Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema
Pamoja na udhaifu mkubwa wa Cdm
Lakini kwa heshima ya msigwa
Ningeshauri ajiuzila siasa
Atafute kazi zingine za kufanya
Anjidhalilisha kula matapishi yake

Dr. Slaa anabaki kuwa mwanasiasa wa upinzani mwenye msimamo
Aliahidi kuachana na siasa za vyama Hadi leo
 
Slaa ni liability amezeeka,Msigwa Bado Yuko hot yaani hapo mnatumia Hadi povu 😂😂
 
Lakini ni ukweli kasema
Yaani nimecheka kwa nguvu, Upendo na Msigwa ni kama wameahidiwa nafasi moja ya uongozi huko ccm, kwa sharti la atakayemzidi mwenzake kuharisha dhidi ya cdm ndio ataipata hiyo nafasi. Yaani huyo Msigwa na Upendo ndio wa kuiponda cdm ili kuipa mvuto ccm? Kwa kizazi kipi cha kuambiwa habari hizo?
 
Wanawapelekea spana tuu 😂😂
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao
Huyu ni mmoja wa wale Nyerere aliwaita malaya.
 
Mnaweweseka sana Kwa Msigwa na Peneza 😂😂
Nilikuwa najua ccm imechoka, ila sikuwahi kudhania imechoka kiasi kufikia wakati wa kuwategemea Msigwa na Peneza kuwapatia mvuto! Bwaahaaa Bwahaaaa nimecheka kinoma.
 
Msigwa ni njaa inamsumbua na ameingia huko CCM kutafutia mabinti zake ulaji.
Amekuwa Malaya wa kisiasa.
 
Nilikuwa najua ccm imechoka, ila sikuwahi kudhania imechoka kiasi kufikia wakati wa kuwategemea Msigwa na Peneza kuwapatia mvuto! Bwaahaaa Bwahaaaa nimecheka kinoma.
Pole sana
 
M
Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi
Mna uhakika Msigwa hajalogwa?

Anadhani hizo porojo zitakiangusha Chadema ambacho kiko mioyoni mwa Watanzania?

Alishindwa Dr John Pombe ambaye ali employ all mechanical, digital and political warfare?
 
Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi
Sio baada ya kushindwa uchaguzi?

Na Angeshinda je?
😅😅😅
Peter Msigwa nimemlaani kwa Jina la Bwana Mungu wa Israeli jambo baya litampata kwa dhihaka anayofanya.

Sisi watu wa Mungu tulimwamini akatangulia mbele ktk mapambabo ameamua kukejeli kazi ya Mungu?

Natamka kwa jina la Mungu, Mungu wa Yakobo. Msigwa Mungu atashughulika na wewe very soon
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema.
Msigwa ni mpumbavu sana kwanini useme sasa wakati ulikuwa sehemu ya uongozi wa Chadema?
 
Back
Top Bottom