Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

PENIELA

SEASON 4

EPISODE 10

MTUNZI : PATRICK.CK



ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Oh my God this is a miracle !!!!...Anitha !! akasema Mathew kwa mshangao

“ Is that real her?? Akajiuliza huku akimtazama tena kwa makini

“ Its her.Ni Anitha…She’s not dead.Amejuaje kama tuko hapa? Akajiuliza Mathew halafu akatoka mbio na kumfuata Peniela .
Kama ilivyomtokea Mathew ,ndivyo ilivyomtokea pia Peniela ,alistuka sana .Hakuamini alichokiona
“ Oh my Gosh ! This is a miracle..She’s alive !! akasema Peniela kwa furaha huku akiruka ruka.
“ What are you waiting Mathew? Go get her in” akasema Peniela.

“ Lazima tuchukue tahadhari .Yawezekana akawa anatumiwa na watu .We must be very carefull” akasema Mathew halafu akachukua bastora na kuelekea getini.Taratibu akafungua mlango mdogo wa geti na kuruka nje kama kima huku akielekeza bastora pande zote kujihami endapo kuna adui

“ Don’t shoot ! Its me Anitha” akasema Anitha

“ Anitha !! akasema Mathew baada ya kuhakikisha Anitha alikuwa peke yake
“ Mahew !! akasema Anitha wakakumbatiana kwa furaha.


ENDELEA………………..



“ Oh my angel you are back!! You are alive !! akasema Mathew.Anitha alikuwa anatokwa na machozi mengi ,alionekana mchovu na alikuwa na michubuko mingi iliyosababishwa na mateso aliyoyapata nyumbani kwa Rosemary Mkozumi.

“ What happened to you Anitha? Akauliza Mathew akimtazama Anitha .
“ Mathew fungua kwanza geti tuingie ndani tutaongea vizuri,” akasema Anitha na kwa haraka Mathew akafungua geti Anitha akaingiza gari ndani .Tayari Peniela alikwisha toka ndani na mara tu Anitha aliposhuka garini akamkumbatia kwa furaha kubwa huku wote wawili wakitokwa na machozi

Anitha akakaribishwa ndani na kabla ya yote Peniela akampeleka bafuni ambako alioga ,akasafishwa majeraha yoye aliyoyapata halafu akampeleka katika chumba apumzike.Mathew akaja na kisanduku kidogo cha dawa ambacho ni miongoni mwa vitu walivyopewa na askofu Edmund.Akakifungua na kuanza kumganga Anitha majeraha yake yote.Kisha mtibu majeraha yake akamchoma sindano huku Peniela akishangaa
“ Sikujua kama una taaluma ya mambo haya ya tiba” akasema .Mathew akatabasamu kidogo na kusema
“ Katika hizi kazi zetu lazima ufahamu mambo mengi na suala la tiba ni moja ya mambo ambayo lazima kuyafahamu.Kwa sasa tumuache Anitha apumzike twende jikoni tukaangalie kitu cha kumuandalia,she looks so weak.Huko alikokuwa sina hakika kama amekula hata chakula” akasema Mathew
“ No Mathew,we have to talk now.Mimi nimewapata ninyi sina wasi wasi tena.Nimepata nguvu kubwa” Akasema Antha

“ Anitha pumzika tutaongea baadae”
“ Hapana Mathew hatuwezi kusubiri.Something big is going on.I have to tell you whats going on”
Mathew na Peniela wakatazamana

“ Whats going on Anitha? What real happened? Where were you? Umefahamuje kama tuko hapa? Akauliza Mathew.Anitha akainuka na kuketi ,akafumba macho kidogo kwa maumivu makali akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ni hadithi ya kusikitisha sana na kila kitu kilianzia usiku ule wewe na Peniela mlipoondoka kwenda nyumbani kwa Peniela.Nilikuwa peke yangu ofisini na mara akaja jaji Elibariki tukaongea kidogo akasema kwamba anakwenda kuniandalia kahawa,na muda huo huo ukanipigia simu na nilipopokea tu nikapigwa na kitu kizito nikapoteza fahamu” akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Nilipozinduka nikajikuta katika chumba chenye giza na baadae nikafahamu kwamba pale ni nyumbani kwa Rosemary Mkozumi”
“ Rosemary Mkozumi??? Is she alive?akauliza Mathew kwa mshangao

“ Yes she’s alive.Rosemary alikuja katika chumba nilichokuwa nimefungwa akanitaka nimueleze mahala ulipo kama ninataka nibaki hai.Sikuwa tayari kufanya alivyotaka .Alimtuma mmoja wa walinzi wake akamlete mtu Fulani na sikuamini macho yangu nilipomuona mtu aliyeletwa ni jaji Elibariki”
“ Elibariki ??? !!..Mathew na Peniela wote wakauliza kwa mshangao mkubwa
“ Hata mimi nilishangaa sana kumuona Elibariki akishirikiana na Rosemary Mkozumi .Inaonekana walikuwa na makubaliano Fulani kwani Rose alimwambia Elibariki endapo anataka amuamini basi adhihirishe hilo kwa kunipiga risasi ,akapewa bastora akanilenga kichwani akaizinga lakini kumbe bastora ile haikuwa na risasi.Endapo bastora ile ingekuwa na risasi Elibariki alikuwa tayari kuniua. ” akasema Anitha kwa uchungu huku machozi yakimtoka.Peniela ambaye naye machozi yalikuwa yanamtoka akamsogelea Anitha akamfuta machozi .
“ This is unbelievable ..Elibariki ??? Akasema Mathew .Anitha akaendelea
“ Elibariki alitusaliti na akaamua kushirikiana na Rosemary mkozumi” akasema Anitha

“ Baada ya hapo nikaingizwa katika chumba cha mateso”
“ Ndani ya jumba la Rose kuna chumba cha kutesea watu?
“ Ndiyo Mathew.That house is like hell .Kuna chumba cha mateso ambacho kina kila kifaa cha kutesea.Vile vile kuna mtu maalum ambaye kazi yake ni kutesa watu anaitwa Fernando.Walinitesa mno wakitaka niwaonyeshe mahala ulipo lakini sikuthubutu kufungua mdomo wangu.” Akasema Anitha akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Leo asubuhi niliingizwa tena katika chumba cha kutesea ,wakanitesa mno hadi nikalazimika kujifanya nimepoteza fahamu lakini bado Rosemary Mkozumi hakuridhika akamwambia Fernando aendelee kunitesa hadi nitakaposema Mathew yuko wapi.Baadae Fernando alinifuata akanieleza kwamba alitaka kunifahamu mimi ni nani.Alionekana kunionea huruma .Nilipomtazama niligundua ni mtu mwepesi kushawishika.Nilitumia mbinu ya kumshawishi kwa fedha na akakubali .Nilimwambia atafute kompyuta iliyounganishwa na intanet akaniletea na nikaitumia teknolojia ya benki bandia kumuhamishia fedha katika akaunti na akaamini baada ya kupokea ujumbe uliomtaarifu kwamba kiasi cha fedha kimetumwa katika akaunti yake.Fernando aliridhika akanitorosha .Baada ya kutoka katika makazi ya Rose nilimulekeza tuelekee katika duka la mavazi akanichagulie mavazi .Wakati akiwa dukani nikatokomea na gari lake” akasema Anitha

“ Dah ! pole sana Anitha” akasema Mathew

“ Ahsante Mathew” akajibu Anitha.Ukimya mfupi ukapita halafu akaendelea.
“ Nilikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwako na kukutana na kitu cha kusikitisha .Hakukuwa na nyumba tena bali majivu.Nyumba ilikuwa imeteketea .Nimewakuta polisi wakifanya uchunguzi wao.Nilichanganyikiwa nikashindwa nifanye nini nikaondoka.Baadae nikapata wazo nikazikumbuka zile pete tulizowahi kuwa nazo.Mimi yangu ilipotea lakini wewe bado unayo
" Mathew akastuka na kutazama vidoleni.Ni kweli katika mkono wake wa kulia alikuwa na pete kubwa ya dhahabu .Anitha akatabasamu

“ Kwa kutumia kompyuta ya Fernando iliyokuwamo mle garini nilianza kuitafuta pete hiyo kwa kutumia satellite na nikafanikiwa kuipata.Kwanza niliiona maeneo ya Kigamboni na baadae ikaondoka nikaendelea kuifuatilia hadi ikafika hapa.Teknolojia imefanikisha tumeweza kuonana tena japo haikuwa rahisi kutokana na intaneti kuwa na kasi ndogo mno”

“ Pole sana Anitha” akasema Peniela
“ Ahsante Penny.Hiyo ndiyo hali halisi ilivyokuwa.Hayo ndiyo mambo yaliyonikuta.Mtu ambaye tulimuamini na kuyaweka rehani maisha yetu kwa ajili yake ametugeuka na kutusaliti.” akasema Anitha.
Mathew alihisi mwili unamtetemeka kwa hasira alizokuwa nazo.Hakuweza kuongea chochote akabaki amejiinamia akiwaza

