Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
M

Mna uhakika Msigwa hajalogwa?

Anadhani hizo porojo zitakiangusha Chadema ambacho kiko mioyoni mwa Watanzania?

Alishindwa Dr John Pombe ambaye ali employ all mechanical, digital and political warfare?
Umemroga wewe?
 
Sikujua kama Msigwa ni KUBWA JINGA kiasi hiki .... I am so disappointed in him.

Kwa hii pesa ya ABDUL na Mama yake .... tutegemee mengi kwa miaka hii miwili. Ila kitu ambacho hajui ni kuwa amefanya very very big Mistake .... Very POOR timing. Bora angehama kile kipindi cha Mwendazake ...!!
Poleni sanaa! Kwa maana JEMBE hili, limetafutwa na CCM kwa zaidi ya miaka 10. Kikwete alimkosa, Magufuli alimkosa lakini kwa mama kaingia King!
Acheni tu, mama ni mwanasiasa aliyekomaa. Na sasa Mchungaji ndani ya kijani anaivua chadema nguo zote.
Hivi mtapitia wapi CHADEMA.
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema.
Sisi wananchi matatizo yetu sio Mbowe na chadema,tuna hitaji ajira,Elimu bora ect
 
Kiukweli haka kabinti, nakapenda pendo la kaka na dada, ni kabinti kanakojielewa, pamoja na Chadema kuwa ni chama hatari kwa vi binti miteremko, haka kabinti sio mteremko na mserereko, hivyo siamini kama Chadema wamekigusa, hivyo sasa hapo alipo CCM ni mahali salama sana.
Rejea zangu za haka kabinti

Kwa wasio mfahamu, kumfahamu zaidi na anasimamia nini, karibuni mitaa hii
Ref: Mnaweza kumsoma Upendo Furaha Peneza humu
Angalia nilipomfahamu, Life After Life: Regia Mtema (RIP) Amerejea Bungeni Kiaina?

  1. Upendo Furaha Peneza (@UpendoPeneza) | Twitte
  2. Upendo Furaha Peneza: Gold in the rough. Vijana CHADEMA mpo?
  3. Upendo Peneza ni malkia Nzinga Mbandi wa BAVICHA
  4. Upendo Peneza: Nahitaji kushinda na nitashinda
  5. Upendo Peneza leo Bungeni; Huyu Dada ana uwezo mkubwa sana
  6. Upendo Peneza wa CHADEMA atoboa siri ya CHADEMA na Sabodo
  7. Mungu amenipa nafasi nyingine ya kumtumikia na kutumikia watu wake. Praise be to God!
  8. Upendo Peneza kapata ajali Geita akitokea kwenye Mikutano ya Kampeni (05 Dec 2014)
  9. Upendo Peneza ataja sifa za mwanaume wa kumuoa
  10. Upendo Peneza (CHADEMA) awalaumu Wabunge wanaohama vyama. Asema chaguzi za marudio ni kucheza pesa za wananchi!
  11. Mheshimiwa Upendo Peneza asisitiza amani akiwa ziarani na Waziri Mkuu
  12. Mbunge Upendo Peneza(CHADEMA) akamatwa Geita mjini, aachiwa kwa dhamana
  13. Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti huyu, ana hoja ya Msingi!

Masikini Chadema...!, lost this Gold in the rough! .
View: https://youtu.be/aHJGqYKrX5U?si=uX9m2pe3OIrHIHTX,
Nimemsikiliza, nimeguswa!.

Nilikuja kumtafuta na nikaja kukutana nae View attachment 2879719
Hapo tulipokutana, yeye akiwa 20 something, mimi nilikuwa 50 something, nikiwa nimeisha oa na nina watoto 10!, hivyo sikuthubutu kumweleza lolote la moyoni mwangu, ila ningekuwa kijana... nakuapia... Haki ya ...!, nisinge kubali, .... naomba nisimalizie!.
Mungu ambariki sana Upendo Furaha Peneza!, hapa CCM imelamba dume!, naomba mimi ndio niwe mwana JF wa kwanza kuwatangazia Mbunge wa Geita 2025!.
P
 
Ishakua Mali kuchakaa
 
Baado mapema sana kutabiri hayo wananchi wa huku Geita ndo wataamua
 
Back
Top Bottom