Pre GE2025 Peter Msigwa: CHADEMA idhibitiwe kabla haijaleta vurugu nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katiba Mpya na Tume HURU ya Uchaguzi sio Tume hii inayozarauliwa hadi na Nape
Katiba Mpya inapatikana Kwa maandamano?

Katiba Mpya inasaidia nini mwananchi?

Baada ya hayo mumeipata? Tume huru ipo au nyie mnataka ya kwenu kichwani? 😂😂
 
Ndugu yangu Mchungaji Msigwa Asali ikipigwa na Jua inakuwa Wanzuki inalevya kaa kwenye kimvuli lamba tatatiiibu vaa na pekos anza kusikiliza zilipendwa.

Hivyo vijikaratasi vya Makala anavyokuandikia ili uvisome ni kujiaibisha tu.
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema.

View: https://www.instagram.com/reel/C9jbLgvIQIb/?igsh=N3N0d2N2a2xzaXQz
 
Siasa ni ajira na ili ubaki kwenye hiyo ajira lazima uponde upande wa pili
 
Mlikuwa mnaandamania nini?

Jibu ni kwamba baada ya maandamano yenu ya awali kupuuzwa Sasa mumepanga kuleta wavuta bangi wafanye looting Ili Mpate attention na kuharibu amani.

Mnatakiwa kudhibitiwa.

Moja ya hoja za maandamano ilikuwa ni hali ngumu ya uchumi, na mfumuko wa bei. Kama serikali imepuuza hoja hizo, basi imepuuza Watanzania waliowengi. Labda wewe ni bilionea hauguswi na changamoto za Watanzania wa kawaida.
 
kama imepangwa gen z iingie tanzagiza itaingia na kukinukisha na hakuna wa kuzuia, haya mambo yako globally coordinated, salama yenu tu tanzagiza isiwemo kwenye huo mpango vinginenvyo mtadhalilishwa na kuachwa uchi sana, usisahauu panya road tu watoto wa miaka 12 walisimamisha mji wote wa dar ije kuwa globally coordinated gen z ?
Ni mchungaji mpumbavu sana asiyejua kuwa mambo yanayotokea duniani ni mambo ya kiroho na yanalenga kubadili mawazo ya binadamu kudhani kuwa wanaweza kubadili asili ya vitu.

Mama samia na watawala wengi duniani wanapotoka kwa kuangalia mambo ya kidunia na kusahau uumbaji wa Mungu kuwa ndio salama ya viumbe vyote.

Tangu awamu hii ianze hata Mungu anadharaulika kuliko matajiri na watawala.

Yaani hata manabii na viongozi wa dini walekua machawa wa kudhani kuwa rasilimali za nchi hii zilizoumbwa na Mungu ni mali ya mama Samia .

Hii ni roho ya kufru kubwa imeingia tanzania. Na waindelea kujega roho ya dhulma na kutapanya rasilimali za asili pataibuka kundi lisilotegemewa na mtu yeyeote na litasambaratisha kila walichokusanya kamwa ajili ya ubinafsi wao na familia zao.

Msigwa alipigana vita vizuri ushindi ulekaribia ndio ametekwa na hakika kabla hajaondoka duniani atavuna alichokipanda mana hakuna CCM yenye nguvu ile ya Magufuli tena Tz. Hakuna uwezekano tena wa kuiba kura na nchi ikwa salama .

Hakuna Lkurugenzi atakayeiba kura akakenua meno .

Nawashauri wapinzai iwe tu wazi kuwa bila katiba mpya basi uchaguzi usiwepo kabisa. Kama katiba ni 2026 basi uchaguzi uwe ni 2027 na sio kinyume chake.

Uchaguzi wa dhuluma utapelekea kumwaga damu za watoto wa maskini kuuana wakitetea matajiri na watawala.

Wanaoumizwa na wizi wa kina Nape ,Kinana Bashe n Samia ni Polisi ambao wengi ni watoto wa maskini. Wanaoumizwa na vurugu ni Waajesi amaboa dengi ni watoto wa maskini . Leo kule kule mali asili watoto wa maskini wanatumiwa na Waarabu walioangamiza tembo wetu karne ya 18 na sasa wamekuja kama waporaji wa ardhi ya hifadhi na wanalindwa kwa mtutu wa binduki kuwahamisha wazawa ambao ni wawekezaji wa mifugo nchini yaani wamasai.

Dhulma za watawala dhidi ya Wazawa ndizo zinazoleta vurugu.

Na Msigwa asijidanganye kuwa kuna watu mil. 65 na wa ataeelea kukaliwa kimabavu na watu wasiozidi elfu 1. Ni kichaa tu asiyeweza kutabiri yajayo kutokana na kukopa kopa na kuiza rasilimali za nchi.

