Ph.D bila kupata Master

Wanandugu,

Je, duniani kuna utaratibu wowote unaoweza kukufanya ukapata Ph.D bila kulazimika kupitia kwanza Masters? Kama inawezekana, ni institutions zipi zinao utaratibu huo?

Muulize Dr. Slaa, Katibu Mkuu wa chadema, ana PhD bila masters bila baccalaureate (bachelor) atakupa maujanja.
 
Inawezekana manake kuna Dr Padri yeye alisomea Biblia sasa hivi anajiita Dr

Nasikia Jk anatarajia kupewa shahada ya Udaktari (PhD ya ukiruka njia ulio tukuka)

Copy to zomba
 
Last edited by a moderator:
asante sana mkuu "the state" mungu akubariki. umenielezea vizuri sana, na kuna mtu ameniambia wanaopata admission harvard kutoka bongo wemesoma shule za kimataifa kama IST na lazima uwe na IB sasa wengine tunasoma local schools na vigezo ni vigumu.
 
asante sana mkuu "the state" mungu akubariki. umenielezea vizuri sana, na kuna mtu ameniambia wanaopata admission harvard kutoka bongo wemesoma shule za kimataifa kama IST na lazima uwe na IB sasa wengine tunasoma local schools na vigezo ni vigumu.

Usijali la fiesta. Kama nia yako ni kwenda havard usikate tamaa. Nenda US kasome bachelor inayoendana na ile unayoitamani ya Havard kwenye university yeyote hata kama ni ya kata na u-uperform vizuri. Hii itakusaidia kuingia kwenye system ya education ya US.Usisome diploma wala ndugu yake na diploma. Hii itakusaidia "ubebeke na utakuwa mwenzao''. After that, omba Havard kusoma bachelor inayoendana na ya kwako utaona jinsi watakavyokuchukua ki-urahisi mpaka utashangaa!. Na kama utakuwa uko serious na masomo, utapasua vizuri na watakupa scholarship za masters wao wenyewe na hata PhD as long as uko vizuri. Cha msingi u-focus kile unachokitafuta na umtangulize Mungu kwanza. However, maelezo yangu ni ya kibinadamu na experience. Ask God for a final answer.
 
Isidhaniwe utaratibu huo kuwa ni njia ya mkato kwa maana ya kufanya vitu vichache. Mara nyingi kunapokuwa na utaratibu huo, mwanafunzi atasoma kwanza masomo ya ku-qualify kwa masters degree. Halafu ataendelea kumpeleka kwenye masomo ya kufanya utafiti na kuandika tasnifu. Kwa hivyo basi, PhD hiyo itasomewa kwa si chini ya miaka minne.
 
bwana State that is excellent. Tungekuwa na wabongo design yako..hakika tungepiga hatua..personally maelezo yako nimeyapenda..very encouraging and supportive kwa wanaodhani kwenye kwenye hizi best unis ni miujiza..

Kwa uzoefu wangu, kwa kweli hizi shule safi za UK na US ziko VERY VERY competitive especially kwa masters na PhD. Mfano utakuta wanafunzi dunia nzima wanagombania nafasi lets say 30 au 50 za international students kuingia in one of these Unis kama Harvard au Yale au Stanford. Sasa hapa utakuta there are some of the brightest students kutoka China, Singapore..you name it! But again kama alivyosema State, God is the final answer. I always tell people..by applying you dont lose anything (though kwetu Tanzania hata hela ya application ni challenge!).

Kwa PhD....uzoefu wangu ni UK. Kwa hizi super elite institutions za UK kama Cambridge, Oxford, LSE, Imperial au UCL....na penyewe ngoma ni nzito. Mfano jamaa yangu ali-apply PhD pale LSE..and aliniambia out of 365 walichukua wanafunzi 8! (unfortunately hakupata). Kifupi its really competitive and by the way dont forget kwamba waingereza hata kwa funding ni wachungu sana!

Again, si lazima uende kwenye hizi super elite universities..you can always go to 'lower ranked unis' lakini..I would say..we all have dreams...kama tungeweza hakuna ambaye asingependa kwenda Harvard, Yale, Cambridge, Oxford au LSE.

Kwa vijana ambao bado mko ambitious, I would encourage you guys to work..really hard and keep on challenging frontiers of knowledge. Hakuna kilicho automatic. Na ukiapply shule..lets masters..well changanya..mfano ukiapply hizo super elites..weka na nyingine kama tano za kawaida! But again..ni vema ukajipima kwa kuangalia grades zako na CV yako kwa ujumla if they can earn you a spot in these best unis.

