sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Katika hali kama hii ndipo unapoona wazi wazi bila kificho kwamba pesa zina elements kubwa sana za ushetani.
Mchezaji wa PSG (timu hii inamilikiwa na shehe tajiri) wiki iliyopita alikataa kuvaa jezi yenye rangi za kuunga mkono ushoga, usagaji na kubadili jinsia, sababu yake kuu ni kwamba ni kinyume na asili yake na pia dini yake hairuhusu.
Sasa ishu inapokuja ni kwamba mchezaji huyu analipwa milioni 200 kila wiki na watu wanaofanikisha hilo jambo wao wanapenda kuunga mkono ushoga, wamechukizwa na mchezaji huyu kutovaa jezi na kwa sasa imembidi mchezaji achague kimoja kati ya kitita cha milioni 200 ama kurudi Afrika.
Muafaka bado haujafikiwa hadi sasa japo kuna picha za uzushi kama niliyoambatanisha zinasambaa .
Je ni kipi atakichagua kati ya milioni 200 za kila wiki ama kurudi afrika.
wachezaji wengine wa kiislam wakiwemo Benzema, Kante, Pogba, n.k wao wanavaa kama kawaida.