Si kweli kwamba pep alimkuta Andre Iniesta yupo kwenye pick. Ukweli ni kwamba pep ndio alimpa nafasi Iniesta tena baada ya kumuuza Deco. Kumbuka Xavi na Deco ndio walikuwa viungo bora pale baca. Pep amepandisha vijana kibao toka kule timu b. Pedro, Busquet, Montoya, mark Batra, na winga mmoja hivi jina nimelisahau. Pep ndio alimuuza Keita ili kumpa nafasi Busquet baada ya kujiridhisha kuwa Busquet ni bora kuliko keita. Watu wakatoa povu ooh jamaa ni mbaguzi.
Kaja epl kakuta man city ina magalasa kibao. Kaijenga timu. Kaondoa magalasa na wazee. Kachukua vijana. Sane, Jesus, Sterling,Stone,nk. Eti mchezaji kama Fabian Delph naye kwa sasa ni bonge la mchezaji. Pep kambadilisha kabisa. Alikuwa wa kawaida.
Kingine. Kwa wale ambao mnategemea maajabu mtasubiri sana. Hivi mnajua kuwa mmiliki wa man city ndie anayemiliki club ya Girona iliyopo kule Catalona? Sasa kwa taarifa yenu tu city ina vijana wasiopungua 6 wenye vipaji vya kweli ambao wamesajiliwa na kupelekwa pale Girona kukuza vipaji.
Hawa watakuwa kama ilivyokuwa kwa Lucas Vazquiz na Asensio wa madrid. Walisajiliwa na kupelekwa kwa mkopo kwenye vilabu vingine. Sasa wamerudi na kazi zao mnaziona. Nasema Pep akikaa City kwa miaka 5 itakuwa ni ligi ya timu 1 tu.