Peter Mollel (Pierre Liquid) amesilimu sasa anaitwa Salum Sheikh Kishk

Ni jambo la kheri ila kwa jinsi Pierre alivyo nachelea kuamini.
Tazama video clip.

Pierre ni mtu mwenye upendo wa hali ya juu, ndiyo maana akakubalika sana na mapungufu yake.

Na mwenye upendo wa dhati kwa watu huwa na imani ya hali ya juu.
 
Hapo ndipo unaona tofauti kati ya Uislamu na Ukristu. Wakristu wanasoma habari hii na kuichukulia "kawaida" tu. Mtu ameamua kivyake. Hakuna wa kumsumbua wala kumfanya cho chote. Lakini angekuwa Muislamu atangaze hivyo, kifo kingekuwa kinamhusu. Ndugu zake wangemkataa na Muislamu yo yote angekuwa na kibali kutoka kwenye dini hiyo kumuua. Ndiyo maana Waislamu wanaoingia Ukristu hubidi kuhama nchi kabisa kwenda kuishi kwingine kabisa ambapo kutakuwa na usalama.
 
Alivyo na kiu ya bia, yuko tayari hata kukana wazazi wake kwa ajili ya fedha. Umaskini kitu kibaya sana
 
Tazama vidwo clip.

Pierre ni mtu mwenye upendo wa hali ya juu, ndiyo maana akakubalika sana na mapungufu yake.

Na mwenye upendo wa dhati kwa watu huwa na imani ya hali ya juu.
Hujanielewa, video nimeitazama ila namaanisha nachelea kuamini kama atabaki katika Uislam na sio maigizo ya kutaka kuongelewa.
 
Sina uhakika baada ya kusilimu huyo Peirre Liquid ataacha pombe.

Wiki tatu zilizopita nilikutana naye hapo Uhasibu Mbagala akipiga zake beer kwenye hiyo pub maarufu ya Liquid Pub.

Mola amsaidie ailinde na kuitetetea imani yake, maana safari ya Pepo siyo rahisi kama tunavyofikiri
 
Hujanielewa, video nimeitazama ila namaanisha nachelea kuamini kama atabaki katika Uislam na sio maigizo ya kutaka kuongelewa.
Sijawahi kukutana nao wa namna hiyo.

Kama ni umaarufu Pierre ni maarufu.
 
Hoja ya ndugu kuleta noma kwasababu mtu kabadili dini, huwa ni pande zote mkuu
 
Tatizo hauuelewi Uislam wala huelewi dini ni nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…