Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

0764294499 ila ukienda huko ya huku yaache huku huku.usije ukasema huku tunakula draft tena kwa kujipakulia na kula kwa tani yako.utaharibu
Kwa hiyo nikitaka kukufata wasap nitumie no. Hiyo au vip?
 
Kwa hiyo nikitaka kukufata wasap nitumie no. Hiyo au vip?
hiyo unamfuata mtunzi .yangu mm ni 0625503998. nenda kwa mtunzi ukamchangie mkuu maana hapa tumemfanyia hujuma
 
0764294499 ila ukienda huko ya huku yaache huku huku.usije ukasema huku tunakula draft tena kwa kujipakulia na kula kwa tani yako.utaharibu
Watu wana viherehere na tamaa ka Dr Joshua na nduguze. Kilichowakimbiza kule halafu wakaanza kumwaga mboga maana yake nn?? Nyie mnahitaji watu kama Abel. Abel halazi damu..
 
SEHEM YA 40

habari kama ilivyozoeleza,ulipigwa wimbo wa taifa n
a wazi
mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akajitokeza
“ Ndugu zangu watanzania habari za usiku
huu.Nimejitokeza mbele yenu usiku huu kuzungumza na
nyi
kuhusiana na masuala mazito yaliyoikumba nchi yetu
leo.
Ndugu zangu watanzania siku ya leo ni siku ambayo
haitasahaulika katika historia ya nchi yetu.Kumetok
ea
matukio mawili ya mashambulio ya mabomu ambayo
tunaamni yamefanywa na magaidi ambayo yamesababisha
damu ya watanzania wasio na hatia kumwagika.
Tuko la kwanza limetokea saa sita za mchana
ambapo hoteli ya Samawati beach hotel imelipuliwa k
wa
mabomu na idadi kubwa ya watu wamepoteza maisha na
wengine wamejeruhiwa wengi wao vibaya sana ikiwamo
kupoteza kabisa viungo vyao.Miongoni mwa walipoteza
maisha ni raia wa kigeni toka mataifa mbalimbali am
bao
walikuwa wamefikia hotelini hapo.
Baadae mida ya saa tisa za alasiri watu ambao
tunaamini ni magaidi walivamia jengo la kibiashara
la Dar city
shopping mall na kufanya shambulio kubwa ambalo
limesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.B
ado
hatuna idadi kamili ni watu wangapi walipoteza mais
ha lakini
pindi idadi kamili itakapopatikana tutawafahamisha.
Makomandoo wa jeshi letu walifanikiwa kuingia
ndani ya jengo hilo wakapambana na magaidi hao wali
okuwa
na silaha nzito na kuwamaliza wote.Kwa taarifa nili
zo nazo
mpaka sasa hakuna gaidi hata mmoja aliyebaki hai.Wo
te
wameuawa na uchunguzi unaendelea ili kubaini kama k
una
gaidi yeyote aliyebaki
Wakati magaidi hao wakitekeleza shambulio lao
ndani ya jengo hilo alikuwemo rais wa Tanzania Dr J
oshua
,alikuwemo pia rais mstaafu wa Tanzania Deus Mkozum
i
akiwa na familia yake vile vile alikuwemo binti mfa
lme wa
Saudi Arabia aliyekuja hapa nchini kwa mapumziko ak
iwa
ameongozana na wenyeji wake ambao ni familia ya Deu
s
Mkozumi.
Wanajeshi wetu walifanikiwa kumuokoa rais lakini
kutokana na mapambano makali yaliyotokea kabla ya
wanajeshi wetu hawajafika baina ya walinzi wa rais
na
magaidi ,rais alikuwa amejeruhiwa na ninachukua naf
asi hii
kulitangazia taifa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano
wa
Tanzania Dr Joshua Joakim amefariki dunia wakati
akikimbizwa katika hospitali kuu ya jeshi.Kwa mujib
u wa
taarifa ambazo zimethibitishwa ni kwamba rais msta
afu
Deus Mkozumi na familia yake nao pia ni miongoni mw
a
watu waliopoteza maisha . .
Ndugu watanzania ,taifa letu limepatwa na msiba
mkubwa sana wa kuondokewa na watu hawa muhimu.Lakin
i
pamoja na masahibu hayo makubwa ambayo taifa letu
limeyapata bado kuna jambo lingine limegunduliwa .K
una
kirusi ambacho inasemekana ni hatari sana na kinach
oweza
kusababisha kifo ndani ya kipindi kifupi, na kinach
osambaa
kwa njia ya hewa tayari kimesambaa hewani.Tayari ba
adhi ya
watu waliokuwemo ndani ya jengo la Dar city shoping
mall
wanatajwa kufariki baada ya kuvuta hewa yenye kirus
i
hicho.Tayari timu ya wanasayansi wetu wameanza uchu
nguzi
ili kubaini ni aina gani ya kirusi na namna ya kuwe
za
kukidhibiti.Tayari tumekwisha omba pia msaada wa
wataalamu toka umoja wa mataifa ambao watafika hapa
muda wowote kuanzia sasa ili kusaidia na wale wa kw
etu
katika kukidhibiti kirusi hicho hatari ambacho kina
sambaa
kwa njia ya hewa na huathiri mfumo mzima wa upumiaj
i
.Wakati wanasayansi wetu wakiendelea na uchuguzi
,wanamchi mnatakiwa kuchukua tahadhari za kujiking
a na
kirusi hiki kwa kuziba pua zenu kwa vifaa malum vya
kukinga
pua na mdomo au vitambaa maalum ambavyo mpango
unaandaliwa ili vitolewe bure katika kila hospitali
hapa
nchini. Naziagiza hospitali za mikoa kote nchini ku
tenga wodi
maalum kwa ajili ya wagonjwa watakaokuwa wameathiri
ka
na kirusi hiki
Ndugu zangu watanzania ,pamoja na msiba mzito
tulioupata wa kuondokewa na wapendwa wetu,nawamba
ndugu zangu tuwe watulivu katika wakati huu wa majo
nzi na
kuwaombea wale wote waliopoteza maisha yao katika
mashambulio ya leo wakiwamo viongozi wetu wakuu wa
kitaifa.Pamoja na mashambulio haya napenda
kuwahakikishia kuwa nchi yetu bado iko salama na ms
iwe na
hofu yoyote.Majeshi yetu ya ulinzi na usalama yako
macho
usiku na mchana kwa kulinda mipaka yetu na kuzuia k
ama
kuna mashambulio mengine yamepangwa kutokea hapa
nchini.Tumeshambuliwa na damu ya watanzania wasio n
a
hatia.Tutapambana na yeyote aliyemwaga damu za
watanzania awe mkubwa ama mdogo.Tutachukua hatua
dhidi ya mtu,kikundi au taifa lolote lililoshiriki
katika
