Peter Msechu afanyiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni

IMG_1174.jpg

IMG_1173.jpg

Huo ndio ulikua mwili wake na ule mwili wake wa kipindi hiki sio wake
 
Huyu jamaa alikuaga na mwili wa kawaida ghafla kaanza kufumuka na alikuwa anafanya masihara kuhusu hili suala
Uwekaji wa puto usije ukaleta mambo mengine tu

Hua nashangaa watu hapa wanasema mtu anakula kidogo lakini anananenepa wanashindwa kuelewa mwili ukiuendekeza ukafumuka kuja kurudi kwenye hali yako ya kawaida ni kazi maana inahisisha hadi homoni mbalimbali mwilini, hivo lazima tuwe na displine na mifumo yetu ya maisha, mtu akishakua kibonge anakimbilia gym ambapo huko anaongeza hamu ya kula kwa kasi asipojicontrol hapo amekwenda tayari,
 
Msechu na Lissu wamefanana wenyewe, kama mtu na mdogo wake.
Kuna ndugu yetu aliwekewa puto akapungua, mkewe mzungu hakupenda alivyoongezeka baada ya ndoa. Sijui ikawaje tena alikuja kunenepa akawa puto halisi.
 
Tena unaambiwa ukitaka kuharibu mwili weka hilo puto wamuulize yule kitale wa EFM alifanya nini kupungua
 
View attachment 2495348

Peter Msechu amefanyiwa matibabu ya kuweka puto tumboni ili kupunguza uzito na unene inayoendelea kutolewa katika hospitali ya Mloganzila.
Peter Msechu amefunguka machache kuhusiana na changamoto ya kuwa na uzito wa kupitia kiasi kama ifuatavyo

"Watu wananisema sana mtandaoni kuwa Mimi ni mnene na siwajibu. Mimi niliamua kuishi maisha yangu. Lakini nimekuwa kila siku nikitafuta tiba mbadala ya kuondoa unene. Natamani Sana kupungua. Sijawahi kujua kushiba kukoje. Nimekuja hapa Mloganzila ili nifanyiwe hili zoezi la kuwekewa puto tumboni ili nipungue na nitafanyiwa leo na watu wataona" amesema Peter Msechu.

"Nafanya kazi sana na Serikali na ninaposafiri huwa naendesha gari mwenyewe kuna wakati mwingine nakuwa kwenye mazingira magumu, nisafiri nifanye kazi, niimbe halafu nisafiri tena nirudi Dar. Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima nirudi Dar.

"Juzi nilisafiri kwenda Mbeya nilipomaliza kazi nilirudi Dar. Hii nayo ni changamoto ya unene, unakuwa mtu wa kuchagua sana. Na wakati mwingine nahofia kuvunja vitanda vya a hotel kwa sababu nilishavunja Sana, hasa hizi chaga. Inanibidi niombe radhi pale reception"

"Watu wanene wapo na wanajigundua Wana changamoto ambazo wanapitia na zipo nyingi. Ukiwa na uzito mkubwa kuna baadhi ya vitu unashindwa kufanya mwenyewe. Nimeshaingia hasara ninaweza kuwa pale nyumbani nafanya kazi zangu kwenye kompyuta nikaona kwenye bustani yangu nataka nikakate majani niko radhi nitoe Elfu 20 nimwite kijana akate majani kitu ambacho ningekata mwenyewe kwa dakika Tatu. Ukipiga hesabu hizo na vitu ambavyo nimepoteza tayari nimeshaingia hasara" amefunguka Peter Msechu.
Ndiyo kwanza bado tupo January lakini Diamond platnumz tayari ameshatoa video bora ya mwaka 2024, kitu gani umekipenda kutoka kwenye hii video ya "yatapita".?
 
Miaka 3 ana 4 huko nyuma msechu alikua anajisifia kwamba anamaliza sahani 3 za wali maharage peke yake na anapenda sana kula na asizuiwe kula.

Leo anasema hata asipokula hapungui.

Aliona sifa kula. Sasa acha yampate.
 
View attachment 2495348

Peter Msechu amefanyiwa matibabu ya kuweka puto tumboni ili kupunguza uzito na unene inayoendelea kutolewa katika hospitali ya Mloganzila.
Peter Msechu amefunguka machache kuhusiana na changamoto ya kuwa na uzito wa kupitia kiasi kama ifuatavyo

"Watu wananisema sana mtandaoni kuwa Mimi ni mnene na siwajibu. Mimi niliamua kuishi maisha yangu. Lakini nimekuwa kila siku nikitafuta tiba mbadala ya kuondoa unene. Natamani Sana kupungua. Sijawahi kujua kushiba kukoje. Nimekuja hapa Mloganzila ili nifanyiwe hili zoezi la kuwekewa puto tumboni ili nipungue na nitafanyiwa leo na watu wataona" amesema Peter Msechu.

"Nafanya kazi sana na Serikali na ninaposafiri huwa naendesha gari mwenyewe kuna wakati mwingine nakuwa kwenye mazingira magumu, nisafiri nifanye kazi, niimbe halafu nisafiri tena nirudi Dar. Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima nirudi Dar.

"Juzi nilisafiri kwenda Mbeya nilipomaliza kazi nilirudi Dar. Hii nayo ni changamoto ya unene, unakuwa mtu wa kuchagua sana. Na wakati mwingine nahofia kuvunja vitanda vya a hotel kwa sababu nilishavunja Sana, hasa hizi chaga. Inanibidi niombe radhi pale reception"

"Watu wanene wapo na wanajigundua Wana changamoto ambazo wanapitia na zipo nyingi. Ukiwa na uzito mkubwa kuna baadhi ya vitu unashindwa kufanya mwenyewe. Nimeshaingia hasara ninaweza kuwa pale nyumbani nafanya kazi zangu kwenye kompyuta nikaona kwenye bustani yangu nataka nikakate majani niko radhi nitoe Elfu 20 nimwite kijana akate majani kitu ambacho ningekata mwenyewe kwa dakika Tatu. Ukipiga hesabu hizo na vitu ambavyo nimepoteza tayari nimeshaingia hasara" amefunguka Peter Msechu.
Hivi na unene ule maliwatoni anawezaje kushusha mzigo na kupangusa spika?

Unene changamoto sana😂
 
Back
Top Bottom