ENDELEA SEASON 5
SEHEM YA 1
“ Dr Joshua “ akasema Donald baada ya chumba
kutawaliwa na ukimya
“ Baada ya kukueleza suala la pili lililonileta hapa,
sasa turejee katika suala la kwanza.” Akasema Donald
“ Sawa endelea” akasema Dr Joshua
“ Awali nilikueleza kwamba tayari tumekwisha fanya
mipango yote ya kumuua Andrew Rodney na Deus Mkozumi
na kazi hiyo itafanywa na Alqaeda na litaonekana ni
shambulio la kigaidi.Serikali ya Tanzania wala Marekani
hazitahusishwa kabisa na tukio hilo badala yake nchi zote
zitaulaani kwa nguvu mtandao wa Alqaeda kwa kitendo
hicho.” Donald akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Ili kuutekekeleza mpango huo,Alqaeda wametoa
masharti mawili.Sharti la kwanza tumuachie huru mmoja wa
watu wao muhimu ambaye tunamshikilia katika mojaya
magereza yetu.Hilo tayari tumelikubali na tutamuachia huru
kiongozi wao.Sharti la pili kuna kiongozi wao muhimu sana
anashikiliwa nchini Saudi Arabia ambaye wanataka
aachiwe.Serikali ya Saudi Arabia haiku tayari kumuachia
kiongozi huyo kwa hiyo Alqaeda wanataka kuilazimisha
serikali ya Saudi Arabia kumuachia kiongozi wao na hilo
wataklifanya kutokea hapa nchini Tanzania”
“ Tanzania tena??!!...Dr Joshua akauliza
“ Ndiyo .Wanataka jambo hilo lifanyikie hapa
Tanzania” akasema Donald na kukawa kimya.Mara mlango
ukagongwa Dr Joshua akaenda kuufungua.Alikuwa ni mmoja
wa walinzi wake
“ Unasemaje Peter?
“ Mzee kuna kitu kimetokea hapa nyumbani sasa
hivi”
“ Kitu gani? akauliza Dr Joshua kwa wasi wasi
“ Kuna mwanamke mmoja amefika hapa anasema
anaitwa Peniela na anadai kwamba anaishi hapa na
anakufahamu na wewe ndiye uliyemruhusu aishi hapa”
Mwili wa Dr Joshua ukastuka kama vile umepitiwa na
chaji za umeme
“ Peniela ???..where is she? Akauliza
“ Yuko nje tunamshikilia”
“ Muachieni haraka aingie ndani ila mpitishe kwa
mlango wa nyuma aende moja kwa moja chumbani kwake
na asiruhusiwe kutoka hadi nitakapomaliza maongezi na
mgeni wangu”akaamuru Dr Joshua
“ sawa mzee” akajibu Peter na kuanza kuondoka Dr
Joshua akamuita
“ Peter sitaki jambo hili alifahamu mtu mwingine
zaidi ya ninyi mlioko hapa.Kuhusu wale polisi pale getini
tafuta namna yoyote ya kuwadanganya .Tell them she’s my
relative or anything.”
“ Sawa mzee nitafanya hivyo” akajibu Peter kwa
adabu
“ Another thing,umewasiliana na Kareem? Akauliza
Dr Joshua
“ Ndiyo mzee nimewasiliana naye ameniambia
kwamba yuko maeneo ya kule msibani”
“ Ok Good” akasema Dr Joshua na Peter akaondoka
“ Peniela !!!.Finaly I’ve got her...” akawaza Dr Joshua
huku akihisi mwili unamtetemeka kwa ndani kiasi cha
kumshangaza hata yeye mwenyewe ...
“ Sijui kwa nini kila ninapolisikia jina Peniela,mwili
wote hunitetemeka.Ngoja kwanza nimalize maongezi na
Donald halafu nitakwenda kuonana naye nifahamu kitu gani
kilichomleta hapa.Nashukuru amejileta mwenyewe ,nilikuwa
naumiza kichwa ningempata wapi.Nilikwisha sahau kabisa
kama nilimkabidhi nyumba hii aishi.” Akawaza Dr Joshua
aliyekuwa amesimama karibu na mlango mara akastuliwa na
Donald
“ Dr Joshua kuna tatizo lolote limetokea? Mbona
umebadilika ghafla?
“ Oh hapana Donald…Tuendelee na maongezi
yetu.Tuliishia wapi?
