Pesa ilikuwa ndiyo sifa ya kwanza kwenye kura za maoni CCM

Pesa ilikuwa ndiyo sifa ya kwanza kwenye kura za maoni CCM

Tujikite kwenye nini kifanyike.
Napendekeza CCM tubadili utaratibu wa uteuzi.Tuanze kuteua wagombea kwa kuanza na kuwachunguza kimya kimya (upekuzi au vetting) na kuwateua bila kura za maoni.Utaratibu wa aina hii hutumiwa na kanisa katoliki kuteua maaskofu wake.
Hata hivyo rushwa imepungua kwa kiwango fulani ukilinganisha na wakati wa kura za maoni kupigwa na wanachama wote.
Hakuna wakati wagombea wa CCM wamejikita kwenye utoaji wa rushwa Kama uchaguzi huu.wajumbe wa CCM hawataki sera za wagombea wanataka fedha tu.mengine mtakutana October. Wajumbe? Wajumbe? Wajumbe? Acha kabisa
 
Mambo yamebadilika ndani ya CCM. Dosari kubwa ni jinsi mchakato wa kupata wagombea unavyoendeshwa ambapo hakuna tena muda wa mwanachama anayegombea kujieleza kwa undani na kumwaga sera na mipango yake ya maendeleo.

HAKUNA mgombea yoyote katika jimbo lolote aliyepata kura tano na kuendelea ambaye hajatoa rushwa kwa wajumbe wanaopiga kura, HAKUNA. Mambo ya umaarufu na sifa zingine yanafuata baadae. Na hii si siri hata wakuu wa chama wanajua.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya huko nyuma kwamba sasa kwenye CCM pesa imekua ndio qualification ya mtu kuchaguliwa kwenye uongozi wakati hapo awali pesa ilikua ni disqualification.

Hatari yake ni kwamba inajenga utamaduni wa watu kununua kura na kununua chaguzi na hata wale malaya wa kisiasa wanatengenezwa na tabia hii ambayo imeachiwa iote mizizi kitu ambacho sio afya kwa mustakabali wa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.
Inasikitisha sana.
 
Hakuna cha fedha wala nini hiyo ilikuwa ni tathmini halisi ya jinsi sisi watiania tulivyokuwa tunajisikia wakubwa na kujikweza ndani ya mioyo yetu na jinsi jamii inavyokuona. Mtu yupo kwenye idara amejiona ni mkuubwa akirudi kwao likizo hata wale aliokua nao anawaona malofa, hashirikiani nao kwa lolote ni kujisifusifu tuu,unaondoka kazini kwa mbweembwe na vihela vyako ndio unajifanya unawagawia, wanavipiga na kukuzuga kuwa kura watakupa.Mwisho wa siku unaipata tathmini ya kuwa wewe ni nani kupitia kura za wazi za hadharani kuwa wewe ni SIFURI bin ZERO na kuonyesha ukomavu wa kidiplomasia walikuwa hawakuambii sasa wamepita nafasi kupitia sanduku la kura na sasa wamekuambia wewe ni sifuri sii lolote level ya ukubwa uliojikweza jamii bado inakuona kama sisimizi tuu.jirekebishe
Aliye vaa viatu ndio anajua kiatu kimebana wapi usiongee bila uhalisia,kuna watu wengi sana wamejitoa katika kushirikiana jamii katika kazi nyingi tena wengine ni viongozi ndani ya jamii zao but wakipigwa chini.
Kule ilikuwa ni fedha pasipo fedha huwezi penyeza hata kidogo.
 
Mambo yamebadilika ndani ya CCM. Dosari kubwa ni jinsi mchakato wa kupata wagombea unavyoendeshwa ambapo hakuna tena muda wa mwanachama anayegombea kujieleza kwa undani na kumwaga sera na mipango yake ya maendeleo.

HAKUNA mgombea yoyote katika jimbo lolote aliyepata kura tano na kuendelea ambaye hajatoa rushwa kwa wajumbe wanaopiga kura, HAKUNA. Mambo ya umaarufu na sifa zingine yanafuata baadae. Na hii si siri hata wakuu wa chama wanajua.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya huko nyuma kwamba sasa kwenye CCM pesa imekua ndio qualification ya mtu kuchaguliwa kwenye uongozi wakati hapo awali pesa ilikua ni disqualification.