kupanga,kufadhili,au kusaidia kwa namna yoyote ile
katika
shambulio la leo.
Natangaza siku kumi na nne za maombolezo ya
kitaifa na katika siku hizo zote bendera zitapepea
nusu
mlingoti.Mtakuwa mkipokea taarifa kupitia vyombo vy
a
habari kuhusu kile kinachoendelea .
Mwisho kabisa narudia kuwaomba ndugu watanzania
tuendelee kuwa watulivu,tudumishe amani na mshikama
no
katika kipindi hiki kigumu bila kusahau kujikinga d
hidi ya
kirusi Aby
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza”
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
alihitimisha hotuba yake kwa taifa.Kilichofuata baa
da ya
hotuba hiyo ilikuwa ni nyimbo za maombolezo.Baada y
a
kutoa hotuba ile kwa taifa waziri mkuu akaingia kat
ika katika
kizito cha baraza la usalama la taifa ili kujadili
matukio
yaliyotokea na hali ya usalama wa nchi.Kwa kuwa Mat
hew
alikuwa na taarifa nzito na nyeti kwa usalama wa nc
hi,waziri
mkuu alimualika ashiriki katika baraza lile ili vio
ngozi wengine
waweze kufahamu kwa undani nini hasa kilichotokea n
a
kinachoendelea hapa nchini
****************
Kikao cha baraza la usalama wa taifa kilimalizika
saa
nane za usiku.Uwepo wa Mathew katika kikao hiki uli
kuwa na
umuhimu mkubwa sana kwani ni pekee aliyekuwa
anafahamu mambo mazito yaliyokuwa yanafanywa kwa si
ri
na mtandao wa Dr Joshua.Baada ya kumalizika kwa kik
ao kile
ilikuwa taarifa kuwa katibu wa rais Dr Kigomba amep
atikana
akiwa ndani ya mojawapo ya magari yaliyokuwapo kati
ka
maegesho ya jengo la Dar shoping mall wakati vikosi
vya jeshi
vilikuwa vinafanya upekuzi katika magari yaliyoeges
hwa
katika maegesho ya jengo lile.Taarifa ile ilisema k
wamba
baada ya kupelekwa hospitali Dr Kigomba amepimwa na
amegundulika hana maambukizi ya kirusi Aby kwani nd
ani ya
gari alikuwa amefungwa kitambaa puani na mdomoni
ambacho ndicho kilichomsaidia asiweze kuathiriwa.Ta
arifa
nyingine ilisema kuwa Abel Mkokasule naye vile vil
e
amekamatwa kufuatia agizo la waziri mkuu.
Mathew aliondoka maeneo ya ikulu akiwa na ulinzi
aliopewa akaelekea moja kwa moja hospitali kufatil
ia hali ya
Peniela .Jiji la Dar kwa usiku huu lilikuwa kimya k
abisa .Ni
magari ya polisi tu yaliyoonekana kuranda randa kat
ika mitaa
mbali mbali yakifanya doria.
Haikumchukua Mathew muda mrefu kufika hospitali
kutokana na kutokuwapo magari barabarani.Alipokewa
na
Edmund na Chin sun ambao hadi muda huo hawakuwa
wamelala.
“ pole sana Mathew “ akasema Edmund na
kumueleza Mathew kilichoendelea wakati hayupo.Edmun
d
alimfahamisha Mathew kuwa upasuaji ulimalizika na
madaktari walisema kwamba ulikuwa na
mafanikio.Madaktari walifanikiwa kuyaokoa maisha ya
Peniela na kwa muda huo aliwekwa katika chumba maal
um
huku madakari wakiendelea kufuatilia hali yake kwa
karibu
“ Ahsante Mungu” akasema Mathew na kushusha
pumzi
Ulikuwa ni usiku mrefu sana kwao wote
watatu.Waliongea mambo mengi yanayohusiana na maish
a
yao mapya wanayotarajia kuyaanza lakini kikubwa zai
di
walifanya maombi maalum kumuombea Peniela
WIKI TATU BAADAE
Habari kubwa iliyotawala vyombo vyote vya habari
dniani kote siku hii ya alhamisi ni ile ya shirika
la afya duniani
kuithibitisha na kuizindua rasmi kinga ya kupambana
na kirusi
Aby.Toka kirusi Aby kiliposambaa na kusababisha maa
fa
makubwa ,makampuni makubwa ya kutengeneza dawa
walichukua sampuli ya damu ya Peniela ambaye ndiye
pekee
aliyekuwa na kinga dhidi ya kirusi Aby na wakafanik
iwa
kutengeneza kinga ambayo baada ya kufanyiwa majarib
io
ilifanya kazi vizuri. Kwa sababu dawa hiyo ilitokan
a na kinga
iliyochukuliwa toka mwilini mwa Peniela wanasayansi
waliamua kumpa heshima ya kipekee na kuiita kinga h
iyo
yenye uwezo mkubwa wa kupambana na kirusi Aby ,Peni
ela.
Kirusi Aby tayari kilikwisha sambaa katika sehemu
kubwa ya dunia na maelfu ya watu tayari walikwisha
poteza
maisha .Kupatikana kwa dawa ya Peniela ilikuwa ni h
abari
njema kwa dunia nzima.Uzinduzi wa dawa ya Peniela
ulifanyika nchini Tanzania na kuhudhuriwa na viongo
zi wa
mataifa zaidi ya sabini
Peniela ambaye kwa sasa hali yake ilikuwa
inaendelea vizuri kutokana na upasuaji mkubwa aliof
anyiwa
alichukuliwa kutoka hospitali na kupelekwa katika u
kumbi
zilimofanyika sherehe za uzinduzi wa dawa hiyo akiw
a
ameongozana na Mathew.Watu wote wakasimama na
kuwapigia makofi.Walitembea katika zuria jekundu hu
ku
wakipunga mikono kuwasabahi viongozi wale wengi
waliohudhuria uzinduzi ule mkubwa wa dawa iliyosubi
riwa
kwa hamu kubwa na mamilioni ya watu duniani. Viongo
zi
mbali mbali walitoa hotuba zao na kisha tukio kubwa
lililokuwa linasubiriwa likafuata.Dawa ya Peniela i
kazinduliwa
rasmi.Lilikuwa ni tukio kubwa kuwahi kutokea nchini
Tanzania ambalo lilirushwa dunia nzima.Peniela alig
euka
kuwa mtu maarufu mno duniani kwani jina lake lilita
jwa
katika kila kona ya dunia.Mikataba aliyoingia na ma
kampuni
makubwa ya kutengeneza dawa duniani ilimuingizia pe
sa
nyingi mno na kumfanya aingie katika orodha ya watu
matajiri duniani.
Baada ya kukamilika kwa uzinduzi ule Peniela
hakurejea tena hospitali bali walielekea katika mak
azi ya
akina Edmund ambako Mathew alikuwa akiishi kwa sasa
.
Baada ya mapumziko mafupi wote wakakusanyika sebule
ni.
“ Peniela “ akaanzisha maongezi Mathew
 
