Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huwa nawashangaa sana wale mnaotaka wanao hama chadema wasikisema vibaya,bali wasema mazuri ya ccm

Ni hivi ccm ina watu wanao kisemea vizur,kwahiyo hawahitaji watu kutoka chadema wakisemee ccm,,wanahitajika watu wa chadema waseme udhaifu na mapungufu ya chama kama bakora ya kuwachapia

Na kiukweli kabisa wanawanyoosha vizur sana tena sana,,upinzani ndio kwaher tena ni swala la mda tu,,kiundwe chama kingine mbadala wa chadema

Kuna mdau mmoja hapo alisema sijui wasisahau mema waliyofanyiwa la sivyo karma itawaadabisha,,hakuna kitu kama hicho kwenye siasa,,kwasababu siasa ni uwongo mwingi na janja janja nyingi,,hapo karma inakaa pembeni,,karma inadili na haki,,kwenye siasa hakuna haki,period.
Alishindwa yule dikteta uchwara Magufuli hadi akaamua kufa ndiye huyo mbilikimo ataweza?
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema.👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/C9mLHisKGrc/?igsh=ZnN2Y2pwdTh4Mmpv

Msigwa kachanganyikiwa nadhani baada ya kukosa uwenyekiti wa Kanda automatically akahisi atakosa ubunge kwa tiketi ya cdm ubunge unamtesa sijui akikosea ubunge na huko ccm itakuwaje

Angekubaliana na situation akabaki mwanachama wa kawaida tu maisha yaendelee

Labda alibadili life style alipopata ubunge ndo shida ilipoanzis
 
Back
Top Bottom