Kabla Pep hajaenda Man City nilikuwa nina mawazo kama ya huyu jamaa.
Baada ya Pep kujoin City, akachukua Ubingwa kwa points 100 msimu wa 2017/18 nikabadili mtazamo, nikasema ngoja nione nini atafanya msimu unaofata.
Alipata upinzani wa hali ya juu sana kutoka kwa Liverpool msimu wa 2018/19, lakini alipambana mpaka akawa bingwa kwa points 98, akimwacha Liverpool kwa point 1 tu.
Kwa mara ya kwanza timu inakusanya points 198 EPL ndani ya misimu miwili, ligi tunayoiamini kwa ushindani.
Kwa mara ya kwanza timu inamaliza na points 97 na haiwi bingwa (kisa Pep).
Pep alimaliza ligi y 2017/18 akiwa na points 100 na magoli zaidi ya 100. All EPL records.
Kwa vipimo hivyo nilivyovieleza hapo juu, Pep kwangu ni kocha bora, nadhani naweza kumweka kwenye top 3 kwa makocha walioko sasa.