Pensheni na kikokotoo: Usichokijua kuhusu uzuri wa kikokotoo, kwa mafanikio na bata la uzeeni

Pensheni na kikokotoo: Usichokijua kuhusu uzuri wa kikokotoo, kwa mafanikio na bata la uzeeni

mrengo wa kushoto

Senior Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
100
Reaction score
185
Lengo zima la mifuko ya jamii ni kumkinga na kumlinda mwanachama wake dhidi ya majanga.

Majanga ni vitu vyoote vinavyoweza kuondoa au kupunguza uwezo wa mtu kuzalisha.

Moja ya janga kubwa ni UZEE.Tunaliita ni janga kwasababu tunaamini huna uwezo wa kuzalisha na kuchangia kiuchumi kama ulivyokuwa kijana.

Fedha ya pensheni ya uzeeni inalengo la kukupinguzia ukali wa maisha katika kile kipindi baada ya kustaafu, kwasababu huwezi kumrithisha mtoto wako kazi yako kama mfanyabiashara itabidi uwe na chanzo cha kipato walao kidogo cha kukusaidia.

Kelele nyingi zipo kwenye swala la Kikokotoo kipi kitumike kitakacholeta tija zaidi kwa mstaafu kati 25/75 ambapo lumpsum (pensheni kubwa) ya 25% kwa pensheni ya kila mwezi ya 75% na hivyo hivyo kwa 33%/67%, 75%/25% ya kiasi cha jumla cha michango pamoja na interest(gawio) la miaka yote ya uchangiaji.

Serekali ipo sahihi kabisa kuweka kikokotoo kilichopo na kwa upande wangu ningependa kingeshushwa zaidi ya hapo tukarudi kwenye 25% ya lumpsum(pensheni kubwa) na 75% (pensheni ya kila mwezi)

KWANINI? Mfano unamichango ya mill 100 katika kipindi chako cha kuajiriwa.

Ukapewa 25mill kama pensheni kubwa na ile 75mill ikigawanywa kwa miaka 10 inakiwa 7.5 kwa mwaka na ukiigawanya 7.5 /miezi 12 unakuwa na laki 625,000 kila mwezi kwa maisha yako yote yaliyobaki hata kama utaishi miaka 60 mingine.

Ukinipa 75 mil na labda sikuwahi kushika hata 10mill kwenye maisha na ajira yangu kwa pamoja,kweli nitafurahia mwaka wangu wa kwanza lakini kumbuka sina nguvu za kuzalisha kama nilivyokuwa kijana,akili maono siyo sawa na vijana siwezi kwenda kuanza kuparangana Kariakoo au karume kwenda china kuafat mzigo na kadhaliaka.

Kitu kikubwa nitaanza kuuliza biashara za kufanya na kuanza kujaribu jaribu. Hapo utapigwa sana na baada ya miaka mi3 hela inaweza kuwa haionekani. Kumbuka nimebakiza 25mill kwenye pensheni ya kila mwezi.
25mill/10miaka= 2.5mill na 2.5mill/12miezi inakuwa 208,000 kwa mwezi.

Anaeishi kwa 625,000 na anaeishi kwa 208,000 kwa mwezi tofauti inaanza kuonekana baada ya miaka 3_4.
Hapo tunajenga wazee tegemezi,ombaomba na waliokosa muelekeo kila siku kulalamikia watoto wao. Hapo ukute bado anasomesha, hajajenga etc.

Unapokuwa huna hela mipango inakuwa mingi lakini ukiipata na hujawahi kuishika wengi malengo yanapotea kabisa na kuitumia vibaya wakijua kesho itakuwepo.
 
Yule boss wako aliejikopesha milioni 200 bila riba yupo? Na yule aliyejikopesha milioni 49 za wanachama kwenda kununua mapazia bado anakuja kazini.Ningekua na mamlaka ningewalawiti bila mafuta nyinyi.
 
