Kwani Mkuu Sheria inasema Jaji hawezi kutenda Kosa au Jinai?
Au kuna mahali sheria za Nchi zinataja kuwa Jaji au Hakimu kamwe hatotenda kosa lolotw la jinai hata kama akiua au akiiba?
Kile kitu Mganga na hao wote walichofanya, walikifanya in the course of their duties, sio kama wao binafsi, DPP huwa hashitaki mtu kibinafsi, ni mwakilishi wa Jamhuri, pale anasimama sio kama yeye binafsi bali ni jamhuri, hivyo Madeleka alishtakiwa na jamhuri, hakushitakiwa na hao. na alishtakiwa baadaya huyo DPP kupelekewa jalada la ushahidi na wapelelezi. mbona hajawaweka wapelelezi? dpp huwa haamki tu na kushtaki mtu, basis yake ni ushahidi unaoletwa na wapelelezi.
pili, Jaji ana immunity, hawezi kushtakiwa kwa mambo aliyoyafanya kama Jaji katika kazi zake za kila siku.labda kwa mambo ya kibinafsi kama vile ameua mtu, amepiga mtu n.k. ila yale yote anayafanya akiwa Mahakamani, hata hakimu ana immunity, hawezi kushtakiwa. basi tuseme Mganga J hayo atakuwa aliyafanya akiwa bado hajawa Jaji, alikuwa DPP, lakini sasaivi ameshakuwa Jaji, hata kwenda kumwona pale unahitaji appointment, huwezi kumshtaki jaji hadi tume ya kumchunguza iundwe na imshauri aliyemteua kutengua ujaji wake ili awe raia wa kawaida. ila akiwa jaji huwezi kumshtaki, lazima umvue kwanza ujaji wake. sasa madeleka anaamini anaweza kumvua Mganga J ujaji wake kwa kufungua mashtaka ambayo Mganga aliletewa jalada la upelelezi na wapelelezi, na akiwa Mahakamani Madeleka mwenyewe akaandika barua kuiomba Mahakama kwamba anataka kuongea na DPP akiri kosa kwa plea bargaining, akaandika barua, akatia saini kwenye plea bargaining agreement, akalipa pesa na kutoka. NI rais gani ataunda tume kuchunguza Jaji katika mazingira ambayo madeleka mwenyewe alikiri kosa Mahakamani?
plea bargaining ni sawa na kukiri kosa, sasa mtu unakiri alafu uje kesho useme ulishtakiwa kimakosa? kweli?
huyu dogo tulishamwambia, anatakiwa kukaa chini ya uangalizi wa watu kama kina Tundu Lisu au Kibatala, hao wangemsaidia. hivi unafikiri T
undu Lisu hajui hayo yote? kwanini yeye
au kibatala hawajafungua mashtaka kama hayo? wanajua ni upuuzi, unajidharaulisha na unadharaulisha tasnia ya sheria. inatakiwa hata ukiwa Mahakamani watu waseme kweli huyu kaleta kitu cha maana, sio kuleta upupu ambao ni sawa na wa watu ambao hawajasoma sheria.