Pesa ilikuwa ndiyo sifa ya kwanza kwenye kura za maoni CCM

 

Attachments

  • VID-20200726-WA0000.mp4
    2.6 MB
Wazo la Magufuli ilikuwa Vijana washiriki katika siasa,ambao wengi wangetoa hela ya fomu tu Tshs.100,000 tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni 3M-5M kumbe huu utaratibu ndio hovyo bora ule wa mwanzo wa wanachama wote.

Imagine Mawaziri wa magufuli karibu wote wameongoza katika kura za maoni huku wengi tunajua fika katika majimbo yao wanachechemea na wamechokwa,ila sababu ya hela wamepenyeza kirahisi sana.

Ingekuwa ni utaratibu wa zamani wa wanachama wote kupiga kura, mawaziri wengi wangedo dokea pua.
 
Rushwa ilitawala mchakato wote wa kuwapata wagombea.
CCM wasipochukua hatua madhubuti kukomesha hii hali watakua wameonyesha mfano mbaya kabisa na huku ni kufeli kwa ahadi yao ya kupambana na rushwa
 
Ikibidi wapitishe majina ya wagombea wasafi hata kama italazimika kumchukua mtu aliyepata sifuri lakini hakutumia rushwa kwenye uchaguzi.
Mkuu hilo sahau. Tulia, Kabudi, Jaffo, Majaliwa, Mpango, Ndalichako, etc wote wakatwe kisa akina nonihino wameangukia pua?
 
Mkuu hilo sahau. Tulia, Kabudi, Jaffo, Majaliwa, Mpango, Ndalichako, etc wote wakatwe kisa akina nonihino wameangukia pua?
Kama hao nao walitumia rushwa kupata nafasi zao na kama kutakua na kusitasita kuwachukulia hatua basi vita dhidi ya rushwa haitafanikiwa kwasababu haipiganwi. Wakati wa CCM ya Mwl Nyerere hapakua na double standard za kuwapendelea baadhi ya watoa rushwa na kuwaonea wengine
 
Hujaweka hata evidence ya rushwa
Mkuu rushwa ina harufu mbaya, rushwa inanuka japo haionekani wakati wanapeana kwa kificho au hadharani. Kinachoonekana ni matokeo ya rushwa. Nzi wa uchafu wa rushwa ni kuchagua watu watakaojenga taifa la mambumbumbu wachumia tumbo hata kama ni Phd holders, no msiba kwa taifa
 
Si mlisema kuwa Magufuli karejesha nidhamu na uzalendo?
 
Hakuna cha fedha wala nini hiyo ilikuwa ni tathmini halisi ya jinsi sisi watiania tulivyokuwa tunajisikia wakubwa na kujikweza ndani ya mioyo yetu na jinsi jamii inavyokuona. Mtu yupo kwenye idara amejiona ni mkuubwa akirudi kwao likizo hata wale aliokua nao anawaona malofa, hashirikiani nao kwa lolote ni kujisifusifu tuu,unaondoka kazini kwa mbweembwe na vihela vyako ndio unajifanya unawagawia, wanavipiga na kukuzuga kuwa kura watakupa.Mwisho wa siku unaipata tathmini ya kuwa wewe ni nani kupitia kura za wazi za hadharani kuwa wewe ni SIFURI bin ZERO na kuonyesha ukomavu wa kidiplomasia walikuwa hawakuambii sasa wamepita nafasi kupitia sanduku la kura na sasa wamekuambia wewe ni sifuri sii lolote level ya ukubwa uliojikweza jamii bado inakuona kama sisimizi tuu.jirekebishe
 
Natamani ingekua hivyo mkuu. Kwamba wajumbe walipiga kura kwa maslahi mapana ya Chama na nchi bila ushawishi wa fedha na mali. Kwamba wangetoa ujumbe mzito kwa wagombea kua wanahitaji mgombea aliyekaribu na watu na aliyebeba agenda yao ya kupambana na umasikini, maradhi na ujinga

Bahati mbaya wajumbe hawakua wakiangalia hayo. Waweza kunitajia mgombea hata mmoja aliyeongoza kura za maoni ambaye hajatumia pesa kuhonga wajumbe?
 
Tujikite kwenye nini kifanyike.
Napendekeza CCM tubadili utaratibu wa uteuzi.Tuanze kuteua wagombea kwa kuanza na kuwachunguza kimya kimya (upekuzi au vetting) na kuwateua bila kura za maoni.Utaratibu wa aina hii hutumiwa na kanisa katoliki kuteua maaskofu wake.
Hata hivyo rushwa imepungua kwa kiwango fulani ukilinganisha na wakati wa kura za maoni kupigwa na wanachama wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…