Unanipangia Hela yangu niitumieje f*!*+#
 
Ni ujinga labda miaka ya kustaafu ipunguzwe Hadi kufikia miaka 40 maana wengi hufa mapema kutokana na mtindo wa maisha ya sasa
Ukifa mapema kuna wategemezi wako ambao unawapenda sana na wanakutegemea wewe kuendesha maisha yao kama mtoto na mke au hata mume..
Hao watakuwa wanufaika wakubwa na utawapunguzia changamoto za kimaisha ambazo zingekuwepo kutokana na wewe kutokuwepo nao..
*Elimu ya watoto inaweza kuendelea
*Mke/mume anapata hata mtaji wa kuanzisha kabiashara kakuwaingizia kipato.
Na wengine wanatoa mpaka msaada wa kukuzika kama mwanachama wao...
 
Hapo chini umesahau kutuambia umetumwa na nani? Hii nchi chawa wamekuwa wengi sana.
🤔🤔 Hayo ni maoni yangu mkuu.
Serekali inajitahidi sana...kuboresha maisha ya MTANZANIA wa kawaida kuanzia kijana mpaka mzee..Na kwa mzee pensheni ya uzeeni ni kila kitu baada ya bima ya afya.
KWANZA UNA BIMA YA AFYA WEWE??
KUNA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII UNATOA MPAKA BIMA ZA AFYA BURE KWA WANACHAMA WAKE WALIOPO MAKAZINI, UNATIBIWA WEWE NA FAMILIA YAKO.
Hii mifuko ya hifadhi ya jamii ipo kumsaidia mwanachama .
 
[emoji848][emoji848] Hayo ni maoni yangu mkuu.
Serekali inajitahidi sana...kuboresha maisha ya MTANZANIA wa kawaida kuanzia kijana mpaka mzee..Na kwa mzee pensheni ya uzeeni ni kila kitu baada ya bima ya afya.
KWANZA UNA BIMA YA AFYA WEWE??
KUNA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII UNATOA MPAKA BIMA ZA AFYA BURE KWA WANACHAMA WAKE WALIOPO MAKAZINI, UNATIBIWA WEWE NA FAMILIA YAKO.
Hii mifuko ya hifadhi ya jamii ipo kumsaidia mwanachama .
Ni mfuko gani huo mkuu? Hebu tueleze kidogo tuelewe

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
"ukiigawanya 7.5 /miezi 12 unakuwa na laki 625,000 kila mwezi kwa maisha yako yote yaliyobaki hata kama utaishi miaka 60 mingine"

Mkuu unauhakika na ulichoandika!?, Sio kwamba serikali inamlipa mnufaika kila mwezi, kwa muda wa miaka 12 tu baada ya kustaafu!?.
 
Swali ni je nikifa baada ya miaka 5?
Af pia unasema wategemezi watafaidika, kwan watalipwa maisha yao yote?
Wacheni kutuchota. Kwanza kufuatilia mafao tu ni kazi kuna wazee wanakufa wakiwa wanazunguka korido za NSSF kufuatilia mafao.
Mtu kasota kazini miaka yake yote na ikifika kwenye mafao bado anadaiwa rushwA?
Wapeni wazee hela zao zote bana, hilo ni jasho lao msijifabye mnajua saaana watatesekaje hela ikiisha.
Bora ungekuja na wazo la kuwapa hyo lunpsum kubwa but in maybe 3 phases ndani ya miaka 5-10. Ili kwamba wale wanaopata mshawasha wa hela nyingi akichoma phase y kwanza akili itakaa sawa hzo phases nyingine.
Msijifabye mna uchungu sana bladihenken. We ni chawa tu na sijui umatumwa na nan.
 
vp mstaafu kama ana biashara yake ashaianzisha tayari, anasubiria hiyo pension iongeze mtaji biashara ikue zaidi awaachie urithi mzuri zaidi.
 
Sikuhzi kuna access ya mikopo sidhan kama kuna mtumishi anaweza fanya kazi miaka 30 hajajenga au kua na biashara...iyo Mosi

Pili ,life expectancy Tanzania is 66Years So kama unataka kutengeneza point fulani angalia kila kitu,Hela zake unampangia matumizi?Ukimpa nyingi blablablah kwani ni fedha zako ama zake?
 
mtoa mada unapakuliwa mbona wabunge mawaziri na viongozi wakubwa wakimaliza muda wao wanapewa mafungu yao wakajimalize mbele wenyewe alaf unaleta mada za watumishi kukadiriwa pensheni zao acha ufaken ww utaliwa kiboga ukiendeleza uchawa wa namna hio
 
Back
Top Bottom