“ Mathew say something” akasema Peniela

“ I don’t know what to say.Hizi ni taarifa mbaya mno ambazo sikuwa nimetegemea kuzisikia.Sikutegemea kabisa mtu kama Elibariki angeweza kutufanyia sisi kitu kama hiki.Nilimuamini kupita kiasi na ndiyo maana nimestuka sana kusikia kitu alichokifanya.” Akasema Mathew na kuzama katika mawazo mengi
“ Kwa nini jaji Elibariki afanye jambo kama hili? Ni yeye aliyetuomba tufanye kazi yake ya kumtafuta muuaji wa Edson kwa nini basi abadilike na kutufanyia hivi? Nakosa majibu ya maswali haya kwani Elibariki anafahamu ni kitu gani kinachoendelea na kitu gani tunachokipigania,kibaya zaidi amediriki kumuachia huru na kushirikiana na Rosemary Mkozumi ambaye anafahamu wazi kuwa anashirikiana na magaidi.Kwa nini Elibariki????? Akajiuliza Mathew huu mwili ukizidi kuchemka kwa hasira.

“ Kwa upande wenu nini kilitokea? Imekuwaje hadi mkafika hapa? Hii nyumba ya nani? Akauliza Anitha

“ Usiku ule” akasema Mathew
“ Tulikwenda kwa Peniela ambako aliwasiliana na Dr Joshua kisha tukaanza safari ya kurudi .Sikutaka Peniela abaki peke yake pale nyumbani kwake nikamtaka turudi wote nyumbani kwangu,Tukiwa njiani ukatutaarfu kwamba kuna simu ya Peniela .Aliyempigia simu ni kijana mmoja anaitwa Josh ambaye alikuwa mlinzi wa John Mwaulaya.Josh alimtahadharisha Peniela kwamba kuna watu wa Team SC41 wametuwa kumfuatilia kwa hiyo achukue tahadhari.Ni kweli tuligundua kwamba kuna watu walikuwa wanatufuatilia na hapo ndipo mapambano makali yakatokea.Tulipambana sana tukafanikiwa kuwaponyoka wale jamaa waliokuwa wamejiandaa kwa lengo la kumpata Peniela.Nahisi tayari walikuwa na wasi wasi na nyendo zake na ndiyo maana walianza kumfuatilia. Nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi hivyo tukataka kurejea nyumbani kwa Peniela nikatibu jeraha lililokuwa linatoa damu nyingi lakini tulipofika tukakuta moto mkubwa unaiteketeza nyumba ya Peniela .Mpaka sasa hautujui nani alifanya kitendo kile lakini tunahisi lazima watakuwa ni team SC41.Ilitulazimu kuomba msaada toka kwa Jason tukaelekea hadi nyumbani kwangu ambako nako tulikuta tukio kama tulilolikuta kwa Peniela.Nyumba yangu ilikuwa inateketea kwa moto.Hatukuwa na namna nyingine ya kufanya ikanilazimu kumtafuta askofu Edmund Dawson” akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Kabla ya kifo chake ,John Mwaulaya alizungumza nami.Nyote mnafahamu kwamba mimi na John Mwaulaya ni maadui wakubwa kutokana na kitukibaya alichonifanyia na nilikubali kwenda kuonana naye kwa sababu ya Peniela.Katika muda mfupi tulioongea alinileza mambo kadhaa mazito ambayo nitawaeleza hapo mbeleni lakini kubwa zaidi alinitaka kwa gharama zozote zile nimlinde Peniela na nihakikshe namfikisha kwa askofu Edmund Dawson.Alinipa namba za siri za kuwasiliana na Edmund na alinitaka niwasiliane naye mara tu nitakapokamilisha zoezi la kukipata kirusi Aby.Alinisisitiza kwamba kwa gharama yoyote ile lazima nihakikishe ninakipata kirusi Aby.Alinionya nisikubali katu kirusi kile kiingie mikononi mwa team Team SC41 au kwa watu ambao wanataka kukinunua toka kwa Dr Joshua kwani litakuwa ni angamizo la dunia.Niliamua kuwasiliana na Edmund mapema kabla hata ya kulikamilisha zoezi lile la kukipata kirusi Aby kwa sababu hatukuwa na namna nyingine ya kufanya na tulihitaji msaada .Edmund Dawson anafanya kazi na shirika la ujasusi la Marekani C.I.A na yuko hapa nchini kwa kazi maalum ya kumchunguza Chin sun ambaye ni mke wake. Edmund na John Mwaulaya walikuwa ni marafki wakubwa na wa siri,na ndiye aliyetusaidia kila tulichokihitaji pamoja na nyumba .Kwa ufupi hicho ndicho kilichotokea kwa upande wetu .Namshukuru sana Mungu ametukutanisha tena Anitha.Nilichanganyikiwa na sikujua ningekuliliaje endapo ungekuwa mepoteza maisha.Ouh Anitha give a big hug !! ” akasema Mathew na kukumbatiana na Anitha kwa furaha,Peniela naye akaungana nao wakakumbatiana wote .

