Pesa za kichawi na kishirikina (Ndagu n.k)

Pesa za kichawi na kishirikina (Ndagu n.k)

Light saber

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2017
Posts
4,368
Reaction score
7,935
Najua wewe mwanajamii mwenzangu ushawahi kusimuliwa ama kusikia kuhusu fedha hizo, au mtu mwenye nazo, au uko nazo basi huu ni uzi wa kushare nasi visa hivyo.

Mimi niliwahi kusikia tajiri mmoja hivi huwa analala chini, na ana noti ya tsh elfu kumi ambayo haitumiagi miaka nenda rudi ndo inayomlindia pesa zake.

Mwingine huwa anaoza ndo pesa zinaingia,wengine ati wana vidonda visivyo pona kadri vinavyooza ndo pesa zinaingia and so many blah blah blah.

Karibu share nasi.
 
Jana nilikuwa natembea tembea nikafika mahala gari yangu ikamaliza mafuta ikabidi niende sheli nikaweke mafuta wakati dada mmoja ananiwekea mafuta nikawa nimetelemka kama kuingalia gari yangu kwa nyuma nilihisi kuwa labda jamaa mmoja amenikwaluza nikiwa naandalia gari nikaonana na jamaa ambaye tulisoma naye chuo mimi nikawa nimepata kazi ya kuajiliwa nataka kuondoka jamaa ana hammer yake tukaenda hoter mmoja yenye ghalama ile mbaya tukakaa nikaanza kuuliza vipi bwana pesa ulipata wapi
jamaa akaanza kucheka sana akasema kuwa kama nataka utajiri nimwambie tu anipe nikamwambia kuwa hebu nipe jamaa akasema kuwa anipeleke kwa mganga ambaye atanipa dawa ya utajiri ambayo kafara yake ni wanawake wenye tamaa na hela tu wewe unamwita demu tu akishakuja tu wewe unampa hela halafu unaanza kumwambia kuwa baby nimepigiwa simu poa niende ila usitembee naye tu hela zako zinaanza kuongezeka tu na yeye ataandamwa na matatizo mengi sana
nilichojifunza jana kumbe wanawake wanaopenda hela wanashida sana imebidi leo nipige maombi kabisa jamaa baadae nikamuacha ili niwahi nyumbani leo
 
Kuna jamaa kule kwetu nasikia halalagi kwenye kitanda, huwa analala juu ya magunia ya bidhaa zake kama mchele na mahindi.

Alikuwa na fremu za duka kadhaa, fremu moja alikuja kuifunga ghafla, na haikufunguliwa miaka na miaka. Ile fremu iliota majani mpaka yakatokeza nje, ilikuwa na uzio wa kuweka bidhaa kwa nje na kulikuwa na baiskeli lkn aliiacha palepale miaka na miaka.

Sijaenda siku nyingi maskani nikienda nitawaletea mrejesho kama ilishafunguliwa ama bado.
Unforgetable
 
Kuna mzee mmoja walienda kwa mganga wapate utajiri...wakapewa masharti kua mwenye nyota mbaya ndie atakufa...wakapata m12 kwenye machimbo...wakati wakurudi wakapata ajali mmoja akafa...mmoja akaendelea kufaidi.. TRUE STORY NILISIMULIWA NA MGANGA ALIYE WAPA UTAJIRI.
 
Kuna mwengine tunaishi mtaa mmoja... yeye havai suruari.. hata akinunua mpya lazima aikate chini.. na kila mwaka anabadili pikipiki..
 
najua mkuu ila share nasi hizo myth moja mbili tatu ulizowahi sikia.

Mambo mengi sana mkuu.

-Kuna jamaa ana semi trailer za kutosha ila aliambiwa na mganga wale awe rafu rafu tu,kwake mboga kuu ni maharage na mchicha chukuchuku,viatu vyake ni mayebo yebo na makatambuga ya matairi ya gari.

-Mwingine alikuwa anamiliki mabasi ya mkoani yeye alipewa masharti kwamba awe anajisaidi porini tu.

-Mwingine kwamba asimgonge mkewe etc
 
Kuna mzee hapa jirani Ni Don ila yeye analalaga kwenye mashine yake ya kusaga unga na Kuna kofia anavaaga Ni chakavu mno na huwa aibadili kamwe!!

Jamaa ana fuso za kupakia nafaka na majumba kibao ya kupangisha

Ana macho mekundu mno akikuangalia tu lazima uogope
 
Back
Top Bottom