Pentekoste iliyochangamka

injili haitegemei pesa kabisaaa ili isonge mbele. kama hukujua biblia imekuwa ikihubiriwa na maskini. yesu hakuwahi kuwa mtu wa injili ya pesa, hata biblia inasema mmepewa bure toeni bure.
 
nakumbuka kuna ndugu yangu mmoja alienda kuonana na mtu mishi ni hela kibao
 
mtumishi anapewa elfu 20 anaitupa anasema unataka muujiza alafu una 20000.
na vipofu wangali wapo na wamekaa kinyenyekevu.
pentekoste imepotea kwa kukosa maarifa
 
Wewe sio kwamba hujui biblia hasha! Unaijua vizuri tu. Tatizo lako Ni pale unapowaponda watumishi wa Mungu.

Kumbuka unapowaponda hata wao kwa upande wao na waumini wao wanakuponda wewe Tena wanasema mmepotea.

Tufike mahala tujitambue wakristo kuacha kupondana watu wa Imani moja. Wale wazee walikuwa wakifanya hivyo kugombea waumini nakutaka sadaka. Lakini haimaanishi sio watu wa Mungu. Kuwasaidia hao Ni kwa kuwaambia na sio kuwaleta public ili watu wa Imani tofauti wajue udhaifu wenu, tutawavutaje kwa Mungu?

Unalofanya unawafungia watu kuja kwa yesu bila kujua
 
MKUU

KUNA WACHUNGAJI WAKONGWE WAMECHOMOKA WAMEANZISHA MAKANISA YAO

UTAELEWA. NZI NA NYUKI AZIKAI PAMOJA

CC
AHMED ALLY
 
hivi kaka inamana hujui si kila ajiitae mtumishi ni wa mungu. soma hapa.
Mathayo 7:21-23
[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


yesu kamwe hajawahi kuwa na ushirika na hawa wapendao umaarufu na pesa.
hakupatana na mafarisayo wala masadukayo wala waandishi .

wengi wajiitao wakristo hata hawajui kuwatambua watumishi wa mungu.


MUNGU HAJAWAHI KUTUMA MANABII WAWILI KWA WAKATI MMOJA KUMBUKA ILO,
MUSA MUSA, ELIYA ELIYA,YOHANA YOHANA N.K
 
una ushahidi wa kimaandiko?
ATCS 2;1 And when the day of Pentecost was fully come, they were all with one accord in one place. 2 And suddenly there came a sound from heaven as of a rushing mighty wind, and it filled all the house where they were sitting. 3 And there appeared unto them cloven tongues like as of fire, and it sat upon each of them. 4 And they were all filled with the Holy Ghost, and began to speak with other tongues, as the Spirit gave them utterance.
 
MKUU

KUNA WACHUNGAJI WAKONGWE WAMECHOMOKA WAMEANZISHA MAKANISA YAO

UTAELEWA. NZI NA NYUKI AZIKAI PAMOJA

CC
AHMED ALLY
soma hapo kaka
1WAKORINTO 1;10
Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la
Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia
zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano
katikati yenu na kwamba mwe na umoja
kikamilifu katika nia na katika kusudi. 11Kwa
maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka
kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe
kwamba kuna magomvi katikati yenu. 12Maana
yangu ni kwamba: Kila mmoja wenu husema,
“Mimi ni wa Paulo,” mwingine, “Mimi ni wa
Apolo,” mwingine “Mimi ni wa Kefa” na
mwingine “Mimi ni wa Kristo”.
13Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye
aliyesulibishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa
kwa jina la Paulo?
 
si kwamba alimradi mtu anafanya miujiza ni mtumishi wa mungu kaka. fumbuka macho uweze kuonaa. maandiko yapo wazi
 
Kila nikikumbuka injili ya akina Bishop Moses Kulola (Ulokole), Mch.Geoffrey Mbwana (SDA) na Reinhard Bonke (Ulokole) Kisha nikawaangalia Hawa akina sijui Mwamposa, Suguye, Zumaridi, Alex Malasusa na wengineo nasema INJILI ISHAKUFA kifo cha mende.
ama hakika hakuna injili kwao kabisa, ni ma motivator na wanasaikolojia
 
Kwa hilo hilo andiko "utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtazidishiwa" je kama wameutafuta ufalme na wamezidishiwa?
 
Kwa hilo hilo andiko "utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine mtazidishiwa" je kama wameutafuta ufalme na wamezidishiwa?
ukiupata maisha yako yanajulikana

Mathayo 6:30-34
[30]Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
(
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

mtu anayeutafuta ufalme wa mbinguni anakuwa na wengi wa naoutafuta ufalme wa duniani.
 
Mkuu wapo wachungaji/ watumishi hawahubiri miujiza na biashara na wana maisha magumu,je hao bado wanautafuta ufalme ndo maana hawana mali?
 
Mkuu wapo wachungaji/ watumishi hawahubiri miujiza na biashara na wana maisha magumu,je hao bado wanautafuta ufalme ndo maana hawana mali?
soma maandiko yako yoote tangu kuja kwa yesu.
nionyeshe mtumishi mmoja aliekuwa tajiri.
mungu haamini katika utajiri na injili.
ni ngumu tajiri kuuona tuu ufalme wa mungu.

maisha ya yesu na mitume yafattilie. utagundua yanafanana.
yes alisema hakuja kuleta amani.
wala kumfata hakuna raha za ulimwengu.
 
Sipo kwa mwamposa Mimi Wala maisha yangu hayana uhusiano na mwamposa kabisa. Namtumia mwamposa kuwakilisha watumishi wa Mungu wote ambao wanapitia vijineno neno.

Maana Tanzania yetu watu wakishakuwa maarufu tu lazima maneno.
Sasa akili yako imewaza na kuwazua ikashindwa kutofautisha taasisi na mtu binafsi?

Yaani RC inayoendesha shughuli mbalimbali za kijamii kama vile utoaji huduma za afya, elimu nk unataka kulinganisha na Mwamposa ambaye fedha zote zinazoingia kanisani zinakuwa kama mali yake binafsi?
 
Sa Roman imeingiaje hapo jmn
 
Kwani wakati roman inaanza ilikuwaje? Nayo ilikuwa hivyohivyo ikaanzisha matawi mikoa na hatimae nchi mbalimbali Hadi dunia nzima kulingana na uongozi tofauti uliokuwa ukiingia. So hata Hawa makanisa Kama TAG ilianza mkoa mmoja hatimae nchi nzima kulingana na uongozi na utimamu/ ushawishi wa viongozi.

Huyu mwamposa unaona Kama fedha zinaingia kwake lkn hawezi ishi milele ataondoka watakuja wengine na Kama watakuwa smart watapeleka huduma hadi duniani.
 
Makanisa ya ki hip-hop, ..mchungaji anabweka waumini wanabweka basi inakuwa tafrani, yaani unaenda kanisani na Panadol mfukoni maana mpaka ibada inaisha kichwa kinakupasua hatari maskio ndo usiseme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…