Peter Madeleka awaburuta Mahakamani Jaji Biswalo Mganga na Kamishina wa uhamiaji Anna Makakala

Peter Madeleka awaburuta Mahakamani Jaji Biswalo Mganga na Kamishina wa uhamiaji Anna Makakala

Madeleka ni mtafuta kiki tu huko twitter hana lolote
 
Hii imekaa kaa kama 'abuse of process of law'

eniweyi, kama wabobezi wanavyodai humu... inaonekana kama matumizi mabaya ya mahakama, kutafuta kiki.

ngoja tuone
 
Madeleka kuna uwezekano mkubwa ana shida ya afya ya akili. msaidieni mlio karibu naye. kwahiyo anategemea kumshitaki mh Jaji mbele ya Hakimu? na kesi yake hiyo si nilisikia kwamba alikiri yeye mwenyewe kwa plea bargaining?
yaani hata kama wakiifuta baadaye, ila tayari tushajua kumbe Buswalo anashitakika as a person tena mbele ya Hakimu.
Sheria siyo siasa, akajibu tuhuma zake.
 
Kupitia ukurasa wake rasmi wa X (Twitter) Peter Madeleka anaandika

HAWAKO juu ya SHERIA na wala HAWANA KINGA ya kutoshitakiwa KIJINAI. Naishukuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa KUIPOKEA kesi hii kwa ADMISSION No. AD/RM/ARS/91511/2023
View attachment 2840791
Hii hati Ina makosa tayari. Wakili Msomi madeleka, punguza jazba, unakuwa na haraka sana ya kukimbilia Mitandaoni. I Frame upya. Wataipiga chini.
 
Madeleka kuna uwezekano mkubwa ana shida ya afya ya akili. msaidieni mlio karibu naye. kwahiyo anategemea kumshitaki mh Jaji mbele ya Hakimu? na kesi yake hiyo si nilisikia kwamba alikiri yeye mwenyewe kwa plea bargaining?
sawa tofaut ya judge na hakimu mi sijajua ni ipi?
lakini pia nataka kujua ugumu wa kumshataki uko wapi???
 
Ngoja nikusaidie kitu manake upo gizani wala siwezi kukutukana kama wewe ulivyotukana. Madeleka ameshitakiwa Mahakamani, ameandika barua kwenda kwa DPP kuomba kukiri kosa ili alipe hizo 2m, DPP amekubali, madeleka anakiri kosa then analipa hizo pesa na anatoka nje. anakaa halafu anakuja kufungua kesi dhidi ya DPP aliyekuwa anafanya kazi kwa niaba ya Jamhuri, na anamshitaki in person, kwa kipi? wakati yeye mwenyewe alikiri kosa na kutia saini kwamba ni kweli alikosea? hapo kuna kesi kweli? tumemshauri sana lakini haelewi ila anataka kupata kiki kwa watu kama wewe. unajua kitu kinaitwa plea bargaining? au wewe ndio wale taborarasa fulani wa mtaani huko.
Madeleka anataka kucheza mchezo wa wale watuhumiwa wanao hojiwa police wanakiri makosa yao kwenye statements zao alafu eti wakifikishwa Mahakamani wanakana maelezo yao na kudai eti walilazimishwa kukiri makosa yao! Huo ni utoto!!
 
sawa tofaut ya judge na hakimu mi sijajua ni ipi?
lakini pia nataka kujua ugumu wa kumshataki uko wapi???
kama hujui hata utofauti wa Jaji na Hakimu, basi kaa pembeni uwe ndugu mtazamaji ujifunze kwa wanaojadili hapa. ni sawa na kusema hujui utofauti kati ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya.
 
yaani hata kama wakiifuta baadaye, ila tayari tushajua kumbe Buswalo anashitakika as a person tena mbele ya Hakimu.
Sheria siyo siasa, akajibu tuhuma zake.
kwahiyo na wewe unasema anashitakika kwa jambo ambalo hakulichunguza yeye, yeye aliletewa tu jalada, na walipopeleka mahakamani madeleka alikiri kosa na kusaini mbele ya Mahakama? unaelewa lakini?
 
Kwanini wewe uko upande wa wapotezaji?
Hapana japo kuna wakati usiogope kusema ukweli kwa kuamini ukisema utaonekanaje kwa jamii..
This guy's step Zinafichua vitu vingi na kuanika sheria wazi (Its obvious because alikuwa polisi ASP) Kwahyo anajua michezo hiyo..

So narudia tena Mara nyingi kwa Nchi yetu watu kama hawa hawanaga historia nzuri za maisha yao ya mbele
 
kama hujui hata utofauti wa Jaji na Hakimu, basi kaa pembeni uwe ndugu mtazamaji ujifunze kwa wanaojadili hapa. ni sawa na kusema hujui utofauti kati ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya.
Usimfukuze mtu JF mwenye nia nzuri ya kujifunza, ameuliza kwa nia njema akiwa amedhamiria kuijua maana, hivyo mpe jibu sahihi ili aendelee kujiona mwanachama wa JF.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Madeleka kuna uwezekano mkubwa ana shida ya afya ya akili. msaidieni mlio karibu naye. kwahiyo anategemea kumshitaki mh Jaji mbele ya Hakimu? na kesi yake hiyo si nilisikia kwamba alikiri yeye mwenyewe kwa plea bargaining?
Halafu utakuta na wewe ni graduate ...... Ni wonder hampati ajira. Mmebaki kuendekeza UCHAWA!!
 
ameshaandika barua kwa Mh. Rais kwamba amsimamishe Mganga J ili kupisha tuhuma. Hoja ni je? anazo sababu za msingi kumfanya Rais amsimamishe Mganga? mtu yeyote na kwa jambo lolote anaweza kuamka tu na kumtaka Rais amsimamishe Jaji kwa sababu yeyote ile ambayo yeye kwa akili yake anaamini ni ya msingi?

Madeleka alituhumiwa, upelelezi ukafanyika,jalada likapelekwa kwa DPP, DPP akaangalia upelelezi jaladani akaona kuna kesi ya msingi, akampeleka Mahakamani based on that evidence, wakati kesi haijaanza kusikilizwa Madeleka ameandika barua kwa DPP na kuitaarifu Mahakama kwamba anaomba kukiri kosa kwa makubaliano, amekubaliwa, amekiri kosa mbele ya Mahakama, na Mahakama imempa adhabu kwa mujibu wa makubaliano. Halafu leo anamtaka Rais amsimamishe Jaji, hiyo ni sababu ya msingi kumfanya Rais kumsimamisha Mh. Jaji? Mwanasheria mwenye akili na makini hawezi kuforesee na kuona hapo ameshusha hadhi ya wanasheria, anaonekana ni mtu aliyesoma sociology tu? worse enough, mlioko huko mtuambie, malalamiko yake yamesharuhusiwa na Mahakama, au Mahakama imeshayapima na kuona ya msingi au la?
 
Yule mama anabebwa na jenda tu hawezi tumbuliwa kisa ni mwanamke lakini performance zero
 
Yule mama anabebwa na jenda tu hawezi tumbuliwa kisa ni mwanamke lakini performance zero
mama ana kosa gani, na DPP ana kosa gani, wakati mtuhumiwa (madeleka) amekiri kosa kabla ushahidi waliosema wanao haujaletwa?
 
Back
Top Bottom