SEHEM YA 41

Dakika chache toka wawasili makaburini gari
lililobeba mwili wa John Mwaulaya likawasili ,jenez
a
likashushwa na kwenda kuwekwa juu ya kaburi lililok
wisha
andaliwa .Watu wote wakasogea pembeni na kumuachia
Peniela nafasi ya kumuaga John Mwaulaya.Alimwaga
machozi mengi sana na baada ya hapo akina Mathew n
ao
wakatoa heshima zao za mwisho na kisha John Mwaulay
a
akazikwa.Baada ya mazishi yale wakarejea nyumbani k
wa
akina Edmund ambako kuliandaliwa chakula maalum kwa
ajili
ya kuagana kilichoambatana na maongezi.Peniela alit
umiwa
wasaa ule kumuomba sana msamaha Edmund na Chin sun
kwa kitendo chake cha kumuua Patrick.Edmund na Chin
sun
hawakutaka sana kuongelea masuala yale kwani tayari
walikwisha ufunga ukurasa ule.Ilipotimu saa moja za
jioni
Mathew na Peniela wakawasindikiza akina Edmund hadi
uwanja wa ndege.Baada ya akina Edmund kuondoka Math
ew
na Peniela wakaelekea ikulu ambako makamu wa rais
aliyerejea kutoka nje ya nchi alikokuwa anapatiwa m
atibabu
ya saratani kwa zaidi ya miezi miwili alikuwa amean
daa
chakula maalum kuwapongeza wale wote waliofankisha
mapambano dhidi ya magaidi na kuwashinda.Kupitia us
iku
huo makamu wa rais pia alitarajia kuzungumza na
watanzania
Kabla ya waalikwa kupata chakula,kulikuwa na
burudani kadhaa toka kwa vikundi mbali mbali vya bu
rudani
na baadae ikafuata zamu ya makamu wa rais kutoa hot
uba
yake ambayo ilirushwa moja kwa moja na televisheni
ya taifa
pamoja na vituo vingine.
Kwanza alianza kwa kuwatambua viongozi wote wa
juu wa kitaifa waliohudhuria na kisha akawashukuru
waalikwa wote kwa kufika kwao halafu akaendelea
“ Ndugu wageni waalikwa na watanzania
wenzangu leo ni wiki ya tatu ,tangu taifa letu tuli
pendalo
lishambuliwe na magaidi na damu ya ndugu zatu wasio
na
hatia ikapotea.Katika historia ya taifa letu katu h
atuwezi
kulisahau tukio lile la kinyama.Magaidi wasio na hu
ruma
walivamia jengo la biashara la Dar city shopping ma
ll na
kuua watu wasio na hatia .Katka shmbulio hilo
tuliwapoteza pia kiongozi wetu wa taifa rais wetu D
r
Joshua Joakim ,pia rais mstaafu Deus Mkozumi pamoja
na
watu wengine mia sita na hamsini na nane. Huu ni ms
iba
mkubwa mno ambao ni vigumu hata kuuelezea.
Shambulio lingine lilitokea katika hoteli ya
Samawati beach hotel ambako watu wengi walipoteza
maisha na wengi wao wakiwa ni raia wa kigeni walio
kuja
hapa nchini kwa shughuli za utalii na mapumziko.Wot
e
waliopoteza maisha yao tunawaombea wapumzike kwa
amani na kwa wale wote waliopata majeraha ama
kupoteza viungo vyao katika mashambulio yote mawili
serikali na watanzania tunawatakia uponaji wa harak
a na
wote tuko nyuma yenu.
Ndugu zangu watanzania ,watu waliotekeleza
mashambulio yale walikuwa na malengo yao lakini kwa
bahati mbaya kwao malengo hayo hayakuweza
kufanikiwa.Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo ni kwam
ba
katika shambulio la Dar shopping mall magaidi walik
uwa
na lengo la kumteka binti mfalme wa Saudi Arabia
aliyekuwa amekuja nchini kwa mapumziko.Lengo kubwa
la
kutaka kufanya hivyo lilikuwa ni kutaka kuishinikiz
a serikali
ya Saudi Arabia imuachie huru kiongozi wao anayeshi
kiliwa
nchini humo. Lengo lao halikuweza kufanikiwa kwani
vijana
wetu shupavu wazalendo na walio tayari kuimwaga dam
u
yao kwa ajili ya kulinda taifa lao walifanikiwa kul
izima
lengo hilo la magaidi ndani ya muda mfupi.Ushupavu
waliouonyesha katika kukabiliana na magaidi wale wa
sio
na hata chembe ya huruma umeudhirishia uimwengu kuw
a
Tanzania si nchi ya kufanyia uharamia wao na hii ni
salamu
kwa wale wote ambao wanapanga au wanafikiria
kutekeleza mipango yao hapa nchini kwamba wasithubu
tu
kufanya hivyo kwani sisi tuko makini na hatujalala
usingizi.Yeyote atakayethubutu kucheza na amani ye
tu
atakiona ”
Makofi mengi yakapigwa kisha makamu wa rais
akaendelea