Hatari yake ni kwamba inajenga utamaduni wa watu kununua kura na kununua chaguzi na hata wale malaya wa kisiasa wanatengenezwa na tabia hii ambayo imeachiwa iote mizizi kitu ambacho sio afya kwa mustakabali wa CCM yenyewe na nchi kwa ujumla.
Si huwa wanasema mh rais amekomesha vitendo vya rushwa, au huwa wanamaanisha rushwa ipi ?
 
Mtu ambaye hana pesa atakuwa na Sera gan , hao ukiwapa uongozi wanaenda kukomboa ukoo wao wa kimaskin badala ya wananchi , kigezo cha Kwanza cha mgombea anatakiwa awe na pesa chafu , istoshe maendeleo ya jimbo yanategemea mikakati ya serikali kuu, ubunge ni bortion tu.
Hivi Obama wakati anagombea alikuwa tajiri kama au kumzidi Donald Trump ?
 
Mtoa mada umeleta mada nzuri lakini uwasilishaji wake hauko sawa. Imeshahukumu na hiyo si sawa. Toa mifano halisi kuliko kuonesha kuwa hali ndio ilikuwa hivyo Kila sehemu.

Jenga hoja vizuri ili iweze kushughulikiwa. Serikali hii inachukia rushwa kwa vitendo
 
Si huwa wanasema mh rais amekomesha vitendo vya rushwa, au huwa wanamaanisha rushwa ipi ?
Anamaanisha amekomesha Rushwa ndani ya serikali yake Ila huko ccm bado haijafika huko kupambana nayo. Tusubiri Ila huko ni pagumbu kupambana na Rushwa,Kati ya vinara ndani ya CCM waliotoa rushwa kwenye uchaguzi wa Kura za maoni wanao ongoza ni prof. Muhongo, sajini,ole sendeka, Dr mathayo David, aliye kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Dr molel na agrey mwandri wa siha, sashisha wa hai, Ibrahim shayo na priscus wa moshi mjini, fred lowasa wa monduli, mnyeti hapa misungwi,kurwa biteko ,marium kaaya katibu wa CCM Kule Moshi vijijini, na weng.
Mtoa mada umeleta mada nzuri lakini uwasilishaji wake hauko sawa. Imeshahukumu na hiyo si sawa. Toa mifano halisi kuliko kuonesha kuwa hali ndio ilikuwa hivyo Kila sehemu.

Jenga hoja vizuri ili iweze kushughulikiwa. Serikali hii inachukia rushwa kwa vitendo
 
Anamaanisha amekomesha Rushwa ndani ya serikali yake Ila huko ccm bado haijafika huko kupambana nayo. Tusubiri Ila huko ni pagumbu kupambana na Rushwa,Kati ya vinara ndani ya CCM waliotoa rushwa kwenye uchaguzi wa Kura za maoni wanao ongoza ni prof. Muhongo, sajini,ole sendeka, Dr mathayo David, aliye kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Dr molel na agrey mwandri wa siha, sashisha wa hai, Ibrahim shayo na priscus wa moshi mjini, fred lowasa wa monduli, mnyeti hapa misungwi,kurwa biteko ,marium kaaya katibu wa CCM Kule Moshi vijijini, na weng.
Hata Pr Muhongo anafanya mambo kwa kutegemea rushwa ?
 
Kiukweli rushwa imeenda km kawaida, mfumo wa wajumbe kuongeka rahisi na wanadhibitika, kuondokana na janga ili, mfumo wa wanachama wote kushiriki kura za maoni ndio ilikuwa busara.
Naamini rufaa zitakuwepo wakishutumiana, na hata takukuru ni binadamu, wanaowafeva uwaachia tu waongane! Tuna tatizo kuletewa wagombea waliowashibisha wao uenda wasiwe na ushawishi kwa wananchi, kazi itaanza hapo!
 
Back
Top Bottom