Laki 5 kuna route kama 3 kwa desktop
1. Nunua Machine zenye Apu za Ryzen, za 2400G ni around 250K na zenye 3400G ni kama 400K, utofauti wa perfomance baina ya hizi mbili sio mkubwa sana, hio kwa Fifa na pes zinatosha kuanzia. Huna haja ya gpu kuanzia labda kwa baadae, gharama extra ni ku upgrade ram kwenda 16GB (ram mbili za 8GB zenye speed moja)
2. Ununue machine ya intel gen ya 8, i5 ama i7 hizi around laki 4 unapata, sometime chini ya hapo, then unatafuta low profile gpu kama GT 1030, Rx 550, quadro 620 etc unaweka unacheza games.
3. Utafute workstation kama HP Z2xx series ama Dell precision, Lenovo Thinkstation etc gen ya 8 kupanda kwa hio budget unapata ama inaweza zidi kidogo halafu utafute Rx580 mbele ya safari.
Kama ndio unaanza na recomend zaidi option ya kwanza ili usichanganyikiwe mbele ya safari..
Kwa Laptop ukipata i3 ama ryzen 3 za kisasa ni bomba zaidi, kuna i3 1215U na Ryzen 5300U zote hizi zina nguvu na uwezo mzuri kiasi chake wa graphics, hii i3 nimewahi ona inatangazwa laki 7, na hio Ryzen nimeona mdau humu kanunua Laki 6, so probably ukitafuta vizuri around budget yako ukapata.
Ukikosa tafuta laptop za Ryzen 2500/3500U hizi unapata 200,000-400,000, ama tafuta Intel gen ya 8 lakini iwe na Nvidia gpu lowend kama Mx150, mx130 etc unaweza pata hio budget.