Peter Msechu adai kupungua kilo 7 baada kuwekewa puto Tumboni

Peter Msechu adai kupungua kilo 7 baada kuwekewa puto Tumboni

Hiyo Kasi ya upunguaji ni kubwa Sana....Dr Janabi alisema ukiwekewa puto unakuwa unakula kidogo unajisikia umeshiba ...Sasa huu ulaji mdogo ndio usababishe upunguaji uwe mkubwa ivi....watu wanaofanya mazoezi wanaelewa kitu kimoja unapoburn calories 7,700 ktk mwili wako ndio unakuwa umepungua kg 1...na hiyo kg 1 ni sawa na ukimbie marathon 3 Kwa siku yaani km 128...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hahahah mwacheni Puto Msechu apungue jamani ameteseka sana.
 
Msanii Peter Msechu amefanikiwa kupunguza uzito wa kilo saba ndani ya siku saba tangu alipowekewa puto na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila ili kumsaidia kupunguza uzito.

Msechu aliwekewa puto hilo Januari 25, 2023 akiwa na uzito wa kilo 143.4 lakini kufikia leo Februari Mosi 2023, ana uzito wa kilo 136.5, wastani wa punguzo la uzito la kilo moja kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa leo kwenye ukurasa wa Instagram wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila, imethibitisha kwamba msanii huyo wa Bongo Flava amepunguza uzito huo ndani ya muda mfupi.

“Msanii Peter Msechu amepungua kilo saba, toka afanyiwe huduma tiba ya kuwekewa puto (intragastric balloon) kwenye tumbo la chakula ili kumsaidia kupungua. Huduma hiyo alifanyiwa Januari 25, 2023, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila,” inaeleza taarifa hiyo.

Msechu pia ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuonyesha kwamba amepunguza uzito huo huku wakiwashukuru madaktari wa Hospitali ya Muhimbili Mloganzila kwa kufanikisha azma yake ndani ya muda mfupi.

“Eeeh Mwenyezi Mungu sijui nikushukuru vipi, niliwekewa puto Januari 25, 2023, picha hiyo nilipiga asubuhi wakati naenda hospitali asubuhi. Leo ni siku ya saba baada ya kumeza puto Februari Mosi, 2023 nimepiga picha hiyo muda ule ule wa asubuhi kama wakati naenda hospitali. Nimepunguza kilo saba kwa siku saba, ina maana kila siku kilo moja inazikwa. Muhimbili hii mmetishaa.

MWANANCHI

“Kipekee kabisa asanteni sana wataalamu wote na madakatari kutoka Hospital ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila, haki ya nani mmebadilisha maisha yangu tayari ndani ya wiki moja tu. Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili Profesa Janabi kongole sana,” ameandika Msechu.
Kupungua kilo 7 katika 143 bado sana. Hivi binadamu unafikishaje uzito huo? Uzembe kupindukia.
 
Hiyo Kasi ya upunguaji ni kubwa Sana....Dr Janabi alisema ukiwekewa puto unakuwa unakula kidogo unajisikia umeshiba ...Sasa huu ulaji mdogo ndio usababishe upunguaji uwe mkubwa ivi....watu wanaofanya mazoezi wanaelewa kitu kimoja unapoburn calories 7,700 ktk mwili wako ndio unakuwa umepungua kg 1...na hiyo kg 1 ni sawa na ukimbie marathon 3 Kwa siku yaani km 128...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Si ndio mwili unajimeng'enya maana unajua hakuna virutubisho vipya, maana ukinywa tu maji umeshiba, mara hausikii njaa kabisa, wakati mwili unahitaji chakula hivyo mwili unaanza kujipunguza kutumia virutubisho vilivyopo mwilini
 
Nawaza atakuwa analinganaje akija kumaliza siku 120 ( miezi 4)? Maana kupungua kilo moja kwa siku sio mchezo
 
Na ndugu yangu alifanya hio ndani ya mwezi akaanza kuwa kama HIV stage 4 🤣🤣🤣 na alikuwa na mwili umenawiri balaa.
Sawa mkuu, najitajidi huu mwezi niweze..
 
Medical Drs kwa local content siwaamini, most likely life expectancy yake itakuwa 10-15 years just my assumption based on typical errors of of our locally trained Drs, 70% guess work and learning through fatal mistakes kwenye miili yetu, huruma na roho wa Mungu hafifu sana
 
Back
Top Bottom