Japokuwa
kidonda
tulichoumizwa
bado
hakijapona lakini maisha yamerejea ya kawaida na wa
tu
wanaendelea na shughuli zao za kila siku bila wasi
wasi,Tanzania imebaki moja na itaendelea kuwa moja
kwani siku zote yanapotokea majanga makubwa ya
kitaifa,watanzania huziweka pembeni tofauti zao na
kushikamana pamoja kama taifa moja yaani jamhuri ya
muungano wa Tanzania”
Makofi mengine mengi yakapigwa.
“ Ndugu zangu watanzania” makamu wa rais
akaendelea
“ Ninapenda kutumia nafasi hii kuwahakikishia tena
kuwa magaidi wote waliohusika katika shambulio lile
la Dar
city
shopping
mall
waliuawa
na
hakuna
aliyesalimika.Pamoja nao kuna watu wachache wa ndan
i
ya nchi walioshirikiana nao ili kufanikisha shambul
io lile
ambao tayari tumekwisha wakamata na kazi bado
inaendelea kuwatafuta wote walioshirikiana na magai
di
kwa namna yoyote ile katika kufanikisha shambulio i
le na
ninawaahidi hakuna atakayesalimika.Tutakwenda mbali
zaidi hadi tuhakikishe tunaufyeka kabisa mtandao wo
te wa
kigaidi ulioanza kujipenyeza hapa nchini kwetu.Naru
dia
tena kuwahakikishia ndugu zangu watanzania kuwa
hakuna yeyote ambaye ana mahusiano yoyote na mtanda
o
wowote
wa
kigaidi
aliyeko
hapa
nchini
atakayesalimika.Tutawasaka
kokote
waliko
na
tutawapata”
Makofi yakapigwa
“ Ndugu zangu watanzania ,katika matukio yale
mawili waliopoteza maisha si watanzania pekee bali
wapo
pia raia wa nchi za nje.Tumepewa pole na mataifa me
ngi
rafiki lakini napenda kutumia nafasi hii kipekee ka
bisa
kuwasilisha kwenu salamu maalum za pole toka kwa
mfalme wa Saudi Arabia .Katika matukio yale mawili
wapo
raia wa Saudi Arabia waliopoteza maisha .Pamoja na
pole
nyingi alizotoa ,pia ametuma salamu nyingi za ponge
zi kwa
vijana wetu waliofanikiwa kuwadhibiti magaidi wale
na
kufanikiwa kumuokoa binti yake salhat ambaye ndiye
aliyekuwa lengo kuu la magaidi.katika salamu zake
ametuma salamu maalum kwa kijana wetu mmoja jasiri
sana anaitwa Mathew .Naomba kokote uliko Mathew
usimame”
Mathew akasimama na kupunga mikono ,makofi
mengi yakapigwa.
“ Ndugu wageni waalikwa na watanzania huyu
mnayemuona ninalazimika kumpa shukrani za kipekee
kabisa kwani huyu alikuwemo ndani ya jengo la Dar ci
ty
shopping mall na ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza
kupambana na magaidi akawaua kadhaa na kufanikiwa
kuwakomboa baadhi ya watu akiwamo binti mfalme
Salhat.Akiwa peke yake alifankiwa kulidhibiti eneo
la juu la
jengo lile na kuwezesha helkopta za jeshi kutua na
makomandoo wetu wakaingia ndani ya jengo kuwafyeka
magaidi.Hongera sana Mathew ,wewe pamoja na wenzako
wote mliopigania nchi yetu kwa moyo mmoja.Majina ye
nu
hayatasahaulika kamwe”
Makofi mengi yakapigwa
“ Ndugu zangu watanzania,uchunguzi tulioufanya
unaonyesha kuwa waliotekeleza mashambulio yale si
kikundi cha Alqaeda pekee bali walishirikiana na w
atu wa
ndani na nje ya nchi.Alipotoa hotuba yake wakati
akilitangazia taifa kifo cha rais,waziri mkuu alito
a ahadi
kuwa hatutaogopa mtu au taifa lolote liilofadhili a
u
kusaidia kwa namna yoyote kufanikisha shambulio
lile.Tumegundua kuna nchi ambayo tulidhani ni maraf
iki na
ndugu zetu kumbe wao ndio wenye kutuzunguka na
kuratibu mipango hii miovu kwa taifa letu.Kama amba
vyo
tumekwisha chukua hatua kwa watu wa ndani ambao
wameshirikiana na magaidi katika kufanikisha shambu
lio
lile,tunachukua hatua vile vile kwa watu wengine au
mataifa ya nje ambao nao walishirikiana na magaidi
wale
na kwa usiku huu ninapenda kuwatangazia kwamba
tumeamua kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na taifa
la
Marekani na tunamtaka balozi wake aondoke hapa chin
i
ndani ya masaa arobaini na nane na katika muda huo
huo
tunamtaka balozi wetu aliyeko nchini Marekani areje
e
nyumbani .Najua maamuzi haya yatawastua wengi lakin
i
kama nilivyosema kuwa hatutamuogopa mtu au taifa lo
lote
liwe kubwa au dogo.Tunao ushahidi wa kutosha
unaotuthibitishia kuwa Marekani walihusika katika
kufadhili shambulio lile la Dar city shopping mall.
Ni aibu
kwa taifa kubwa kama Marekani kufanya kitendo kiovu
kama hiki.”
Makofi yakapigwa kwa wingi.
“ Nafahamu kitendo cha kuvunja mahusiano na
Marekani kina athari kubwa katika uchumi wetu lakin
i
hatuwezi kuendelea kuwa na rafiki kama huyu .Tutata
futa
marafiki wengine ,tutajifunga mkanda na tutasonga m