“ Nilikueleza kwamba Alqaeda wana kiongozi wao
anayeshikiliwa nchini Saudi Arabia na wanataka kuishinikiza
serikali ya Saudi Arabia imuachie huru na jambo hilo
litafanyika kutokea hapa Tanzania” akasema Donald
“ Naomba unifafanulie vizuri Donald.Wanataka
kufanya nini kuishinikiza serikali ya Saudi Arabia imuachie
kiongzo wao? Akauliza Dr Joshua ambaye macho yake
yalionyesha wazi alikuw ana wasi wasi mwingi
“ Binti mfalme wa Saudi Arabia aitwaye Salhat
Abdullah atatembelea Tanzania kwa mwaliko wa rafiki yake
ambaye ni Dr Lucia Mkozumi .Salhat na Dr Lucia wanafanya
kazi pamoja katika shirika la fedha la umoja wa mataifa kwa
hiyo ni marafiki wakubwa.Binti mfalme huyo ambaye
anapendwa mno na baba yake atakapofika hapa Tanzania
atatekwa nyara na atatumika katika kuishinikiza serikali ya
Saudi Arabia imuache kiongozi wa Alqaeda ili Salhat aachiwe
huru.Kwa jinsi Salhat anavyopendwa na baba yake lazima
atakubaliana na matakwa ya Alqaeda tu.”akasema Donald
“ Wanataka kumteka mtoto wa mfalme? Hebu
nifafanulie Donald watafanyaje hilo? Mbona mambo mengi
yanataka kutokea hapa nchini ndani ya kipindi kifupi?
“ Mpango mzima uko hivi.Lucy ambaye ndiye
aliyemualika salhat kuja hapa nchini ataongozana naye hadi
katika jengo la biashar ala Dar city shopping mall kwa lengo la
kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali kwa ajili ya kupeleka
zawadi katika vituo vya watoto wanaoishi na virusi vya
ukimwi kwani Salhat anayo taasisi yake inayojishughulisha na
kuwahudumia watoto wa aina hiyo .Katika msafara huo Dr
Lucia anapaswa kuhakikisha kuwa baba yake Deus Mkozumi
anaambatana nao .Wakati manunuzi yakiendelea Lucia
atampeleka Salhat katika duka moja linalouza
vinyago..Atakapofika huko Alqaeda watalivamia jengo hilo
na kuwachukua mateka Dr Lucia na Salhat na hapo ndipo
Deus Mkozumi atakapouawa”
Dr Joshua akatoa kitambaa na kujifuta jasho lililoanza
kumtoka usoni.Alihisi joto kutokana na mambo mazito
aliyoelezwa na Donald
“ Nini kitafuata baada ya hapo? Akauliza Dr Joshua
kwa wasi wasi
“ Dr Lucia Mkozumi ataachiwa huru,Salhat
ataendelea kushikiliwa na magaidi na ili aachiwe huru
watashinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wao kwanza”
akasema Donald
“ Itakuaje endapo madai yao yasipotimizwa? Akauliza
Dr Joshua
“ Ikitokea kwamba madai yao yasipotimizwa
wataondoka na Salhat na itakulazimu kuwasaidia kuondoka
hapa nchini lakini kwa utafiti uliofanyika tunaamini lazima
madai yao yatatekelezwa kwani mfalme anampenda mno
mtoto wake.Kiongozi wao atakapoachiwa huru watamuachia
Salhat na watapotea zao”
Dr Joshua akafikiri kidogo halafu akasema
“ Nina wasiw asi katika shambulio hilo litakalofanyika
Dar city shopping mall,watu wasio na hatia watapoteza
maisha yao.”
“ Ni kweli hilo unalolisema Dr Joshua na haliwezi
kuepukika.Lazima watu wapoteze maisha .Nadhani
unafahamu namna mashambulizi ya kigaidi
yanavyokuwa,lazima idadi kadhaa ya watu wapoteze maisha”
“ Naogopa sana Donald kusema chochote kwa sasa
hasa nikivuta picha ya watu wasio na hatia wakiwa wamelala
chini hawana uhai...Inaniogiopesha sana.Damu ya watu hao
wasio na hatia itatuandama sisi tuliosaidia kufanikisha
shambulio hilo.” Akasema Dr Joshua
“ Usiogope Dr Joshua.Kazi ya urais ni ngumu na kuna
nyakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu sana kwa
maslahi mapana ya nchi.Wakifa watu kumi au ishirini si kitu
kwani kuna mamilioni ya watu waishio vijijni watakwenda
kunufaika na huduma za maji,afya,elimu,kilimo n.k.Kwa hiyo
usiogope Dr Joshua kufanya maamuzi kwani maamuzi
utakayoyafanya leo yanaakisi maendeleo makubwa kwa
Tanzania kwa miaka mingi ijayo.Nakuhakikishia Dr Joshua
baada ya miaka kumi Tanzania hii uionayo sasa haitakuwa
kama unavyoiona leo.Itakuwa na mabadiliko makubwa mno
lakini haya yote yanategemea maamuzi utakayoyafanya
kuhusu suala hili” akasema Donald.Dr Joshua akainamisha
kichwa akiwaza na baada ya muda akasema
“ Dr Lucia Mkozumi anafahamu kuhusiana na baba
yake kutakiwa kuuawa ?
“ Anafahamu kila kitu na ameshiriki katika kuandaa
mpango huo.Dr Lucia mkozumi hafahamiki kabisa hapa nchini
na tukio hili litachangia sana katika kumtangaza.Dunia yote
watamfahamu yeye ni nani ndani ya kipindi kifupi sana na
atakapotangaza kuwania urais wa Tanzania haitakuwa kazi
ngumu kumnadi.Dr Joshua kila jambo lina sadaka yake na Dr
Lucia Mkozumi yuko tayari kwa lolote ili aweze kuupata urais
wa Tanzania” akasema Donald..Dr Joshua akakosa neno la
kusema
“ Dah ! huyu Lucia lazima atakuwa ni mwanamke
mwenye roho ngumu sana.Kama kweli amekubali baba yake
auawe na magaidi basi ni mwanamke anayefaa kabisa kuwa
rais kwani urais unahitaji mtu mwenye kuweza klufanya
maamuzi magumu kama aliyofanya Dr Lucia.She’s a monster
just like me.Lakini hata hivyo siwezi kuukataa mpango huu
kwani umekuja kwa wakati muafaka kabisa.Kwa muda mrefu
nimekuwa nkitafuta namna ya kumuondoa Deus Mkozumi
kwani amekuwa akiingilia sana mambo yangu na sasa nafasi
hiyo imejitokeza na siwezi kuiacha.Nitaitumia fursa hiyo
kumuondoa si Deus Mkozumi peke bali na mke wake
Rosemary Mkozumi.I hate that woman so much.Najua
atakuwa ni kikwazo kikubwa kwangu kufanikisha mambo
yangu .Lazima nimuondoe haraka sana Yule mwanamke ili
mpango huu usiingiliwe na kikwazo chochote”
“ Dr Joshua !!” akaita Donald na kumstua Dr Joshua
toka mawazoni
“ Donald mambo uliyonieleza ni makubwa na mazito
sana lakini ninaiona faida kubwa mbele yake.Japokuwa
uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa lakini idadi
kubwa ya raia wake bado masikini na kwa ahadi hizi ambazo
serikali ya Marekani imeziahidi ninayaona mabadiliko
makubwa kwa Tanzania.Kwa upande wangu mimi sina tatizo
katika hili ilimradi tu ahadi zote zuilizoahidiwa
zitekelezwe.Najua baada ya matukio hayo kutokea mtikisiko
kidogo wa uchumi lakini nina imani ndaniya kipindi kifupi
hali tarejea kuwa ya kawaida.” Akasema Dr Joshua .Donald
kwa furaha aliyoipata akainuka na kumpa mkono Dr Joshua
“ Hongera sana Dr Joshua.Wewe ndiye rais unayeona
mbali.Una mtazamo mpana sana kwa nchi
yako.Ninakuhakikishia kuwa maamuzi yako ya leo yatakuwa
na faida kubwa sana kwa nchi yako siku za
usoni.Nakuhakikishia wananchi wa Tanzania watakukumbuka
daima kwa kuwaachia rais kama Dr Lucia ambaye wakati wa
uongozi wake serikali ya Marekani itamwaga misaada mingi
sana kwa serikali yake itakayowanufaisha mamilioni ya
watanzania.Nataka nikuondoe wasi wasi pia kwamba mambo
yote yatakayotokea si Tanzania wala Marekani
watakaolaumiwa bali ni mtandao wa Alqaeda.Wakati dunia
ikiwalaani magaidi ,mamilioni ya watanzania watakuwa
wanapata huduma za maji safi ya kunywa,huduma bora za
afya,elimu nishati ajira pamoja na mambo mengine mengi
toka kwa serikali ya Marekani.Kwa kauli yako hiyo
mheshimiwa rais unaniruhusu niwataarifu wakubwa zangu
kwamba umekubali ili tuweze kuendelea na hatua
inayofuata?
“ Bila shaka Donald,unaweza kuendelea na hatua
inayofuata.Nini kinachofuata baada ya hapa?
“ Hatua inayofuata ni kumleta nchini rais mtarajiwa
Dr Lucia Mkozumi na tutakuwa na maongezi ya pamoja
mimi,wewe,Dr Lucia pamoja na mratibu wa mashambulio
mawili toka Alqaeda .Dr Lucia yuko nchini Afrika ya kusini
akiwa ameambatana na binti mfalme Salhat nitawasiliana
naye usiku huu na kesho atakuwa hapa nchini na kesho hiyo
hiyo jioni tutakutana hapa kwa ajili ya kukaa kikao kizito cha
kupanga mikakati ya utekelezaji wa matukio yote.” Akasema
Donald.
“ Sawa Donald.Tutaonana hiyo kesho.Tutakutana
hapa hapa kwani ndiyo sehemu salama zaidi kwa sisi kuongea
na kupanga mipango yetu” akasema Dr Joshua na kuagana na
Donald akamsindikiza hadi lilipo gari lake akaondoka zake na
Dr Joshua akarejea sebuleni akaketi sofani
“ Mambo aliyotumwa Donald aje anieleze ni mambo
mazito mno lakini endapo yatafanikiwa kutekelezwa basi nchi
yetu itapata manufaa makubwa kuliko athari zitakazojitokeza
katika utekelezaji wake .Nchi itayumba kidogo lakini ndani ya
kipindi kifupi itakaa sawa na wananchi watasahau kabisa
matukio yote.Suala hili ukilitazama kwa upana wake ni kweli
Marekani wanastahili kulinda maslahi yake kutokana na
kufanya uwekezaji mkubwa sana hapa nchini kuliko nchi
nyingine yoyote afrika.Uwekezaji huu unawapa nguvu ya
kuweza kuingia hadi katika siasa zetu na kuchagua rais
wanayemtaka ambaye wanaamini atakuwa na manufaa
kwao.Hili si tatizo as long as wananchi wetu wananufaika
kwa misaada mikubwa itakayotolewa na Marekani.Kipindi
changu cha uongozi,serikali ya Marekani wamekuwa ni
wafadhili namba moja wa bajeti yetu ya serikali na miradi
mingi ya maendeleo na endapo nikifanikisha Dr Lucia awe
rais kama wanavyotaka misaada itaongezeka maradufu”
akawaza Dr Joshua na kukumbuka kitu akatabasamu
“ Dr Lucia Mkozumi,huyu mwanamamama japokuwa
sijabahatika kuonana naye lakini anaonekana anafaa sana
kuwa rais.Anaonekana ni mtu jasiri na asiyesita kufanya
maamuzi makubwa “ akawaza Dr Joshua akajimiminia whisky
katika glasi na kunywa funda kadhaa
“ Kwa upande wangu nimeahidiwa mambo mengi
makubwa .Kikubwa zaidi ni fedha nyingi.It’s a lot of
money.Maisha yangu baada ya kustaafu yatakuwa mazuri
mno.I’ll be like an angel in heaven.Laiti kama jambo hili
lingekuja mapema kabla sijaanza mchakato wa kukiuza kirusi
Aby katu nisingeuza kitu kile kilichojaa mikosi na hadi sasa
mke wangu na mwanangu Flaviana wangekuwa bado hai..”
Mara wazo likamjia Dr Joshua
“ Kwa kuwa kuna huu mpango mpya umekuja ambao
unaonekana ni bora zaidi na una maslahi mapana kwangu na
kw anchi kwa nini nisiachane na mpango ule wa kukiuza
kirusi Aby?.Kirusi kile naona kama vile kina mkosi kwani
mpaka sasa tayari nimemkwisha wapoteza watu wangu
wawili wa karibu sana halafu kitu kingine ni kwamba
sifahamu Hussein anataka kukitumiaje kirusi hicho.”
Dr Joshua akanywa tena funda la mvinyo
“ Hapana siwezi kumpa Hussein kile
kirusi.NItamrejeshea fedha zake zote .Najua itakuwa ngumu
lakini hakuna namna nyingine lazima niachane na mpango
ule na nielekeze nguvu katika mpango huu wa Marekani
ambao una maslahi manono kwangu..”
Akatulia tena akanywa funda lingine la mvinyo
“ Dah ! Imekuwa ni siku ndefu sana iliyokusanya
mambo mengi na kichwa changu kimechoka.Nahitaji
kupumzika lakini kabla ya yote lazima nikaonane na Yule