PreGE2025 Peter Msigwa: Nawashauri G55 waje CCM, hawana ushawishi kuendeleza siasa za mageuzi

PreGE2025 Peter Msigwa: Nawashauri G55 waje CCM, hawana ushawishi kuendeleza siasa za mageuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
ohooo kwahiyo CCM ndio jumba bovu, wabovu wabovu wote wanakuja huko, wakinywa uji wanatulia tuliii
SIyo jumba bovu. Wao ndio wamewalipa ili waondoke chadema. Na kutoa kauli za shutuma kwa uongozi wa chama uliochaguliwa kihalali.
Wawachukue. Maana huko chauma wanaenda kufa kabisa kisiasa.
 
CCM ni mzigo kwa watanzania, mzigo ambao hata tembo hawezi kuubeba, ila watanzania tumetishwa hilo zigo.
 
Moyo na akili ya Msigwa vimebaki Chadema ila mwili tu ndio umeenda CCM
 
Kwa tafsiri hiyo,
Kadubi alieshkuru kutolewa jalalani na jiwe

Inaonekana mpk Sasa bado yupo jalalani.

Kwa kifupi,
Mwamba mpk Sasa Hana tofauti na matonya
 
Amesema kweli kabisa! Nje ya CDM hawawezi kueleweka!
Waende tu CCM wakasugue mabenchi Lumumba.
 
“Hawa wanaohama sasa hivi CHADEMA ndio waliokuwa wanakiharibu chama na mimi ningewashauri tu kwamba wajiunge na CCM kusema kwamba wanaenda chama kingine cha upinzani kufanya siasa za mageuzi ni uongo”

“Wote hao niliwatuhumu hata kabla sijahama CHADEMA kwamba wanaharibu uchaguzi ndani ya chama wanaleta fujo walikuwa wanaamini kwamba Mbowe atashinda sasa Mbowe hakushinda wanaondoka kwa sababu zao zingine”

“Wale wakienda vyama vingine vya upinzani hawataaminiwa na wananchi na nikiwa mkweli kabisa sioni kama wanaacha maumivu ndani ya CHADEMA kwa sababu ni watu ambao hawana ushawishi kwa umma”-Peter Msigwa

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Chanzo Nipashe
Msigwa ni mkweli sana tatizo jahazi alilolipanda lina samaki waliooza
 
Back
Top Bottom