Otherwise..vijana wanaotafuta shule..keep on working..inawezekana..msikate tamaa. Maana hata wanokwenda kwenye hizi shule nzuri ni watu kama sisi. Ila ninachoona watanzania wengi wetu hatuchangamkii fursa..tunakata tamaa mapema..we rule ourselves out before we are ruled out!

NB: Before making your application ni muhimu sana ukacheck grammers na makosa madogo madogo kwenye CVs na documents nyinginezo. They speak volume on your behalf.
 
Wanandugu,

Je, duniani kuna utaratibu wowote unaoweza kukufanya ukapata Ph.D bila kulazimika kupitia kwanza Masters? Kama inawezekana, ni institutions zipi zinao utaratibu huo?

Nyie mabongo lala jadilini jinsi ya kupata elimu bora, kupata maji, huduma safi za afya kutwa kujadili watu wewe PhD ya Dr. Slaa ikifutwa itakupa maji? Itakupa elimu? Acheni ujinga taifa linateketea
 
Dr slaa
philosophy 3yrs(sawa na degree)
theology 3yrs(ongezea hapi degree nyngne- masters

yap; na anavigezo vya kusoma PHD: ingawa kwenye kwenye hzo course hapo juu kwenye system kikatoliki hawaiti degree wala masters
 
Mbona hamsemi kwamba Marehemu Prof Haroub Othman (Naomba kusahihishwa) pia alipata PhD bila kusoma Masterz?
Hizi ni sifa za kuingia PhD UDSM
Doctor of Philosophy (Ph.D.)
A candidate for admission to the Doctor of Philosophy degree shall hold the following qualifications:
a) An honours degree of the University of Dar es Salaam or an equivalent degree from a recognized University. Candidates who hold an unclassified degree e.g., M.D. should have at least a B grade average in the subject of intended Ph.D study.
AND

b) Masters degree of the University of Dar es Salaam or an equivalent Masters degree from a recognized university.
c) Candidates with a First Class or Upper Second class degree, or holders of a distinction or a credit in the case of unclassified degrees, may also be considered for Ph.D. registration. Such candidates have to initially register for the Masters degree and do at least one full year's postgraduate training. If they demonstrate outstanding performance, and obtain the authorisation of the Senate on the recommendation of the relevant College and DPGS Boards, they may upgrade their registration to Ph.D candidacy.
 

thankx mwana forum... umetuelewesha mengi mno...!
 
Muulize Dr. Slaa, Katibu Mkuu wa chadema, ana PhD bila masters bila baccalaureate (bachelor) atakupa maujanja.

Duh!!! watu kwa ufukunyuzi hamjambo. Yaani na mbwembwe zote hana hata bachelor? Hii kali.
 
Inawezekana manake kuna Dr Padri yeye alisomea Biblia sasa hivi anajiita Dr

Unajua "course contents" za hiyo biblia(theology/divinity) au unafikiri ni sawa na hizo shahada zetu?...matatizo ya shule za kata ndiyo haya tunayashuhudia kwenye post kama yako hapo juu

The guy has specialized in canon law....or sorry, you have no idea, what is it?!..
 
duh kweli hapa sie wa shule za kata ticha mmoja huyo huyo kiswahili and physics tukae kimya kwanza kushuhudia mtanange
 
duh kweli hapa sie wa shule za kata ticha mmoja huyo huyo kiswahili and physics tukae kimya kwanza kushuhudia mtanange


Mhh! Eti ticha mmoja huyohuyo Physics na Kiswahili, umenichekesha sana kijana
 
Mhh! Eti ticha mmoja huyohuyo Physics na Kiswahili, umenichekesha sana kijana

acha tu kama huamini sikumoja tembelea shule za kata vijijini ujionee hali halisi, nadhani unaweza ukakubali kwanini matokeo yao ya mitihani yanakua sio mazuri.
 
acha tu kama huamini sikumoja tembelea shule za kata vijijini ujionee hali halisi, nadhani unaweza ukakubali kwanini matokeo yao ya mitihani yanakua sio mazuri.

Pamoja na sababu nyinginezo, unajua wanafunzi wengi waliokuwa wakipenda na kuwa "vinara" wa Physics pia walikuwa wakipasi kiswahili bila tabu, lakini kwa "waliobobea" katika kiswahili hawakuweza hata kidogo kupasi Physics, sasa ishu ni kwamba hawa vinara wa Physics+(Biology, Math, Chem.Geog) hawa wote aidha ni madaktari au mainjinia wazuri, hivyo sidhani kama wako huko kwenye hizo shule za kata; hii inaniaminisha kuwa huyo mwalimu anayefundisha Kiswahili na Physics, bila shaka specialization yake ni Kiswahili-Hahaha...(Only Fallacy of composition)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…