“ Kwa hiyo kitu gani kinachoendelea hivi sasa ? akauliza Anitha.
“ Bado kazi yetu ya msingi ni kuhakikisha tunakipata kirusi Aby.Kwa vyovyote itakavyokuwa ni lazima tuhakikishe tumekipata kirusi hicho.John Mwaulaya alinisisitiza mno jambo hili.Viongozi wakuu wa Team SC41 wanataka kukipata kirusi hicho kwa ajili ya kukiachia hapa Tanzania.”

“ Tanzania ?? akasema Peniela kwa mshangao

“ Ndiyo wanataka kukitumia nchini Tanzania”

Peniela na Anitha wakatazamana.Taarifa zile ziliwastua sana,Mathew akaendelea

“ Wakati wakifanya utafiti wa mafuta na gesi katika kina kirefu cha bahari,watafiti wa kampuni ya mafuta na gesi ya Solenergy ya Marekani waligundua uwepo wa madini aina ya Gramonite ambayo ni madini yenye thamani kubwa kuliko madini mengine yote tunayoyafahamu .Baada ya ugunduzi huo kampuni hiyo haikutaka kutoa taarifa za uwepo wa madini hayo kwa serikali ya Tanzania na mpaka leo hii serikali ya Tanzania haifahamu chochote kuhusu uwepo wa madini hayo ya thamani kubwa chini ya bahari.Taarifa hizi ziliwasilishwa kwa siri kwa serikali ya Marekani nao wakaanza mikakati itakayowawezesha kuyapata madini hayo.Njia pekee na rahisi ambayo wangeweza kuitumia na ambayo imefanikiwa sehemu nyingi afrika ni kwa kuanzisha migogoro ya ndani ya nchi.Walianza kuwatumia wanasiasa ili wapandikize chuki miongoni kwa watanzania na kuchochea machafuko lakini njia hiyo ilishindwa japokuwa nchi ilitikisika.Walijaribu kutumia njia ya kupandikiza chuki za dini lakini pia njia hii haikufanikiwa na ndipo walipoikabidhi kazi hiyo kwa team SC41 ili waweze kukipata kirusi hicho na kukisambaza kwa lengo la kusababisha maangamizi makubwa.Wakati nchi ikiwa katika taharuki wao watakuja kama wafadhili na wakati huo huo kuchimba na kuondoka na kiasi kikubwa kama si chote cha madini.Huu ni mpango wa siri kubwa sana na John mwaulaya ni miongoni mwa watu wachache sana waliobahatika kuufahamu na ndiyo maana akanisisitiza kwamba tuhakikshe Team SC41 hawakipati kirusi hicho.Endapo tutashindwa na team Sc41 wakafanikiwa kukipata nchi yetu itashuhudia maangamizi makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa.Kila nyumba itakuwa na msiba na hakutakuwa na wa kumzika mwenzake.Maelfu kwa maelfu ya watu watateketea ndani ya muda mfupi kwa hiyo ndugu zangu tuna jukumu zito la kuhakikisha tunakipata kirusi hicho kwa gharama zozote zile.Tunatakiwa kuja na mikakati mizito ya namna ya kukipata kirusi hicho kabla Dr Joshua hajakikabidhi kwa Hussen ambaye ndiye mnunuzi na tayari amekwisha fika kwa ajili ya kukichukua “ Mathew akawatazama wanawake wale wawili ambao nyuso zao zilionyesha woga mkubwa.
“ Mara ya mwisho” akaendelea Mathew
“ Taarifa iliyokuwa mezani kwetu ni kwamba siku ya leo yatafanyika makabidhiano ya kirusi Aby na Dr Kigomba ndiye anayetakiwa kumkabidhi Hussein kirusi hicho kwa hiyo basi mtu pekee ambaye anaweza akatukuongoza katika kukipata kirusi hicho ni Dr Kigomba.Kama mtakumbuka tayari simu yake ilikuwa imeunganishwa katika mifumo yetu na vile vile tulimpa saa ambayo nayo iliunganishwa na mifumo yetu na tulikuwa na uwezo wa kufuatilia na kujua kila mahala aliko lakini kwa kuwa kila kitu kiliteketea Anitha una jukumu la kurudisha tena mifumo yote iliyopotea na tuanze tena kumfuatilia Kigomba.Hilo linawezekana? ” Akauliza Mathew
“ Ndiyo inawezekana Mathew lakini tunahitaji kupata kompyuta mpya yenye uwezo mkubwa na kasi.Kompyuta hii ya Fernando haitaweza kumudu program zile kwani uwezo wake ni mdogo.”
“ Ok hilo halina shaka.Tutapata kompyuta hiyo.Itatulazimu kwenda katika maduka yanayouza kompyuta pamoja na kufanya manunuzi ya vitu vingine ambavyo tutavihitaji humu ndani.Mimi na Peniela tutakwenda na wewe Anitha utabaki hapa unapumzika.Usihofu hapa ni sehemu salama”
“ Mathew are you sure you are going to be safe out there? Akauliza Anitha kwa wasi wasi
“ Usihofu Anitha,I’ll be fine” akasema Mathew