bele
bila ya kutegemea ufadhili toka kwa mataifa ambayo
hawana malengo mazuri na sisi.Nataka nitumie nafasi
hii
kufikisha ujumbe kwa mataifa yote duniani kuwa Tanz
ania
ni nchi huru na kamwe hatutakubali kuingiliwa na ta
ifa
lolote katika mambo yetu ya ndani ya nchi ,na taifa
lolote
litakalothubutu kufanya hivyo tutaliondoa katika or
odha ya
marafiki zetu bila kusita”
Makofi mengi yakapigwa
“ Ndugu zangu watanzania ili tuweze kujinusuru na
majanga kama haya ya kukandamizwa na mataifa
makubwa kwa sababu ya umasikini wetu,lazima tuamue
kuanza sasa safari ya kujitegemea na kujenga uchumi
wetu
sisi wenyewe bila utegemezi wa mataifa ya nje.Tufan
ye kazi
kwa bidii,tuimarishe viwanda vyetu vya ndani tuzali
she
bidhaa bora na tutumie bidhaa zetu zinazozalishwa n
a
viwanda vyetu wenyewe bila kusahau kulipa kodi.Tuna
zo
rasilimali nyingi ambazo Mungu ametubariki nazo na
endapo tutazitumia vizuri zitatusaidia kuinua uchum
i wetu
na kutuondoa katika utegemezi.”
Makofi mengi yakapigwa
“ Ndugu watanzania kabla sijamaliza hotuba yangu
napenda niwahakikishie kuwa Mungu analipenda sana
taifa letu na anazidi kutubariki kwani leo katika h
istoria ya
nchi yetu na dunia imezinduliwa kinga ambayo itaok
oa
mamilioni ya watu duniani dhidi ya kirusi Aby ambac
ho
hadi sasa kimekwisha ua maelfu ya watu duniani kote
.Ni
mtu mmoja tu katika dunia hii ambaye alikuwa na kin
ga
dhidi ya kirusi hicho na kinga hiyo imetumika kuoko
a
mamilioni ya watu.Tuna bahati kubwa kuwa mtu huyo
anatoka hapa Tanzania.Mabibi na mabwana naomba wote
tusimame tumpongeze Peniela”
Watu wote wakasimama na kupiga makofi mengi
wakimpongeza Peniel;a halafu makamu wa rais akaende
lea.
Ndugu watanzania namalizia hotuba yangu kwa
kuwashukuruni sana kwa maombi yenu .Kwa muda wa
zaidi ya miezi miwili niliyokuwa nje ya nchi kwa ma
tibabu
na sikuweza hata kushirikiana nanyi katika msiba mk
ubwa
uliotupata .Kwa sasa naendelea vizuri na afya yang
u
imeimarika na ninawaahidi kuendelea kuwatumikia
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni sana kwa kuniskiliza.
Hivi ndivyo makamu wa rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alivyohitimisha hotuba yake h
alafu
zikafuata ratiba nyingine
Saa sita za usiku Mathew na Peniela waliondoka iku
lu
.Safari yao ilikuwa ya kimya kimya .Hawakurejea ten
a katika
makazi ya akina Edmund na badala yake wakaelekea mo
ja
kwa moja katika hoteli moja kubwa.Peniela alionekan
a kuwa
mbali sana kimawazo na macho yake yalijaa
machozi.Mathew alilitambua hilo na hakutaka kumseme
sha.
Hawakurejea tena katika makazi ya akina Edmud
badala yake wakaelekea katika hoteli moja kubwa san
a jijini
Dar wakachukua chumba.Hata baada ya kuingia chumban
i
bado Peniela aliendelea kumwaga machozi .,Mathew
akamfuata karibu akamfuta machozi
“ Peniela stop crying ..” akasema lakini ilikuwa n
i
kama vile amekitonesha kidonda kwani Peniela alizid
i
kumwaga machozi
“ Tafadhali usilie Peniela.It’s over now.The war i
s
over .All the monsters are gone...Dr Joshua is gone
,mtandao
wake umefumuliwa na unaendelea kufumuliwa,Dr Kigomb
a
amekamatwa ,Abel Mkokasule pia amekamatwa na wote
wanaisaidia polisi katika uchunguzi ,vile vile Kare
em naye
amekamatwa na wote hawa wanasaidia katika kuutambua
na
kuufyeka kabisa mtandao wa Dr Joshua.Ukiacha hayo ,
Team
SC41 is no longer exist kwa hiyo hakuna tena kitu c
ha
kuhofia.”
Huku akibubujikwa na machozi Peniela akasema
“ Mathew huwezi kujua ni uchungu kiasi gani
nilionao moyoni mwangu .I wish I were dead...!!
“ Hapana Peniela tafadhali usiwaze hivyo.Huna
sababu ya kufika huko”
“Mathew nasikia uchungu mwingi kwa mambo
yaliyotokea ambayo yamesababishwa na mimi.Ni wiki y
a tatu
sasa najaribu kutafuta ni neno gani nitalitumia kuk
uomba
msamaha kwa mambo niliyoyafaya lakini nimekosa.”
“ Shhh..!!Mathew akamuwekea Peniela kidole
mdomoni.
“Peniela that’s the past.Dont talk anything about
the
past.Forget what happened and focus on your future.
.”
“ No Mathew .No ! I did a lot of awafull things.I
did
something that I cant even forgive myself.For what
I did I
cant even look in your eyes and say I’m sorry” akase
ma
Peniela huku akilia
“ Peniela we all do mistakes.We all did mistakes.N
i
kawaida ya mwanadamu kukosea.Naomba usahau yote
yaliyotokea na tuangalie ya mbeleni”
 
