Pre GE2025 Peter Msigwa hayuko huru, anapangiwa nini cha kusema na Amos Makala. Ushahidi wa video huu hapa

Pre GE2025 Peter Msigwa hayuko huru, anapangiwa nini cha kusema na Amos Makala. Ushahidi wa video huu hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
..Peter Msigwa hayuko huru huko alikokwenda.

..amefungwa remote, na anapangiwa nini cha kusema na Amos Makala.

..inaelekea Msigwa alikaririshwa, lakini katikakati ya press conference ikaonekana amesahau, Makala akampa makaratasi asome.

..kwenye video angalia kuanzia dakika 4:20
View attachment 3031046
Tatizo la Msigwa ni madaraka wala hana kingine.
 
Ama kweli Msigwa kaamua kujitia dole mwenyewe, Msigwa huyu aliyekuwa anaongea kwa kujiamini bungeni na bunge lote linakuwa kimya kumsikiliza kwa madini anayotema leo hii anafundishwa cha kusema na huyu kifutu Makalla. Amejidhalilisha sana yeye binafsi na familia yake. Msigwa akiwa kwenye ufahamu wake halisi anamzidi mara 100 huyu kifutu Makalla kwa uwezo wa kuongea na kujenga hoja.
 
..wanamdhalilisha Msigwa.

..huyu anahitaji kukombolewa.

..Nitaanzisha mchango wa kumkomboa kumsaidia arudishe dau alilolipwa.
Kwamba Msigwa ni mateka wa CCM na handler wake ni Makala? 😅

Ni rahisi zaidi kumeuelewa Msigwa kwa kukubaliana na maamuzi yake, ni yeye pekee anayejua kwanini ameamua hivyo.
 
Kwamba Msigwa ni mateka wa CCM na handler wake ni Makala? 😅

Ni rahisi zaidi kumeuelewa Msigwa kwa kukubaliana na maamuzi yake, ni yeye pekee anayejua kwanini ameamua hivyo.

..ndio nasema tumchangie arudishe fedha alizopewa ili awe huru.

..Msigwa sio mtu wa kudhalilishwa namna hii.

..aliingia ktk kikao kavaa suti, wakamvua wakamvalisha shati na kofia ya mboga-mboga.

..baadae Makala anampangia hata cha kusema?!!
 
Umesahau huyu faini alilipiwa na Magufuli?

Ccm wamejaa mazezeta kama Lucas Mashambwa, halafu hao Madc wenyewe ni kina Magoti sina shaka kwa Msigwa kupewa Udc.

..labda wampe Uenezi wa CCm ndio stahili na viwango vya Msigwa.

..hivi Nchimbi, Mongela, Makala, wangekuwa upinzani wangefika alipofika Msigwa?
 
..ndio nasema tumchangie arudishe fedha alizopewa ili awe huru.
Yawezekana ndoano aliyomeza sio pesa pekee.

..Msigwa sio mtu wa kudhalilishwa namna hii.
Husimlie yamini binaadam mwenye pumzi.

..aliingia ktk kikao kavaa suti, wakamvua wakamvalisha shati na kofia ya mboga-mboga.
Kwamba ilitumika mikono yao na sio yake kuvaa sare za CCM sidhani Kama ina Ukweli wowote.

..baadae Makala anampangia hata cha kusema?!!
Ninachoona hapa, kama ambavyo Makalla yuko kazini ndivyo na Msigwa nae yupo kazini.

Wanasiasa wawili wakifanya kazi yao ya Siasa, hadharani.
 
Back
Top Bottom