Pesa Sio kila Kitu unajidanganya

Mungu ni mmoja tu ndiye ninaemzungumzia. Muumba wa mbingu na nchi pamoja na mimi na kila kitu.

Hii ni kwa imani yangu, naheshimu ya kwako japo kwangu sio sawa.
Physically HAUWEZI, Spiritually UNAWEZA.

Ukiamka umekata kamba hata hayo matrilioni hauwezi kuyalipa, uhai wako ni nini?

Hauwezi kupata pesa ya kulipa Bill bila Mungu kwanza
Hauwezi kwenda kulipa Bill bila uhai kwanza

TAFAKARI
Ningependa kuelezewa maana ya dhana "Mungu" kabla hujaendelea.

Dhana au neno "Mungu" ni nini? Au ni nani? Ni kitu gani?
 
Watu wanajifanya wanapinga huku sote tunajua kuwa ndugu zetu wapo wengi huko vijijini hawana pesa na bado wanaishi tena maisha ya furaha-na barter trade bado inafanya kazi kwa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa au huduma kwa huduma.
Mfano kijijini kwetu kama wewe ni mgonjwa huna hela utaenda kwa mganga utatibiwa ukipona utapewa kipande cha Shamba utalima mnamalizana.
 
Ningependa kuelezewa maana ya dhana "Mungu" kabla hujaendelea.

Dhana au neno "Mungu" ni nini? Au ni nani? Ni kitu gani?
Kwanza neno Mungu ni jina la utambulisho likitamkwa mtu anatambua unaongelea nini. Wengine husema God, Allah,Yehova Adonai, Brahma nk. Kutegemeana na jamii husika.

Mungu ni nguvu (power or energy). Unaweza kujiunganisha na hiyo nguvu kutekeleza jambo lolote unalotaka. Lazima uzingatie kanuni za matumizi ya hii nguvu.

Mfano, Umeme ni nguvu iliyopewa jina la umeme. Mtu anaweza kuunganisha jiko kwenye hii nguvu akapika, balbu ya kijani, nyekundu au bluu akapata mwanga anaotaka, pasi akanyoosha nguo. Lakini kufanya yote haya lazima kuzingatia kanuni za matumizi vinginevyo itakuwa majanga.

Kwa ufupi, sijui kama nimeweza kujibu ulichotaka
 
Kosa pesa ukose vyote.
Bila pesa huna access na huduma bora ya afya.
Huna pesa muda mwingine hata amani ndani inakosa. Watoto wanalia njaa, wana mahitaji unakosa kuyatimiza, una madeni kwa mangi.
Bila pesa hata kilimo cha kisasa huwezi kukifanya unaishia kulima ili tu upate chakula cha kusukuma siku.
Katika dunia ya sasa pesa ni muhimu sana sana maana hata huko kwenye nyumba za ibada wanaiba toa ndugu toa kile ulichonacho kingine.
 

Mtupori huenda unaishi karne iliyopita mwenzetu, mchango mzuri though! Amani na Afya unailindaje bila fweza mwenzetu?
 
Kwanza neno Mungu ni jina la utambulisho likitamkwa mtu anatambua unaongelea nini. Wengine husema God, Allah,Yehova Adonai, Brahma nk. Kutegemeana na jamii husika.
Sawa tuko pamoja πŸ‘πŸΎ
Mungu ni nguvu (power or energy). Unaweza kujiunganisha na hiyo nguvu kutekeleza jambo lolote.
Anhaa....!! kumbe kwa maelezo yako "Mungu" ni nguvu ambayo ndiyo imeiunda hii dunia na tunaweza kuitumia kwa manufaa fulani?

Kwamba ni kama nguvu ya umeme na kwa uelewa wangu mkuu, vyanzo vya nguvu ya umeme ni vingi mfano:

Renewable sources - Maji[H.E.P], Upepo[Turbines], Jua[Solar], Mawimbi ya bahari[Tidal].

Non-renewable sources - Oil, Natural gas, Nuclear fossils.

Kwakua umeme unajikana chanzo chake ni nini?

Ningependa uendelee kunifundisha ni nini Chanzo cha "Mungu"?.
 
Ndugu, hii nguvu is neither created nor destroyed. Na kila kitu ni nguvu, kimeundwa na nguvu.

Ni Alfa na Omega kwa watu wa dini

Kwa wana sayansi ni Neither Created nor destroyed.

Ipo na itakuwepo
 
Unaposema pesa sio kila kitu hakikisha unazo kwanza ndo useme.
 
Ndugu, hii nguvu is neither created nor destroyed. Na kila kitu ni nguvu, kimeundwa na nguvu.

Ni Alfa na Omega kwa watu wa dini

Kwa wana sayansi ni Neither Created nor destroyed.

Ipo na itakuwepo
Kwa muongozo wako Mungu ndiyo "Energy".


Hii Energy[Nguvu] ambayo Sayansi inatuambia "Energy can neither be created no destroyed but can change in different form", Hata sayansi yenyewe haijajua ilitokeaga wapi hadi leo hii.



Lakini wewe hapo nyuma ukanifundisha kwamba hii Energy/nguvu ni "Mungu" na ukasema ukiitaka hii nguvu mda wowote unaipata [Hujasema hivi?], ila mimi nikakutaka uniambie chanzo cha "Mungu" ni nini?


Umerudi kunijibu tena "Mungu" ndiyo hiyo hiyo nguvu ambayo yeye ndiye kaiumba "So confusing" ,,,,,,,,,!πŸ˜‡πŸ˜‡


Ngoja nikulize swali kwa uzuri sasa : Huyo "Mungu" pamoja na hizo "Nguvu", vyote kwa pamoja chanzo chake ni nini?
 
Pesa si kila kitu lakini hata kuandika pesa si kila kitu hapa JF umehitaji internet inayolipiwa kwa pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…