SEHEM YA 42

nikikukamata.” Akasema Mathew na kunyamaza akafumba
macho
“ Now you have me,you can do all that you promised
yourself to do when you find me” akasema Peniela h
uku uso
wake ukiwa umeloa machozi mengi yaliyokuwa
yakimtoka.Mathew naye ambaye naye macho yake yalija
a
machozi akasema
“ They say everything happens for a
reason.Ninaamini hata haya yote yaliyotokea ni kwa
sababu
maalum kwa hiyo siwezi kukufanya chochote Peniela n
a
kama
ningetaka
kufanya
nilivyopanga
kukufanyia
nisingepambana kuyaokoa maisha yako ningekuacha ufe
ndani ya jengo lile.Kama nilivyokueleza kuwa kila k
itu
hutokea kwa sababu maalum ni sababu hiyo ndiyo ina
yonipa
ujasiri wa kusema kwamba nimekusamehe yale yote
uliyonikosea” akasema Mathew na kuzidisha kilio kwa
Peniela
“ No Mathew you don’t have to do that.Sistahili
msamaha wako .Mambo niliyokufanyia ni makubwa na
hayastahili msamaha” akasema Peniela
“ Peniela hata nikisema leo hii nikuchome kisu kam
a
ulivyomchoma Anitha bado haitanisaidia kitu,Anitha
will
never come back.Nimeyaacha mambo yote yapite na
nimekusamehe.Peniela You’ve been through a lot and
its
time now to start your new life ,that life you’ve
been
dreaming for a very long time.Yale yote uliyoyahita
ji katika
maisha yako yamekwisha timia na yana kwenda
kutimia.Ndoto yako kubwa ilikuwa ni kuachana na tea
m SC41
na kuishi maisha ya kawaida kama wengine.Hilo limet
imia
kwani Team Sc41 haipo tena na uko huru kuishi maish
a
unayoyahitaji.Ndoto yako nyingine ilikuwa ni kuwa t
ajiri
mkubwa na ninahisi hilo ndilo lililokufanya ukakich
ukua kile
kirusi lakini hata hilo nalo limetimia .Wewe kwa sa
sa ni mtu
maarufu na tajiri mkubwa.Damu yako imetumika
kutengeneza kinga ambayo imeokoa maisha ya mamilion
i ya
watu duniani.Leo hii kila kona duniani jina ako
linatajwa.Umeingia katika orodha ya watu maarufu
waliowahi kutokea katika dunia hii so Peniela go li
ve the life
that you’ve been dreaming “ akasema Mathew .Ilmchuk
ua
Peniela dakika mbili kuinua kichwa na kusema
“ Mathew I have no life.Ni kweli nimejulikana duni
a
nzima na nimebahatika kuwa na pesa nyingi na ni kwe
li hiyo
ilikuwa ni ndoto yangu kujulikana duniani kote na k
uwa na
pesa nyingi na vyote hivyo nimevipata lakini havina
maana
yoyote tena kwangu kwa sababu sintakuwa na furaha.
Nimepoteza watu wangu wote wa muhimu ambao
ningefurahi nao I’ve lost you..Hakuna kitu kinachon
iumiza na
kuniua taratibu kama kukupoteza wewe.Sikuwahi kukut
ana
na mtu ambaye nilifurahi kukutana naye kama
wewe.Sikuwahi kukutana na mtu aliyeguswa na maisha
yangu kama wewe.Toka moyoni mwako uliguswa na
kuumizwa sana na maisha yangu niliyokuwa naishi nda
ni ya
team SC41 na ulijitolea kwa kila uwezavyo kuhakikis
ha
ninaachana na maisha yale.Kukupoteza mtu kama wewe
ni
kupoteza kitu cha thamani kuliko hata utajiri nilio
upata na
ndiyo maana sioni tena sababu ya mimi kuendelea kui
shi .
Nitaishi vipi bila furaha wala amani moyoni mwangu?
Akauliza Peniela
“ Peniela hujawahi kunipoteza.I was there and I’ll
always be there by your side.Peniela there is one i
mportant
thing I want to tell you”
“What is that ? akauliza Peniela .Mathew akamshika
mikono akamtazama usoni
“ Peniela I love you .Nakupenda toka ndani ya moyo
wangu.Upendo nilio nao kwako siwezi kuueleza .What
I feel
for you is more than love.Nguvu ya upendo wangu kwa
o
ndiyo iliyonifanya niyaweke pembeni yale yote yaliy
otokea
na kufikiria kutaka kuufungua ukurasa mpya wa maish
a
pamoja nawe.Peniela unahitaji maisha mapya,mimi pia
nimekwisha kata shauri la kuachana na kazi zangu zo
te
ninazozifanya na nianze maisha mapya.Nataka unikub
alie
niwe mpenzi wako.Nakuahid.......”
Mathew hakumaliza alichotaka kukisema Peniela
akamrukia akamkumbatia na kumporomoshea mabusu
mazito.Alikuwa ni kama mtu aliyepatwa na uchizi wa
ghafla.Hakuwa ametarajia kusikia maneno yale toka k
wa
Mathew
“ Oh God hank you for this miracle........” akasema
Peniela huku akimtazama Mathew kama mtu anayetazama
kitu cha kustusha .Akambusu tena na kusema
“ Mathew you don’t have an idea how many days
and night I’ve been waiting to hear those words you
’ve just
said to me.Naamini kukutana kwetu haikuwa bahati mb
aya
.Mungu alikuwa na makusudi yake .Baada ya miaka min
gi
kupita nkilitafuta penzi la kweli hatimaye nimefani
kiwa
kulipata.Nilianza kukupenda sekunde ya kwanza nilip
okutia
machoni.Sikuwa na uhakika bado na hisia zangu but I
knew
there is something strong between us.Mathew nakupen
da
zaidi ya ninavyoweza kukueleza.Karibu katika moyo w
angu
Mathew.Wewe ni mfalme wangu niongoze ,niamuru
chochote nami nakutii.” Akasema Peniela kwa hisia k
ubwa .
“ Mathew ahsante sana kwa kunipenda ,najua
unayafahamu
vyema
maisha
yangu
ya
nyuma
niliyoishi,unayafahamu madhaifu yangu lakini bado
umechagua kunipenda.Huu ni upendo wa kweli na wa
dhati.Nakuahidi kuachana kabisa na yale maisha yang
u ya
nyuma na moyo wangu ninaukabidhi kwak😵uh Mathew .
.”
akasema Peniela na kumkumbatia Mathew .
***************
Siku mpya imeanza .Ukurasa mpya wa mapenzi
mazito ulifunguliwa kati ya Mathew na Peniela.Ni Ma
thew
aliyekuwa wa kwanza kuamka na kuanza kumtazama Peni
ela
aliyekuwa bado katika usingizi mzito
