Peter Msechu afanyiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni

Peter Msechu afanyiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni

Hilo puto linaingizwa likiwa tupu kupitia njia ya chakula linapelekwa Hadi tumbo la chakula, likifika huko linajazwa upepo, kwa hiyo kasehemu ka chakula kanabaki kadogo, sehemu kubwa unakuwa umechukuliwa na Hilo puto. Kwa hivyo mhusika anakuwa akila tu kiduchu anajiona kavimbiwa. So automatically mtu atapungua.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Samahani Dokta mbona huku mtaani wanasema linaingizwa kwa njia ya haja kubwa?
 
Hilo puto linaingizwa likiwa tupu kupitia njia ya chakula linapelekwa Hadi tumbo la chakula, likifika huko linajazwa upepo, kwa hiyo kasehemu ka chakula kanabaki kadogo, sehemu kubwa unakuwa umechukuliwa na Hilo puto. Kwa hivyo mhusika anakuwa akila tu kiduchu anajiona kavimbiwa. So automatically mtu atapungua.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Yeye anataka umwambie linapitia makalioni.
 
View attachment 2495348

Peter Msechu amefanyiwa matibabu ya kuweka puto tumboni ili kupunguza uzito na unene inayoendelea kutolewa katika hospitali ya Mloganzila.
Peter Msechu amefunguka machache kuhusiana na changamoto ya kuwa na uzito wa kupitia kiasi kama ifuatavyo

"Watu wananisema sana mtandaoni kuwa Mimi ni mnene na siwajibu. Mimi niliamua kuishi maisha yangu. Lakini nimekuwa kila siku nikitafuta tiba mbadala ya kuondoa unene. Natamani Sana kupungua. Sijawahi kujua kushiba kukoje. Nimekuja hapa Mloganzila ili nifanyiwe hili zoezi la kuwekewa puto tumboni ili nipungue na nitafanyiwa leo na watu wataona" amesema Peter Msechu.

"Nafanya kazi sana na Serikali na ninaposafiri huwa naendesha gari mwenyewe kuna wakati mwingine nakuwa kwenye mazingira magumu, nisafiri nifanye kazi, niimbe halafu nisafiri tena nirudi Dar. Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima nirudi Dar.

"Juzi nilisafiri kwenda Mbeya nilipomaliza kazi nilirudi Dar. Hii nayo ni changamoto ya unene, unakuwa mtu wa kuchagua sana. Na wakati mwingine nahofia kuvunja vitanda vya a hotel kwa sababu nilishavunja Sana, hasa hizi chaga. Inanibidi niombe radhi pale reception"

"Watu wanene wapo na wanajigundua Wana changamoto ambazo wanapitia na zipo nyingi. Ukiwa na uzito mkubwa kuna baadhi ya vitu unashindwa kufanya mwenyewe. Nimeshaingia hasara ninaweza kuwa pale nyumbani nafanya kazi zangu kwenye kompyuta nikaona kwenye bustani yangu nataka nikakate majani niko radhi nitoe Elfu 20 nimwite kijana akate majani kitu ambacho ningekata mwenyewe kwa dakika Tatu. Ukipiga hesabu hizo na vitu ambavyo nimepoteza tayari nimeshaingia hasara" amefunguka Peter Msechu.
Hilo PUTO linaingizwaje tumboni...?
 
Naona feedback imeanza
Screenshot_20230203-081214_1.jpg
 
Jana TU asbh saa 4 nilimtembelea rafk yangu bonge flani ofsn kwake, tulkua na kikao flani.

nilishangaa jamaa anapiga chapati 4 na maziwa nusu Lita. Kapiga yote mpk kamaliza.

Mi nilikunywa kikombe robo na chapat moja nikatosheka

Saa 7 tu analalamika njaa inauma,
Kapiga Simu nyumbn anafoka wawaishe ugali,Wakati Mimi bado nahs nmeshiba[emoji1787]
Watu wengi wanene ukifuatilia wanapenda sana kula...
 
Na hyo procedure ya maputo ni sh ngapi?? Maana kuna shoga angu juzi nikamwambia hongera naona karibia unajifungua sijaonana nae kitambo kidogo amenuna mpk leo...nikajaambiwa ni tumbo lake
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom