Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Pesa sio kipimio sahihi cha uzalishaji wa vitu.
Chukulia mfano, mtu anaponda kokoto kwa kutumia mkono kwa siku 20 na kuweza kujaza tipa, na mwishowe analipwa laki 1; wakati huo huo mwingine ameudhuria kikao cha nusu saa tu, anapata laki 5; hii haiko sawa.
Mkulima anatumia muda mwingi kwenye kilimo, na baada ya mavuno, gunia anauza elfu 30 au 40; wakati huo huo boda boda anaingiza hiyo hela kwa siku; hii haiko sawa.
Fundi ujenzi anajenga boma lote kwa shilingi milioni moja, na kugawana hiyo pesa na vibarua wake; wakati huo huo, mwingine yuko ofisini anafanya kazi za kawaida anapata zaidi; hii sio sawa.
Kwa mazingira haya, bora mfumo wa kubadilishana vitu (barter trade), urudi; ukitaka gunia la mahindi, leta gunia la mpunga; ukitaka ng'ombe leta mbuzi watano; ukitaka mafuta leta asali lita 20; ukitaka kuku leta samaki n.k
Hii itafanya watu wazalishe vitu vinavyoonekana, na vyenye thamani halisia.