“ Siamini kama ni kweli nimefanikiwa kuyaanza
maisha mapya na Peniela.Ninampenda sana Peneila na
sijui
ningefanya nini endapo angefariki dunia.From now on
I’m
going to protect her.I’m going to make her the happ
iest
woman on earth.Nobody will never hurt her” akawaza
Mathew na mara Peniela akafumbua macho.
“ Wow .it’s another day.What a beautifull
morning.How are you my king? Akasema Peniela huku
akitabasamu
“ I’m ok my queen.Unajisikiaje?
“ Ninajisikia furaha mno.Nina amani kubwa moyoni.I
feel like I’m in heaven.My night was wonderfull.Kat
ika
maisha yangu sijawahi kuwa na usiku mzuri kama wa
jana.Ahsante sana Mathew kwa kufanya usiku wangu wa
kwanza nawe kuwa wa kihistoria.Maisha yangu yana fu
raha
na amani” akasema Peniela wakapeana mabusu
mazito.Peniela akamtazama Mathew usoni na kugundua
kuna kitu kilikuwa kinamsumbua.
“ Mathew I can read your mind,there is something
bothering you.Niambie una tatizo gani?
“ Hakuna tatizo Peniela”
“ Hapana Mathew ,sura yako inaonyesha kabisa una
tatizo.Niambie mfalme wangu nini kinakusumbua?
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Kuna jambo Fulani John Mwaulaya alinieleza siku
ile
alipotaka nionane naye”
“ Alikueleza nini?
“ Aliniambia kwamba familia yangu iko hai bado
.MKe wangu na watoto wako hai”
Peniela akastuka akainuka na kukaa
“ No ! that cant be possible.Familia yako ulidai
iliteketea katika moyo.Iweje leo wawe hai?
Mathew akatabasamu kidogo na kusema
“ John Mwaulaya was wa monster lakini kuna nyakati
alikuwa na moyo wa huruma.Alidai hakuona sababu ya
kuiteketeza familia isiyokuwa na hatia.Walichokifan
ya ni
kuchukua maiti katika mojawapo ya chuo kikuu cha ut
abibu
ambazo hutumika kwa mazoezi na kuziweka ndani ya
nyumba yangu wakazichoma moto.Familia yangu ilichuk
uliwa
na kupelekwa Marekani ambako wanaishi hadi sasa.Len
go la
kufanya hivyo ni ili kunichanganya akili na waweze
kunipata
kirahisi lakini hawakufanikiwa kunipata.”
“ Oh my God so what’s going to happen to us?
Akauliza Peniela kwa wasiwasi.Mathew akatabasamu na
kusema
“ Usihofu malaika wangu.Nothing is going to happen
to us.Tulichokianzisha anayeweza kukitenganisha ni
Mungu
pekee.Sina mpango wa kuvuruga maisha yao kwani kwa
sasa
mke wangu amekwisha olewa and they live happily.Joh
n
Mwaulaya alinipa anuani ya mahala wanakoishi endapo
nitahitaji siku moja kuwatembelea.”
“ Kwa hiyo nini mipango yako ? akauliza Peniela
“ Kama nilivyokueleza kuwa kwa sasa sina mpango
wa kuyavuruga maisha yao.Kitendo cha mimi kujitokez
a
kwao kitawavuruga sana kwani tayari wanafahamu mimi
nimekwisha fariki.Sitaki kuyavuruga maisha yao ya f
uraha
waliyonayo sasa hivi.Kilichomo katika akili yangu k
wa sasa ni
mimi na wewe kuwa mwili mmoja yaani tufunge ndoa.”
Peniela akamkubatia Mathew akambusu kisha
wakainuka na kwenda kuoga na kujiandaa kwa ajili y
a ratiba
ya sku ambayo ingeanzia hospitali na baadae walipan
ga
kwenda kutembelea kaburi la Anitha ambaye alizikwa
wakati
bado Peniela akiwa amelazwa hospitali.
MIEZI MINNE BAADAE
Ni siku ya pili ya fungate lao wakiwa katika hotel
i
moja kubwa visiwa vya Zanzibar. Baada ya kufunga nd
oa
waliamua kuja kupumzika katika visiwa hivi .Wakiwa
wamejilaza ufukweni wailifurahia jua na upepo mzuri
wa
bahari,muhudumu wa hoteli akafika akiwa na simu mko
noni
akasimama kwa adabu pembeni ya akina Mathew
“ Karibu “ akasema Peniela
“ Samahani kwa usumbufu,kuna mtu ambaye
amekuwa akipiga simu toka asubuhi nah ii ni mara ya
nane
anapiga simu anasema anatokea Marekani ,”
“ Marekani anaitwa nani? Akauliza Mathew na kuvua
miwani ya jua aliyokuwa ameivaa
“ Anasema anaitwa Zita.Anasema nikupe simu kuna
jambo la muhimu anataka kungea nawe kaka” akasema Y
ule
muhudumu
“ Hapana ,mwambie kwamba sina muda wa kuongea
naye sasa hivi na sihitaji simu yoyote kwani niko k
atika
fungate”
“ Darling do you know her? Akauliza Peniela
“ Ndiyo ni Yule aliyekuwa mke wangu” akasema
Mathew kwa sauti ndogo
“ It’s ok my love,take that call” akasema
Peniela.Mathew akamtazama halafu akaichukua simu
muhudumu Yule akaenda kusimama mbali
“ Hallow” akasema Mathew lakini hakujibiwa
“ Hallow” akasema tena lakini hakuna mtu aliyejibu
“ Hallow” akasema kwa mara ya tatu na safari hii
sauti ya mwanamke ikaitika upande wa pili wa simu
“ Hallow” Ilikuwa ni sauti ambayo Mathew
aliitambua mara moja.
“ Zita !! akasema
“ Mathew !! akasema Zita halafu zikapita sekunde
kadhaa za ukimya
“ Congraturations Mathew “ akasema Zita
“ Zita how are you” akasema Mathew
“ I’m fine Mathew ,we’re all fine” akajibu Zita ha
lafu
ukapita tena ukimya
“ Mathew samahani sana kwa kukusumbua najua
huhitaji usumbufu kwa sasa kwa sababu uko katika fu
ngate
kwa hiyo sitaki kuchukua muda wako mwingi naomba ka
ma
dakika tano tu za kuongea nawe” akasema Zita
“ Go ahead” akasema Mathew.Zita akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ Katika maisha yangu sintoisahau ile siku ya uzin
duzi
wa dawa ya Peniela kwani wakati dunia nzima ikiwa
inasherehekea mimi nilikuwa nalia baada ya kumuona
mtu
ambaye kwa miaka hii yote nilifahamu kuwa
amefariki.Mathew sitaki kuongea sana kwani nafasi h
ii ya
kuongea nawe nimekuwa nikiitafuta kwa miezi kadhaa
sasa
 