Anitha akampa orodha ya vitu ambavyo anavihitaji halafu Mathew na Peniela wakaingia katika mojawapo ya magari yaliyokuwapo hapo wakaondoka kuelekea madukani kufanya manunuzi
“ Bado naona ni kama muujiza kuonana tena na Anitha.Sikutegemea kabisa” akasema Mathew wakiwa garini.

“ Hata mimi sikutegemea kabisa.Nilijua lazima wote waliteketea kwa moto.Lakini kuna mtu mmoja ambaye Anitha hajatueleza yuko wapi ? Naomi.Naye alikuwemo mle ndani usiku ule.Where is she?
“ Nina hakika lazima Rosemary alimchukua.Simuhofii Naomi bali jaji Elibariki.Yule alikuwa nasi toka awali na anafahamu kila tulichokipanga.Kama ameamua kutusaliti na kumfungua Rosemary Mkozumi basi hatasita kuanika mipango yetu yote .Kitu ambacho nashindwa kupata jibu lake ni kitu gani kimembadilisha Elibariki ghafla namna hii na kumshawishi afanye hivi alivyofanya? Kwa nini atufanyie hivi wakati huu ambao tumekaribia kabisa kufanikisha operesheni yetu? Kuna jambo gani baya tumemkosea akaamua kututenda hivi? Where is he now? Akasema Mathew
“ Kweli nimeamini kikulacho ki nguoni mwako.Angetufanyia hivi mtu mwingine ningeweza kumsamehe lakini Elibarki !!! I’ll never forgive him.Tulimchukulia ni mwenzetu kumbe ni chui katika kundi la kondoo.Noah rafiki yangu alipoteza maisha wakati akimuokoa asiuawe lakini yote haya ameyasahau.” akasema Mathew kwa hasira

“ Kokote aliko lazima nihakikishe ninamsaka na kumpata.hata kama si leo wala kesho lakini nitamsaka hadi siku ninaondoka katika dunia hii.Kwa sasa amekuwa ni adui yangu mkubwa .Usalti alioufanya ni mkubwa mno na hauvumiliki hata kidogo. Ameifanya kazi yetu kuwa ngumu zaidi.Kutokana na jambo aliolifanya jaji elibariki hatuwezi tena kuendelea na mipango yetu ya awali kwani hatujui lengo la kutufanyia hivi ni nini:” akasema Mathew

“ Unashauri tufanye nini Mathew? Akauliza Peniela aliyekuwa katika usukani.Mathew akainama akazama mawazoni.
“ Unawaza nini Mathew? Akauliza Peniela .Bado Mathew aliendelea kuinama na hakujibu chochote.Safari ikaendelea kimya kimya.Kichwa cha Mathew kilijaa mawazo mengi

“ Lazima anafikiria kitu kikubwa sana.Ngoja nimuache aendelee kuumiza kichwa ili kufikiri kitu tutakachokifanya kwani sisi sote tunamtazama yeye” akawaza peniela


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
Yyyg
tutghttp://
 
Yaani nahisi wewe hukereki kama mimi. Mtu anakopi story episode nzima as if aki-comment tu bila kukopi hatutamuelewa.

Kama unatumia cm, usitumie app ya jf, ingia tu kupitia browser unayotumia, hao wanaoquote episode nzima hawatakusumbua.
 
Back
Top Bottom