Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Wewe unasema akina Messi, Inesta na Xavi ndio walimfanya Guardiola kuwa bora.Nitakununulia huo mvinyo bila tashwishwi yeyote ile, tena mimi ndo nitakukumbusha, tatizo hiyo siku haitakuja kutokea tena.
Hapo hapo kwa Enrique ndo mnapojifunga sababu Luis kashinda kila kitu ambacho Pep alishinda Barca, hata baada ya kuondoka kwa Xavi bado Luis alishinda UCL na ligi, je nae ni kocha bora mithili ya Pep? Ila Luis huyo huyo alifeli vibaya alipokuwa Italy kabla ya kwenda Nou Camp. Ndo maana tunasema Messi, Iniesta na Xavi walifanya makocha waonekane bora ilhali hawana lolote lile.
Tafadhari wasikie Telegraph wanavyosema hapo chini:
"Pep Guardiola’s 2008-12 spell in charge of Barcelona was when Xavi truly excelled and won the bulk of his trophies. He translated his manager’s demands and ideas into spellbinding performances on the pitch, managing to record 100 per cent passing accuracy several times when frequently passing the ball over one hundred times per game."
Zingatia maneno yaliyokolezwa wino mweusi. Kabla ya Guardiola Xavi na wengine walikuwepo lakini hawakuwa na ubora kama wakati wa Guardiola.
Source: Xavi: The greatest midfielder of a generation