Taifa lenye mipango ya kukuza na kujega uchumi lilipaswa kuwa na akiba ya dhahabu zaidi ya tani Elfu kumi mpaka sasa na sio kununua Korosho na mahindi pekee yake.

Seukali ingepunguza kodi ya vifaa vya ujenzi, na pia kujenga nyumba za bei nafuu kwa wakulima na sio kununua mahindi halafu unapandisha bei ya vitu na bidhaa nyingine zote .

Mipango ya kuwanufaisha wanasiasa ndiyo itakayoibua kundi lisilo na siasa na kuwaimbiza wanasiasa kama Msigwa wanaodhani kuwa ukiwa CCM basi una amri juu ya uhai wa watu wengine .
 
Aliyekuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni Mchungaji Peter Msigwa amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji (mstf) Francis Mutungi kuhakikisha anafuatilia kwa karibu vyama vya siasa vya upinzani nchini ili kujuwa namna vinavyoendesha mambo yao

Mchungaji Msigwa ametoa ushauri huo hivi karibuni akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza vyama hivyo alivyodai kuwa vinalenga kuleta vurugu nchini vimekuwa vikiendesha mambo yao kinyume na Katiba za vyama vyao zinavyotaka jambo ambalo amedai kuwa linapaswa kudhibitiwa

Akitolea mfano chama chake cha zamani (CHADEMA) Mchungaji Msigwa amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuwa Tume ya Taifa Uchaguzi (Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi) haiko huru, sambamba na kukosoa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini uhalisia uliopo ni kwamba viongozi wa chama hicho hawafuati hata Katiba ya chama chao jambo ambalo linapelekea wakose uhalali wa kukosoa Katiba ya nchi

Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho

Amesema amelazimika kuondoka kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwa tayari kushuhudia akiendelea kutumika, kwani kwa muda mrefu amekuwa akikosoa sera na mipango ya CCM na serikali wakati ndani ya chama chao (CHADEMA) mipango na Katiba havifuatwi

"Katiba ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA -Chama cha Demokrasia na Maendeleo) haifuatwi, nasema kwa ujasiri mkubwa kwa sababu nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa takribani miaka 10 najuwa kinachofanyika" -Mchungaji Peter Msigwa.

Jambo TV

===

Nilimsikia Mbowe na kile kijalida chao cha Twitter wakidai kwamba mambo ya Gen Z yatakuja Tanzania sio muda ati Watanzania wavae sura ya Ujasiri.

Mbowe na genge lake wanatakiwa waelewe kwamba Watanzania sio punguani kwamba wataanza kuuana kisa kumpigania yeye Mbowe na wahuni wenzake eti waingie Madarakani.

Mbowe aelewe tuu kwamba Watanzania sio wapumbavu na kamwe hawawezi kuingia kwenye upunguani kisa kumfurahisha yeye.

Ni hivi Watanzania Wana utamaduni wa kuamtatua Changamoto zao pasi kuuana kama ambavyo genge la Chadema wanashadidia.

Kwa kuthibitisha Hilo walioanzisha kile waliita maandamano baada ya Wananchi kuwapuuza wakaishia mitini na sijui waliambulia nini.

Yaani walidhani eti Samia ataingia Polisi Barabarani kuwapa chati ila hakufanya hivyo matokeo yake wako wapi ? 😂😂😂😂😂

My Take
Hongera Msigwa kwa tahadhari hii uliyoitoa Kwa Serikali, naamini wahusika watawadhibiti mapema.
Mamluki chawa wamezidi kwa ufadhili wa wanavidumu,baada ya wengine kuonq mirija yao imekatiliwa mbali wanakuja na hoja mfu baada ya usaliti.
 
Amesema Katiba ya CHADEMA imeelekeza kuwa uchaguzi wa ngazi ya chini utasimamiwa na ngazi ya juu (yaani uchaguzi wa ngazi ya msingi utasimamiwa na tawi, uchaguzi wa ngazi ya tawi utasimamiwa na kata, uchaguzi wa kata utasimamiwa na jimbo, itaenda hivyo hadi kufikia ngazi ya Taifa) lakini viongozi wa chama hicho wakaamua kukengeuka Katiba ya chama chao na sasa chaguzi zinazofanyika ndani ya chama hicho zinafanyika kwa njia ya 'oparesheni' kwa kuwatumia maafisa walioteuliwa na makao makuu ya chama wanaoitwa ZOC (Zonal Oparation Commander) ambao kimsingi hawajatwa popote kwenye Katiba ya chama hicho
Ingawa Msigwa ni malaya wa kisiasa ila kwa hapa ana hoja. CHADEMA ijitafakari sana kwenye kufuata katiba yake. Ubabe wa Mbowe utazidi kuzalisha malaya wengi wa kisiasa.
 
Ikitokea hivyo wanavidumu watafaidi kwani watajiokotea tu.
 
Back
Top Bottom