Peter Msechu afanyiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni

Peter Msechu afanyiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni

Sio Kila Mtu anafaa kuwekewa Puto. Puto inategemea na BMI. Madaktari Tanzania Ndio Maana Wanaua Wagonjwa. Mtu wa Kg 144 unamuwekeaje Puto? Akipungua Sana Kg 20/16. Hii Publicity itakuja Kumcost…. Uzuri Jamii Forum Ipo.

Tukutane Mwakani Tarehe kama Ya Leo.

PM alifaa kufanyiwa Bariatric Surgery. Ambapo angebaki na Kg 72 which Ni Sawa kwake.

Nashangaa Serikali Kuacha Kuendelea kuenea kwa Matangazo ya Balloon wakati madhara yake ni Makubwa. Ballon Inafaa kwa Mtu chini ya Kg 90 sio zaidi ya 100

Mwisho. Kupungua unahitaji ku change life style Completely. Hata Kufanyiwa Bariatric Surgery, Kifupi ni Kumaanisha Unabadirisha Mfumo wa Maisha kuanzia kuacha pombe, namna ya kula na kila kitu ndio maana Psychologist huhusika, Psychiatrics huhusika, Dietician huhusika, Daktari wa Mazoezi, Endocrinologist, General Surgeon na Wengine.

Fuatilia Duniani, Madaktari nguli wamekataa matumizi ya Balloon.
Aseee....
 
Hilo puto linaingizwa likiwa tupu kupitia njia ya chakula linapelekwa Hadi tumbo la chakula, likifika huko linajazwa upepo, kwa hiyo kasehemu ka chakula kanabaki kadogo, sehemu kubwa unakuwa umechukuliwa na Hilo puto. Kwa hivyo mhusika anakuwa akila tu kiduchu anajiona kavimbiwa. So automatically mtu atapungua.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Nawaza in long run..hiyo sehemu ambayo puto imeikava haiwezi kudevelop kama ukungu hivi kupelekea some complications..ikiwemo cancer...
 
View attachment 2495348

Peter Msechu amefanyiwa matibabu ya kuweka puto tumboni ili kupunguza uzito na unene inayoendelea kutolewa katika hospitali ya Mloganzila.
Peter Msechu amefunguka machache kuhusiana na changamoto ya kuwa na uzito wa kupitia kiasi kama ifuatavyo

"Watu wananisema sana mtandaoni kuwa Mimi ni mnene na siwajibu. Mimi niliamua kuishi maisha yangu. Lakini nimekuwa kila siku nikitafuta tiba mbadala ya kuondoa unene. Natamani Sana kupungua. Sijawahi kujua kushiba kukoje. Nimekuja hapa Mloganzila ili nifanyiwe hili zoezi la kuwekewa puto tumboni ili nipungue na nitafanyiwa leo na watu wataona" amesema Peter Msechu.

"Nafanya kazi sana na Serikali na ninaposafiri huwa naendesha gari mwenyewe kuna wakati mwingine nakuwa kwenye mazingira magumu, nisafiri nifanye kazi, niimbe halafu nisafiri tena nirudi Dar. Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima nirudi Dar.

"Juzi nilisafiri kwenda Mbeya nilipomaliza kazi nilirudi Dar. Hii nayo ni changamoto ya unene, unakuwa mtu wa kuchagua sana. Na wakati mwingine nahofia kuvunja vitanda vya a hotel kwa sababu nilishavunja Sana, hasa hizi chaga. Inanibidi niombe radhi pale reception"

"Watu wanene wapo na wanajigundua Wana changamoto ambazo wanapitia na zipo nyingi. Ukiwa na uzito mkubwa kuna baadhi ya vitu unashindwa kufanya mwenyewe. Nimeshaingia hasara ninaweza kuwa pale nyumbani nafanya kazi zangu kwenye kompyuta nikaona kwenye bustani yangu nataka nikakate majani niko radhi nitoe Elfu 20 nimwite kijana akate majani kitu ambacho ningekata mwenyewe kwa dakika Tatu. Ukipiga hesabu hizo na vitu ambavyo nimepoteza tayari nimeshaingia hasara" amefunguka Peter Msechu.
Hilo puto wameliingiizia wapi?
 
Haya matatizo yasikie kwa watu wengine. Nina dada alikuwa anakunuw maji na chakula kidogo sana na mda mwingine anafunga sana ila alikuwa ananenepa tu. Mda mwingine usione mtu mnene ukajua anakula sana. .
Asilimia kubwa ya wabongo tunaamini kula sana ndio kunenepa, kuna jamaa pia namfaham aisee anakula si mchezo, naposema anakula jua anakula kweli kweli, ila mwili wake ukiuona huwezi amini
 
Hakuna kitu kinachochomfurahisha mtu mnene kama kumuona mtu mnene zaidi kumzidi yeye!!
Utasikia hebu jitahidi mazoezi kidogo , [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahaaa, hio nishawahi mshuhudia boss wangu anamcheka jamaa mmoja tulikutana naye sehemu mnene sana bahati mbaya ni mfupi!
Jamaa alicheka sana, wakati hata sie huwa tunamahangaa tumbo lilivyozidi [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Sio balozi wa maputo ya kuwekewa huyu🤔?Kama kweli sawa maana hawachelewi hawa kesho atatusuta hapa utasikia :"new deal new dollar mlinicheka mwenyewe im makin monii"
Balozi wa kuwekewa maputo mloganzira
 
Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima nirudi Dar.
Hotel za aina gani hizo chafu?

Atakuwa analala guest za 10 hadi 20 ndio maana anaogopa. Akalale kuanzia 60 hadi 300,000 mbona ni zaidi hata ya kule anakokimbilia kulala nyumbani kwake.

Aache kulala uchochoroni
 
Hahahaaa, hio nishawahi mshuhudia boss wangu anamcheka jamaa mmoja tulikutana naye sehemu mnene sana bahati mbaya ni mfupi!
Jamaa alicheka sana, wakati hata sie huwa tunamahangaa tumbo lilivyozidi [emoji1][emoji1][emoji1]
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom