hivi akili mnawekaga wapi? Hayo mambo ya New world order ni upuuzi ulioanza muda mrefu na ulifeli tangu enzi za vita za wazungu walizoziita world war 1&2 ambapo waliunda kila mbinu za kuufanya ulimwengu uwe kitu kimoja huku wakiusimika uongozi wa taifa moja kubwa kutawala mataifa mengine, hilo lilifeli.
Kama walifeli katika kipindi cha giza la ukoloni na ujima ndio waweze hivi leo?
Mambo ya kutawala ulimwengu kupitia Order ya kikundi kimoja chenye sheria zake na plan zake hilo haliwezekani kwa sasa, labda miaka 300 ijayo.
Kwanini haiwezekani?, kwasababu hayo mambo ya new world order yameletwa na watu magharibi wakiwepo hao fake jews, na baadhi ya Muslims, ambapo kwasasa hawa kwa upande waliopo unaofungamana na USA wanapata pingamizi kubwa kutimiza sheria&plan zao kutoka mataifa mengi yenye nguvu kama vile Russia,China, Iran, North Korea, Cuba, India, na baadhi kutoka Afrika,
Suala la kuutawala ulimwengu kwa Sheria moja na kanuni moja si jepesi kama mnavyodanganywa humo makanisani na misikitin, kuutawala ulimwengu na kila mtu inahijika nguvu kubwa ya kitechnolojia, ushawishi, ambapo kwa sasa hiyo nguvu haipo na haijawai kuwepo acheni kudanganywa.
Ili uutawale ulimwengu ni lazima mataifa yote makuu kama Russia, china, India, USA, UK, Canada, German, France, Italy, Japan, UAE, Saud Arabia, Qatar, Iran, South+North Korea, wakubali kuweka tofauti zao na wakubaliane kufanya jambo moja, jambo ambalo kwasasa haliwezekani wala dalili za kuwezekana kwake hakupo.
Ili uutawale ulimwengu vile vile ni lazma uwe na control ya Afrika nzima, ambako kuna population ya watu wengi ambao hawapo hata katika database ya control ya kimaeneo, tamaduni, sheria, hiyo technology ya kuamlisha kila mtu afuate mambo fulani hamna kwa sasa.