Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
- Nilijua utarukia hilo, hapana ameorodheshwa kwenye Wizara ya kazi, Brela wanaorodhesha makampuni, lakini waajiri wote lazima waishie kuorodheshwa wizara ya kazi, again yale yale hoja hakuna! ni vyema ukajionea huruma mkuu kama ulivyosema!
FMEs!
- Sasa unamteteaje Rostam huku huna dataz zake mkuu?
FMES!
Haya sasa. Waajiriwa wa makampuni yote tanzania wanaorodheshwa wizara ya kazi? Madereva, makarani, walinzi n.k ? Huko wizara ya kazi, idara gani? Na kila akihama au akiachishwa mfanyakazi lazima uripoti wizara ya kazi? na kila ukiajiri mtu mpya ni lazima uripoti wizara ya kazi? Unajua kweli unachozungumza?
Kweli hautuonei huruma wenzako.
Amandla.........
Mimi nasema caspian ni ya Rostam. Wewe uliye na data tofauti ndiye unayepaswa kuziweka hadharani ili uongo wetu uwe wazi! Kigugumizi cha nini, Mkuu, kuwataja wenye Caspian na Mirambo?
Amandla.........
- Jioneee huruma mwenyewe kwa uvivu wa kutofikiri, kwamba Wizara ya kazi nimesema wanaorodheshwa waajiri, sio waajiriwa Bwa! ha! ha! Duh unachekesha sana hapa mkuu Bwa! ha! ha! ha!
FMES!
- Ninaruida tena kwamba hizo kampuni kule Brella haziko under Rostam, na hata zingekwua haziajiri wafanyakazi 6000 kama alivyosema! Kwa hiyo hizi ni kamba mkuu!
Respect.
FMES
For some resorn kuna watu wengi tu wanamakampuni Under trust. Ukiwa na kampuni sio lazima jina lako liwe kwenye shareholders list. Kuna watu wengine wanawatumia their attoney to represent their shares therefore I dont see any problem
please shoot me!
Mimi nasema caspian ni ya Rostam. Wewe uliye na data tofauti ndiye unayepaswa kuziweka hadharani ili uongo wetu uwe wazi! Kigugumizi cha nini, Mkuu, kuwataja wenye Caspian na Mirambo?
Amandla.........
Wengine tunakuja jf wa kutoa maoni na msimamo...wengine hii ni kazi!!
maswali mazuri FMES, naona kwenye hili tuko pamoja mpaka kieleweke kama anataka, asipotaka tumlazimishe RA atueleze kwa kutumia state machinery!!- Mkuu mimi ndiye hasa nimemuandama Rostam kwa kauli yake kwamba ameajiri wafanyakazi 6000, huku akiwa hana kampuni hata moja iliyoandikishwa kwa jina lake, kama Mengi. Kama hoja yako ni valid basi angesema kampuni zinazomilikiwa na familia yangu, tumekuomba sana uzitaje umeshindwa kabisaa sasa unajaribu kuhalalisha hoja yake Rostam kwa habari ambazo hazina uhakika, ninakuomba tena hebu zitaje kampuni zzinazomilikwa na familia yake kwa sababu Brela hakuna kampuni hata moja iliyosajiliwa kwa jina lake, au familia yake!
- Kampuni ya Caspian haiko kwa jina lake, na wala yeye sio majority share holder, meaning kwamba anaficha something, sasa ni nini hasa anachoficha?
- Rostam amedai kwamba Mengi ni fisadi kwa sababu amekopa hela nyingi sana za Commodity Import Support, lakini Rostam mwenyewe alipobawna sana na Kubenea ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa ushahidi, Rostma alikubali kwamba hata yeye anadaiwa hela nyingi sana za mtindo huo huo wa Commodity Import Support, ambazo zilitolewa na wafadhili kwa ajili ya kuwasaidia wafanya biashara nchini, alisema " wengi tulikopa na tunaendelea kulipa."
Sasa hivi kazi ni moja tu nayo ni kukata mzizi wake wa urafiki na rais, then kumfikisha kwenye sheria, pole pole tunamkaribia maana kesi ya Mengi tayari iko mahakamani.
Respect.
FMES!
Imetoka hapa:ThisDay
Mbona mnachanganya mambo? Kutokana na taarifa mnayo quote, Caspian Construction Limited ambayo inajulikana kuwa ni ya wakina Rostam walikuwa na asilimia 19 za share za Vodacom na Planetel ambayo kutokana na maelezo ya Mzee mwanakijiji ni ya Noni, ilikuwa na asilimia 16, jumla kwa pamoja walikuwa na asilimia 35. Inavyoelekea ( ingawa si wazi) Planetel na Caspian waliuza share zao kwa Mirambo ( ambayo inadaiwa tena kuwa ni ya Rostam). Inavyoelekea tena ni kuwa Mirambo ilikuwa ikitafuta mkopo kutoka nje za nchi na walitaka kutumia share zao kama collateral kwa mkopo huo na si kuwauzia hao wageni. Share hizo zingeuzwa kama wange default kwenye mkopo huo. Sasa kuna ufisadi gani kwa mfanyabiashara kuomba kibali cha kuweka share zake mwenyewe kama collateral? Au tatizo ni kuwa benki yenyewe ni ya kigeni? Katika hii dunia ya kisasa ambapo fedha hazina mipaka lazima suala hili lingejitokeza. Kudai kuwa kujitokeza huko ni alama ya ufisadi ni unfair.
Amandla.........
Ulishathibitisha BRELLA?
Tatizo ni hayo makampuni kumilikiwa na vivuli vya watu kule BRELLA na kutumika kama money laundering na wajanja wachache.
Kwani ni Caspian tu ndiyo iliyokuwa rejistad Brela?
Hoja gani tena, Mkuu? Mnajicontradict wenyewe halafu unanilaumu mimi! Mzee Mwanakijiji ndiye aliyeleta hoja mama hapa sasa wewe unataka tumdharau tukusikilize wewe? Mzee Mwanakiji ambae si mshabiki wa Rostam by all means anasema hizi kampuni ni za Rostam na wewe ambae nawe si shabiki wa Rostam unasema si zake, sasa tumuamini nani? Mbona unashindwa kutueleza hizo kampuni za Caspian na Mirambo ni nani wameorodheshwa kama wamiliki? Ni lazima uwajue maana unajua kuwa si Rostam wala ndugu zake wameorodheshwa! Hili nalo lina ugumu gani? Au hauwajui il hali ulikuwa unafurahisha baraza! Na kama unavyodai, Rostam hamiliki kampuni yeyote (ikiwemo Kagoda) hayo mapesa ya EPA aliyachota vipi? Alikuwa anaenda dirishani BOT kupokea?
Tuoneeni huruma wenzenu. Hatuja soma lakini si punguwani kiasi hicho!
Amandla.........