Pesa za kichawi na kishirikina (Ndagu n.k)

Light saber

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2017
Posts
4,368
Reaction score
7,935
Najua wewe mwanajamii mwenzangu ushawahi kusimuliwa ama kusikia kuhusu fedha hizo, au mtu mwenye nazo, au uko nazo basi huu ni uzi wa kushare nasi visa hivyo.

Mimi niliwahi kusikia tajiri mmoja hivi huwa analala chini, na ana noti ya tsh elfu kumi ambayo haitumiagi miaka nenda rudi ndo inayomlindia pesa zake.

Mwingine huwa anaoza ndo pesa zinaingia,wengine ati wana vidonda visivyo pona kadri vinavyooza ndo pesa zinaingia and so many blah blah blah.

Karibu share nasi.
 
 
Kuna jamaa kule kwetu nasikia halalagi kwenye kitanda, huwa analala juu ya magunia ya bidhaa zake kama mchele na mahindi.

Alikuwa na fremu za duka kadhaa, fremu moja alikuja kuifunga ghafla, na haikufunguliwa miaka na miaka. Ile fremu iliota majani mpaka yakatokeza nje, ilikuwa na uzio wa kuweka bidhaa kwa nje na kulikuwa na baiskeli lkn aliiacha palepale miaka na miaka.

Sijaenda siku nyingi maskani nikienda nitawaletea mrejesho kama ilishafunguliwa ama bado.
Unforgetable
 
Kuna mzee mmoja walienda kwa mganga wapate utajiri...wakapewa masharti kua mwenye nyota mbaya ndie atakufa...wakapata m12 kwenye machimbo...wakati wakurudi wakapata ajali mmoja akafa...mmoja akaendelea kufaidi.. TRUE STORY NILISIMULIWA NA MGANGA ALIYE WAPA UTAJIRI.
 
Kuna mwengine tunaishi mtaa mmoja... yeye havai suruari.. hata akinunua mpya lazima aikate chini.. na kila mwaka anabadili pikipiki..
 
najua mkuu ila share nasi hizo myth moja mbili tatu ulizowahi sikia.

Mambo mengi sana mkuu.

-Kuna jamaa ana semi trailer za kutosha ila aliambiwa na mganga wale awe rafu rafu tu,kwake mboga kuu ni maharage na mchicha chukuchuku,viatu vyake ni mayebo yebo na makatambuga ya matairi ya gari.

-Mwingine alikuwa anamiliki mabasi ya mkoani yeye alipewa masharti kwamba awe anajisaidi porini tu.

-Mwingine kwamba asimgonge mkewe etc
 
Kuna mzee hapa jirani Ni Don ila yeye analalaga kwenye mashine yake ya kusaga unga na Kuna kofia anavaaga Ni chakavu mno na huwa aibadili kamwe!!

Jamaa ana fuso za kupakia nafaka na majumba kibao ya kupangisha

Ana macho mekundu mno akikuangalia tu lazima uogope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…