Uchaguzi 2020 Peter Msigwa awasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania

Inaonyesha namna gani kwenye chama cha Chadema, demokrasia ilivyokomaa........

Kule kwenye chama cha kijani, ukisikika tu una mpango wa kuchukua fomu na kutaka kumpinga Jiwe, unafukuzwa toka kwenye Chama!
Kweli nyani haoni kundule, Wangwe, Zitto, Mwambie, Sumaye Hawa wote walichukua form kumpinga Mbowe. Wako wapi leo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msigwa haaminiki?
 
Leo Peter Msigwa amekuwa kiumbe asieaminika?!

Maisha yanaenda kasi sana.
Sio ahaminiki tu, pia mjinga, amezoe kuwadanganya waumini wake, na amechukua hiyo hadi kuwazushia watu mabalaa, ni mpuuzi!
 
chadema kuna tatizo mtu kugombea anaandika barua? kawaida inatakiwa achukue fomu ya kuomba kugombea aijaze na kuirudisha hili lichama la chadema mbona limekaa kienyeji sana
 
chadema kuna tatizo mtu kugombea anaandika barua? kawaida inatakiwa achukue fomu ya kuomba kugombea aijaze na kuirudisha hili lichama la chadema mbona limekaa kienyeji sana
Kwani wewe unapangiwa utaratibu wa kuishi nyumbani kwako? Kila nyumba Ina taratibu zake.
 
Msigwa naye anataka urais??!!! Duh! Hatari sana. Narudia kusema huu mchakato wa kuwania urais kupitia Chadema ndio kaburi la Chadema. Chadema sasa inakufa kifo cha mende.
 
chadema kuna tatizo mtu kugombea anaandika barua? kawaida inatakiwa achukue fomu ya kuomba kugombea aijaze na kuirudisha hili lichama la chadema mbona limekaa kienyeji sana
Ni mtindo tu usihofu, na ni mzuri, ungetumika kwenye serikali za mitaa tusingepata viongozi wa vitongoji wasiojuwa kusoma na kuandika kama walivyo leo wengi, kwetu ni kibao na wamefanikiwa kwa kuwa walipita kwa wengine kuenguliwa sababu walitumia anuani ya mkurugenzi!
 
Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa leo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania
ni haki yake kuboresha cv kabla ya kutoka duniani
 
Ni haki yake kikatiba, sio Kule ccm kuchukua fomu ya urais Ni marufuku.chama kitaamua nani anafaa.nawapongeza chadema kwa kweli
 
chadema kuna tatizo mtu kugombea anaandika barua? kawaida inatakiwa achukue fomu ya kuomba kugombea aijaze na kuirudisha hili lichama la chadema mbona limekaa kienyeji sana
Kila chama kina taratibu zake usikariri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…