SEHEM YA 43 NA........................

bila mafanikio hadi leo hii nilipofanikiwa.Mathew n
ataka tu
nikwambie kwamba mimi na wanangu tulichukuliwa na
kuletwa Marekani na tuliambiwa kwamba umefariki dun
ia
kuna watu wamekuua na kwamba hata sisi tulikuwa
tunatafutwa tuuawe.Nililia sana na nilijilaumu sana
kwa nini
ukachagua kuifanya kazi ile ya upelelezi? Baada ya
kufika
Marekani tulianza maisha mapya na baada ya miaka mi
tatu
nikapata bwana nikaolewa nikijua kwamba umekufa.Kwa
sasa mimi na wanangu tuna uraia wa Marekani na toka
nilipoondoka Tanzania sijawahi kurejea kwani John
aliniambia kwamba sitakiwi kuonekana tena Tanzania
kwani
siku nikitia mguu wangu ndio utakuwa mwisho wangu.K
wa
sasa nina watoto wawili kwa huyo mume wangu mpya na
tunaishi kwa furaha.Nimebadili jina naitwa Martha.
Wanao
wote wazima na wanaendelea vyema na maisha yao ila
maisha yao yamebadilika ghafla baada ya kugundua kw
amba
baba yao yu hai.Jambo hili limewastua sana .Tumewat
afutia
mtaalamu wa saikolojia ambaye anaendelea kuwasaidia
wakubaliane na hiki kilichotokea.Watakapokuwa tayar
i
watakuja kuonana nawe but for now they are not read
y
yet.Mathew sitaki kuchukua muda wako mwingi ila nap
enda
kukwambia kitu kimoja kuwa kazi yako uliyochagua ku
ifanya
ndiyo iliyofanya hadi mambo haya yakatokea.Ndiyo
iliyotutenganisha.Mara nyingi nilikuwa nikikusisiti
za uachane
na kazi hiyo lakini hukutaka kunisikia hadi yalipo
tokea haya
yaliyotokea.Ninachotaka kukushauri ni kwamba umepat
a
mke mzuri sana na nina hakika ameirudisha furaha ya
ko
tena.Peniela ni mwanamke mrembo na dunia nzima
inamuheshimu nakuomba ,muheshimu ,mtunze na
usimuumize kama mimi kwa sababu ya kazi hiyo
uifanyayo.Ukitaka maisha yako yawe na furaha achana
kabisa
na hiyo kazi unayoifanya.Huwezi kuwa na maisha ya k
awaida
yenye furaha na amani ukiwa katika kazi hiyo.Nawata
kia
maisha mema yenye furaha na amani na mpatapo nafasi
mjapo hapa Marekani msiache kuja kututembelea.Ahsan
te
sana Mathew na fungate jema.” Akamaliza Zita na kuk
ata
simu.Mathew na Peniela wakaangaliana
“ Ni mipango ya Mungu mimi na wewe kuwa
pamoja.Yote yaliyotokea yametokea ili mimi na wewe
tukutane.Let’s enjoy life my angel” akasema Mathew
na
kumbusu Peniela wakainuka na kuingia majini kuogele
a.
TAMATI


UKITAKA KUJIPATIA RIWAYA/STORY YA KIJASUSI NA YAKUSISIMUA YA WIMBO WA GAIDI. KUTOKA KWA MTUNZI WAKO MAHILI NA BINGWA WA RIWAYA ZA TAHARUKI HUSSEIN ISSA TUWA .KITABU KINAACHIWA WIKI HII

0655428085 WAHI NA UPATE COPY YAKO MAPEMAA .KAMA UJUAVYO VITABU VYA TUWA HUWA VINAGOMBEWA KAMA NJUGU.
 
PENIELA%20%20SEASON%205
 
hivi lege hatuwezi kutengenezea movie hii story! tena inaweza ikawa deries kabisa na tukauza au hii idea ilishafanyiwa kazi
 
hivi lege hatuwezi kutengenezea movie hii story! tena inaweza ikawa deries kabisa na tukauza au hii idea ilishafanyiwa kazi
Ikiwa km move itauza sana tatizo ni technology na vifaa coz itahitaji vitu vingi mno ita ukimpa hii story Jonson sitatham au boern bona utaipenda
 
Asante lege.kwa watu wenye msimamo ni Mathew peke yake ingawa sikutegemea kama yeye n.a. penny wangekuwa wapenzi
 
Thenks LEGE atimae chenye mwanzo pia kina mwisho asante sana
 
Sema huu msimu Wa pili mwamisha akuweka sana zile chachandu za msimu Wa mwanzo ambao ulikuwa unafanya story iwe tamu zaidi
Ata hiii tamu ila chakula kitamu sana ila pili pili inachangia kuongeza ratha[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
 
Back
Top Bottom