Peter Msigwa: Baada ya kushinda kesi ya Mbowe, nini hatma ya mauaji ya Akwilina?

Peter Msigwa: Baada ya kushinda kesi ya Mbowe, nini hatma ya mauaji ya Akwilina?

Ila utawala wa jiwe ulikuwa una umuhimu mkubwa sana. Yaani alikuja na kuondoka ndani ya muda mfupi ili liwe funzo kwa Watanzania.
Shamba darasa, Mungu aliruhusu tujifunze
 
"Baada ya kushinda kesi ya Mh Freeman Mbowe na wenzake, mjadala sasa ni juu ya matumizi ya 350M, hatujadili uhai wa Akwilina. Nani alimuua? Nani anawajibika? Mkurugenzi wa Kinondoni anawajibikaje? Kwanini hakutoa barua za mawakala? Athari walizopata warufani. Uhuni huu utaisha lini?"

- Mch. Peter Msigwa

-
Hatma ya Aquilina itajadili mahakama na Mkurugenzi wa kinondoni Kajulumuguru
 
Sasa umuhimu wake ulikuwa upi?Hebu elezea.
Umuhimu wa jiwe;

1. Tumebaini udhaifu mkubwa, katika katiba yetu, ambayo inampa mamlaka makubwa rais, na rais akiyatumia basi inakuwa shida tu ndani ya nchi.

2. Tumewabaini Watanzania majasiri na waoga. Watanzania majasiri miongoni mwao ni Lisu!

3. Tumejifunza uthubutu. Jiwe alikuwa anathubutu ingawa uthubutu wake ulileta matokeo chanya au hasi katika jamii.

3. Tumejifunza wanasiasa wengine wa Tanzania ni njaa kali sana na wanafiki, wapo kwa maslahi yao na siyo kwa ajili ya wananchi. Hapa tunarejea wale waliounga mkono juhudi na wale wa kusifia ila kwa sasa wanapingana na jiwe.

4. Tumejifunza, kama nchi, planners of the state lazima wawe makini sana, ili waweze kuwachuja na kuleta viongozi makini katika nchi. Hapa hadi upinzani unatakiwa kuangaliwa wagombea wao, kwa sababu inaweza kutokea bahati nzuri wakachukua nchi pia. Mwingine anafaa kuwa mbunge, na si rais. Rejea, jiwe mwenyewe alisema alisukumizwa tu kwenye urais tu!

5. Tumejifunza kwamba, bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, kamwe wapinzani wasahau kuchukua hii nchi. Watakuwa wanashinda majimbo kutokana na huruma ya kiongozi aliyepo madarakani. Rejea engua engua ya wagombea wa upinzani. Hakuna hata mgombea mmoja wa CCM aliyeenguliwa.

6. Tumejifunza, kiongozi yoyote wa Afrika akitaka kupigania maslahi ya Afrika mwisho wake lazima uwe mbaya. Jiwe, aliingia kwenye ligi na wazungu katika kulinda rasilimali za nchi. Rejea kuzuia makinikia, lakini kwa sasa yanasafirishwa.

7. Tumejifunza pia, kama kiongozi wa nchi usipende kuwaamini sana wasaidizi wako, kiasi kwamba husikilizi malalamiko ya wananchi wanapowalalamikia viongozi hao. Rejea malalamiko ya wananchi kwa Sabaya.

Yapo mengi ya kujifunza, chanya na hasi
 
Msigwa Jengeni Ofisi hivi hamuoni aibu?? mnataka Dola hata ofisi hamna??
 
Wakuu bado sura ya mdogo wetu Akwilin Akwilina inanijia. Sijui kwanini jambo kubwa kama hili lilimalizwa kiaina katika dunia ya leo. Kulingana na mazingira ya kifo kuhusisha vyombo vya usalama ni wakati sasa wa kulifungua jarada la kesi ya Akwilin ili wahusika wawajibishwe.
 
Msigwa Jengeni Ofisi hivi hamuoni aibu?? mnataka Dola hata ofisi hamna??
Ccm ilijenga ofisi gani katika nchi hii, hivi wakitolewa madarakani si watakuwa kama Kanu, Unip na UPC.
 
Ikitokea nchi imeshikwa na wapinzani tusidai tens katiba itumike hii hii.
 
This is tricky.

Ila inapotokea kuna shoot out na stray bullet ikampata mpita njia askari hua hawahesabiwi kua na makosa.

Hii ni dunia nzima.

Badala yake waliosababisha shoot out ndiyo huhesabiwa wamesababisha kifo. Ishu inakuja kuprove kama kulikua na ulazima wa kushoot.

Binafsi sidhani kama hii kesi itarudi mahakamani ili kuwashtaki askari. Tunaambiwa kwamba serikali ilisimamia mazishi na kusomesha ndugu wa marehemu. Best thing ambacho ilitakiwa tujifunze ni kua na risasi za mpira kama mbadala na crowd control iwe ni lazima.

Kuna askari alijirekodi akisema yupo tayari kuua kila asiyetii sheria bila shuruti. Yuko wapi?
 
... ni lazima Akwilina atendewe haki! Binadamu tena asiye na hatia, mpita njia, hawezi kupigwa risasi na vyombo vya dola halafu ikapita hivi hivi! Waliotoa amri na waliofyatua risasi bado wangalipo hai; mtoto mzuri yule atendewe haki hata kama hatunaye tena.
Chadema walimponza binti wa watu eti nae alitaka aandikwe kuwa mwana harakati
 
Chadema walimponza binti wa watu eti nae alitaka aandikwe kuwa mwana harakati
... acha kashfa ... Akwilina aliuliwa akiwa ndani ya dalala tambua hilo. Kwa hiyo wote waliokuwemo ndani ya ile daladala walitaka watambuliwe kama wanaharakati? Risasi ingeweza kumpiga yeyote mle.
 
Back
Top Bottom