Uchaguzi 2020 Peter Msigwa awasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Peter Msigwa awasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania

Anatumia nguvu nyingi huku mizizi ya shingo ikimtoka kutuaminisha kitu huku akijua kuwa ni uongo . Sijui anatuchukuliaje
Ni haki ya kila Mwanachadema kuomba kuteuliwa. Mbona CCM mwaka 2015 walijitokeza kama 30?! Kama kungekuwa na demokrasia ndani ya CCM wangejitokeza wengi tu. Lakini wanaogopa kwa yatakayowapata, maana wanaweza kupotea hivi hivi!
 
Msigwa naye anataka urais??!!! Duh! Hatari sana. Narudia kusema huu mchakato wa kuwania urais kupitia Chadema ndio kaburi la Chadema. Chadema sasa inakufa kifo cha mende.
Mara mia chadema kuliko ccm, urais kugombea mwiko kwa wanachama isipokuwa jiwe
 
Hatuwezi kukubali kamwe, Taifa letu, moja, pendwa kuongozwa na mtu Mwongo, mzushi na mnafiki. Kama aliweza kumzushia mzee Kinana Mambo ya ajabu, itakuwaje akiwa na dola?
Baada ya kukiri kwa kinywa chake mwenyewe kuwa alimzushia uongo Kinana , Msigwa hafai kuwa hata Mwenyekiti wa tawi wa chama.
 
Ni haki yake ila mwisho wa siku atakuja kujitoa na kusema anamuunga mkono Lissu.Hata Nyalandu nae atakuja kujitoa na kumuachia Lissu hiyo nafasi.Huu ni mkakati wa kisiasa wa kumpa Lissu nguvu zaidi katika uchaguzi huu japo hatuna Tume Huru.

Kama anataka kutafuta sababu ya kuondoka CHADEMA kupitia mchakato wa uteuzi, muda utasema.
Mkuu mbona unashindwa kujiamini au kuwaamini wanachadema wenzako kwa hiyo tuseme huna Imani na Msigwa?

Ama Kweli kwa maneno yako basi Chadema inasikitisha kwann unamuamini Lisu tu, na hawa wengine hawaaminiki? Yani wanachadema wenyewe hawaaminiani duuh kazi ipo

pujo
 
Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa leo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania,

---
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjinikupitia chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Peter Msigwa pamoja na Muheshimiwa Tundu Lissu wametangazwa kuwasilisha barua ya kutia niaya kuwania Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanial

Kwa nyakati tofauti wamewasilisha barua hizo kwa katibu mkuu wa chama hicho ambapo Lissu anadaiwa kuongea na Watanzania muda wowote.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa na Mjumbe wa CC ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Peter Msigwa amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, ya kutia nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hizo ni hesabu ndefu kama ulikuwa sifuri darasani huwezi kukokotoa hii huyo ni mchezaji wa akiba ikiwa lissu atapewa red card
 
Anatumia nguvu nyingi huku mizizi ya shingo ikimtoka kutuaminisha kitu huku akijua kuwa ni uongo . Sijui anatuchukuliaje
Atakuwa sio binadamu huyo,ana mizizi shingoni?
 
🤣🤣🤣 kituko cha nusu mwaka.

Ila kanusa Iringa mjini sio sehemu sahihi sana kwake
 
Attachments

  • y2mate.com - Mhe. Msigwa akifyatuka Juni 20, 2012_T3wgDb2PRAI_144p.mp4
    11.5 MB
Kwani jamaa ana fungu la kumkatia mwenye saccos yake??

Aaangalie tu yasije kumpata ya kumpata.
 
Ni haki yake ila mwisho wa siku atakuja kujitoa na kusema anamuunga mkono Lissu.Hata Nyalandu nae atakuja kujitoa na kumuachia Lissu hiyo nafasi.Huu ni mkakati wa kisiasa wa kumpa Lissu nguvu zaidi katika uchaguzi huu japo hatuna Tume Huru.

Kama anataka kutafuta sababu ya kuondoka CHADEMA kupitia mchakato wa uteuzi, muda utasema.
Afadhali huyo muda aje aseme tu maana najionea vitimbi tu!
 
Back
Top Bottom