ Oh Samahani Abel kuna jambo nilikuwa nawaza.Ahsante sana kwa taarifa hii.Endeleeni kumfuatilia Kigomba kila aendako na kila anachokifanya kisha unipe taarifa.Nataka kufahamu watu anaokutana nao na kama ikiwezekana nataka kujua hadi kile wanachokiongea.
Kitu kingine ambacho kinaweza kuwasaidieni kumpata vizuri Kigomba ni kwamba ni mdhaifu mno kwa wanawake.Utumieni udhaifu huo kufanikisha kazi yenu” akasema Dr Joshua
“ Ahsante sana mzee kwa wazo hilo.Tutaendelea kumfuatilia Kigomba na nitakupa taarifa kamili jioni ya leo.Tukiachana na suala la Kigomba kuna kazi ulinipatia ya kumpata Jessica na kumpeleka Dark house.Napenda kukutaarifu pia kuwa alfajiri ya leo tumefanikiwa kumpata na tayari amepelekwa dark house tunasubiri maelekezo yako”
Dr Joshua akaachia tabasamu kubwa na kusema
“ Good Job Abel.Najuta kwa nini nisingekutumia wewe toka awali,ninsingefika hapa nilipofika”
“ Unasemaje mzee? Akauliza Abel
“ Oh sorry,forget what I said.Kazi nzuri sana umeifanya Abel .Endelea kumuweka Jessica Dark house hadi hapo nitakapokupa maelekezo mengine.Jioni ya leo nataka tuonane kuna kazi ambayo nataka uifanye.
Nilikudokeza kwamba kuna mtu yuko sehemu Fulani anashikiliwa kwa hiyo nataka mtu huyo akachukuliwe toka mahala hapo naye pia apelekwe dark house.Ni kazi ya hatari kidogo kutokana na mahala aliko huyo mtu kuwa ni sehemu yenye ulinzi mkali kwa hiyo waweke tayari vijana wako” akasema Dr Joshua
“ Usijali Dr Joshua.Vijana wako tayari kwa kazi muda wowote”
“ Ahsante sana Abel kwa taarifa nzuri.Nenda kaendelee na kazi na tutaonana hapa jioni ya leo.Nitakufahamisha muda nitakaokuwa na nafasi” akasema Dr Joshua na kuagana na Abel akaondoka
“ Dr Kigomba alikwenda kufanya nini nyumbani kwa Jacob usiku ule mwingi? Kuna kitu gani kinaendelea kati yao? Naanza kuhisi Kigomba kuna jambo analipanga na Jacob na lazima jambo lenyewe litakuwa ni kuhusiana na ile package.
Ngoja kwanza nimalize shughuli za msiba wa mwanangu halafu nitaamua niwafanye nini lakini wakae wanajua kwamba kama wana mipango yoyote mibaya juu yangu wanajisumbua bure kwani hawatafanikiwa .Kushindana nami ni sawa na kushindana na moto wa nyika..
Mimi ndiye raia namba moja hapa nchini na kila kitu kipo ch…..” Mlio wa simu ukamstua Dr Joshua akaichukua na kutazama mpigaji.Alizifahamu namba zile ni namba za zamani za Dr Kigomba
“ Hallow Kigomba” akasema Dr Joshua
“ Mr President habari za asubuhi ?
“ Habari nzuri Kigomba.Kuhusu ile simu yako nataka kuikabidhi kwa vijana wetu wa usalama waifanyie uchunguzi na kubaini kama kweli imeunganishwa halafu utarejeshewa.Habari za toka jana?
“ Habari nzuri mheshimiwa rais.Nitashukuru sana mzee kama nitarejeshewa simu yangu kwani watu wengi wanaifahamu ile namba wananitafuta na kunikosa” akasema Dr Kigomba na kunyamaza kidogo halafu akasema
“ Dr Joshua kuna jambo limenistua na ndiyo maana nimekupigia simu.Nimekuja katika hii hoteli ambako Hussein na ujumbe wake walifikia kwa lengo la kutaka kuhakikisha wako salama lakini kitu cha kushangaza Hussein na ujumbe wake wamehamishwa alfajiri ya leo.Unafahamu chochote kuhusu jambo hili? Akauliza Dr Kigomba
“ Ndiyo ninafahamu Kigomba na mimi ndiye niliyetoa maelekezo hayo”
Kupitia spika za simu Dr Kigomba akasikika akishusha pumzi.
“ Kigomba kuna tatizo lolote kwani? Akauliza Dr Joshua
“ Hakuna tatizo Dr Joshua kama wamehamishwa kwa amri yako.Naweza ukaniambia wamehamishiwa wapi?
“ No I cant tell you now.” Akasema Dr Joshua na kuzidi kumkasirisha Dr Kigomba
“ Dr Joshua whats going on? Kwa nini unanificha na hutaki kunieleza kitu gani kinachoendelea ? Don’t you trust me?
“ Kigomba nimekwisha kueleza kwamba subiri kwanza tuyamalize masuala ya msiba halafu tutakaa na nitakueleza kila kitu kinachoendelea.Do you understand me Kigomba? Akauliza Dr Joshua.
“ Yes I do” akajibu Dr Kigomba
`
“ Good.Now come over here.I’m waiting for you.Shughuli zinatakiwa kuanza mapema” akasema Dr Joshua na kukata simu
“ Damn ! you Joshua.Unajifanya wewe una akili sana basi nitakuonyesha namna ulivyo mjinga!!.akawaza Dr Kigomba akiwa garini akielekea kwa Dr Joshua .Akachukua simu na kumpigia Jacob Kateka.
“ Habari za asubuhi Dr Kigomba? Akauliza Jacob baada ya kupokea simu
“ Habari nzuri Jacob.Nimekupigia simu kukufahamisha kuhusu sarakasi za Yule mtu wetu,Nimetoka katika hoteli niliyokuwa nimewatafutia Hussein ana ujumbe wake,nimekuta wameamishwa hoteli alfajiri ya leo.
Nimempigia simu Dr Joshua nikamuuliza kama analifahamu jambo hili akasema kwamba ni yeye aliyetoa amri ya kuwahamisha Hussein na ujumbe wake na amegoma kabisa kunieleza mahala alikowahamishia.Zote hizi ni harakati zake za kutaka kuniengua katika mpango wetu na kumiliki kila kitu mwenyewe.
Nitakuja kuonana nawe jioni ya leo ili tupange mikakati mizito nini tufanye” akasema Dr Kigomba akaagana na Jacob Kateka kwa miadi ya kuonana jioni.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…