Sasa umuhimu wake ulikuwa upi?Hebu elezea.
Umuhimu wa jiwe;
1. Tumebaini udhaifu mkubwa, katika katiba yetu, ambayo inampa mamlaka makubwa rais, na rais akiyatumia basi inakuwa shida tu ndani ya nchi.
2. Tumewabaini Watanzania majasiri na waoga. Watanzania majasiri miongoni mwao ni Lisu!
3. Tumejifunza uthubutu. Jiwe alikuwa anathubutu ingawa uthubutu wake ulileta matokeo chanya au hasi katika jamii.
3. Tumejifunza wanasiasa wengine wa Tanzania ni njaa kali sana na wanafiki, wapo kwa maslahi yao na siyo kwa ajili ya wananchi. Hapa tunarejea wale waliounga mkono juhudi na wale wa kusifia ila kwa sasa wanapingana na jiwe.
4. Tumejifunza, kama nchi, planners of the state lazima wawe makini sana, ili waweze kuwachuja na kuleta viongozi makini katika nchi. Hapa hadi upinzani unatakiwa kuangaliwa wagombea wao, kwa sababu inaweza kutokea bahati nzuri wakachukua nchi pia. Mwingine anafaa kuwa mbunge, na si rais. Rejea, jiwe mwenyewe alisema alisukumizwa tu kwenye urais tu!
5. Tumejifunza kwamba, bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, kamwe wapinzani wasahau kuchukua hii nchi. Watakuwa wanashinda majimbo kutokana na huruma ya kiongozi aliyepo madarakani. Rejea engua engua ya wagombea wa upinzani. Hakuna hata mgombea mmoja wa CCM aliyeenguliwa.
6. Tumejifunza, kiongozi yoyote wa Afrika akitaka kupigania maslahi ya Afrika mwisho wake lazima uwe mbaya. Jiwe, aliingia kwenye ligi na wazungu katika kulinda rasilimali za nchi. Rejea kuzuia makinikia, lakini kwa sasa yanasafirishwa.
7. Tumejifunza pia, kama kiongozi wa nchi usipende kuwaamini sana wasaidizi wako, kiasi kwamba husikilizi malalamiko ya wananchi wanapowalalamikia viongozi hao. Rejea malalamiko ya wananchi kwa Sabaya.
Yapo mengi ya kujifunza, chanya na hasi