Pesa za silva zinapotea mtaani

Pesa za silva zinapotea mtaani

Hivi karibuni mtaani kumekuwa na uhaba wa pesa za sarafu kwa maana hamsini, mia, mia mbili, na mia tano.

Imefikia hatua makonda wa daladala wanapata shida ya kupata chenchi za kuwarudishia wateja kwa sababu ya hii kadhia.

Ukienda dukani na elfu kumi, unaweza unaweza usihudumiwe kwa sababu ya ukosefu wa chenchi. Sio sarafu hata pesa za noti nazo hamna

Miongoni mwa sababu zilizochangia haya ni uuzwa wa chenchi unafanyika hasa sehemu za stendi. Biashara ya namna hii ilipigwa marufu kipindi miaka michache nyuma lakini sasa imerudi tena. Ukifika stendi ndogo ya mbezi, utaona hili. Konda wa

Kingine ambacho kinachangia uadimikaji wa sarafu ni yale madubu ya kamali ya wa china. Mchezo huu huchezwa kwa kutumia mia mbili. Pesa hiyo ambao huangizwa ndani ya dubu hukaa mda mrefu mno kabla ya kutolewa, hii hufanya pesa hii isiwe kwenye mzunguko mda mrefu.

Wito wangu 'wenye mamlaka, hebu fanyeni hima kuangalia na kulidhbiti hii kadhia haraka iwezekavyo'
Mjmi sizijui rangi.Hivi zile sarafu za Tsh hamsini,mia na mia mbili(tukiacha mia tano)ni za rangi ya SILVA/SILVER
NB;Tukiachana na mambo ya "Silversands"@
 
Kichwa cha habari sarafu ya silva ,thread sarafu mchanganyiko, tuelewe kipi bwashee
 
Sio kwamba hizo shilingi zipo humo ndani n bajeti kwa ajili ya atakayeshinda? na ndio mzunguko wnyw huo
Au ndo hakuna kushinda 😂


Eh bc hao wachina n Choka mbaya sasa c 200 200 ndo wanajaza magunia kukaa nazo ndani 😂
Nimenya kazi na wachina anachokisema ni sahihi, kwenye kambi zao wamezifungia mia mbili nyingi ili ziweze kuendesha biashara yao ya bonanza!
Wanazoziweka kwenye mashine ni kiasi kidogo tu kwa ajili ya mzunguko kwa atakayeshinda... Lakini probability ya mchina kuliwa ni chache sana😂😂!
 
Dubwi kwasasa hawatumi hizo mia mbili, wamekuja na pesa zao ziko kama mia mbili lakini zao nyeupe
Bado wanatumia mia mbili karibia makampuni yote, kampuni mpya kama slots and keno, meteora na agamalotto ndo wamekuja na hizo coin za china kama backup plan endapo wakiishiwa mia mbili mashine iendelee kupiga kazi!
 
Haya madudu ilibidi yapigwe marufuku
Hayawezi kupigwa marufuku leo wala kesho, yanaingiza mapato makubwa alafu kuna wakubwa wa nchi wamewakingia mgongo hao wachina wanakula nao sahani moja!
 
Back
Top Bottom