Ph.D bila kupata Master

Mhh! Eti ticha mmoja huyohuyo Physics na Kiswahili, umenichekesha sana kijana

hii kitu ni kawaida kwa shule za kata ambazo zina mwalimu mmoja wawili au watatu.mi mwenyewe kabla sijaacha ualimu nimewahi kufundisha biology form 2 na chemistry form 1. wakati masomo yangu ya kufundisha was geo na hist maana a level nilisoma arts,ila olevel nilisoma mkondo wa science,na a level nilosoma kwa credits za masomo ya sayansi ns arts baada ya combination kugoma kubalance ns hesabun nikala mswaki ambao sijui hadi leo hii ulitokea wapi. hii ndio bongo.
 
Yes, mi nafahamu watu wawili, lakini ni University za Ulaya. Kinachotokea ni kuwa mwanafunzi anaanza Masters programme lakini njiani kutokana na mwelekeo wa data na aina ya matokeo basi msimamizi wake anaweza kudai-kuipandisha daraja hiyo kazi ili iwe ya kutoa PhD. Kwa hilo mwanafunzi ataongeza aina fulani fulani ya "analysis" na mwelekeo wa kazi yote, akifaulu anapewa PhD yake.
 
Mkuu pascal acha mawazo ya kivivu kama unapenda ile tyto bas anza hata uganga wa jadi au wa tba mbadala uwe kama dk ndodi, dk rahabu au hata uwe profesa kama vile profesa maji marefu, coz unachokitaka kitakusumbua sana hata kwenye field au eneo lolote ama sivyo ukitunukiwa huo uende zako kuwa mbunge huko mambo ni rahis tu, mara kugonga meza au kusinzia kama kawa.
 

Guys mko kama sio watanzania, relying on your moral assistance and encouragement, ki ukweli nimekua inspired na mawazo yenu! Mungu awatie nguvu kwa sababu najua sio mimi tu nliefaidika!!!
 

The state japokuwa sijakuuliza mimi swali hili ninakushuru kwa lugha nzuri uliyoitumia kujibu maswali yote Mungu akubariki sana natamani kama ningekuona hongera sana kwa ustaarabu wako
 
There are so many universities vinavyo offer PhD without Msc, you just have to do your homeworks guys. I am doing this program, and this is my final year, I will put my publications in the near future!! If you are looking for Engineering Research Programs don't hersitate to contact me through my inbox.
 
Dah kuna misconceptions nyingi kidogo kwenye thread hii.

Kwa nchi ninayojua (marekani), ukiona mtu ana PhD lakini hana Masters, maana yake siyo ameruka Masters au amefanya ujanja.

Katika masomo mengi, hasa sayansi, vyuo vingi havina hata programu za Masters. Kwa mfano watu walioko na Masters ya Physics au Chemistry marekani ni wachache sana. Kwa Engineering ni sawa, lakini kwenye Basic Sciences (Physics, Chemistry, na Biology) ni wachache kabisa. Kwa sababu kama unataka kuwa mwanasayansi (tofauti na mhandisi) bila PhD huwezi kupata kazi za basic research.

Hivyo, ukimaliza bachelors ya Physics (kwa mfano) marekani, na unataka kuwa Physicist, lazima uende moja kwa moja kusoma PhD (ambayo inachukua muda wa miaka 5 mpaka 7, inategemea na spidi unayofanya dissertation yako).

Hautapata Masters, lakini kwa kweli coursework ya Masters ipo ndani ya hiyo PhD. Kwa hiyo mara nyingi ukikuta mtu anayo Masters ya somo la sayansi, alikuwa anasoma PhD lakini haikumaliza. Kama unasoma PhD na umemaliza coursework ya kutosha, ukitoka kwenye hiyo programu kabla ya kumaliza, chuo kitakupa Masters. Kwa kiingereza hiki kitu kinaitwa "consolation prize". Lakini hiyo Masters unaweza kupata tu kama umemaliza coursework ya kutosha na umeshafanya Masters Thesis.

Ushauri wangu ni kwamba msione mtu mwenye PhD lakini hana Masters amechukua shortcut. Hapana. Mara nyingi ukiwa accepted kwenye PhD program baada ya kumaliza bachelors, maana yake ni kwamba coursework ya Masters ipo ndani ya hiyo PhD.
 
umemaliza kila kitu mkuu
 
Mbona wanasema kwa Tanzania ukisoma PhD bila kuwa na masters ukirudi TCU wanakudisqualify. Je, kuna mtu yoyote ambae imemtokea hii? Naomba uzoefu wenu wadau!
 
Wanandugu,

Je, duniani kuna utaratibu wowote unaoweza kukufanya ukapata Ph.D bila kulazimika kupitia kwanza Masters? Kama inawezekana, ni institutions zipi zinao utaratibu huo?
What important is competence in the subject matter. Unaweza ukawa na PhD 10 na bado ukaonekana kiazi. Dogo piga msuli usitafute njia ya mkato.
 
What important is competence in the subject matter. Unaweza ukawa na PhD 10 na bado ukaonekana kiazi. Dogo piga msuli usitafute njia ya mkato.
The vise versa is true! You can't be competent with standard seven education, still more education is needed to improve your competence!
 
Hyo ni sawa kusoma sekondary bila kupitia primary xul
 
Inawezekana kbs, hata Sumaye alikuwa na Diploma then akaenda kufanya Masters Degree kule Harvard
 
Kama inawezekana mbona vyuo havitangazi huo mfumo ukafahamika kwa wanaohitaji elimu ya aina hiyo kama ilivyo kwa degree zingine? Wekeni na link za hivyo vyuo vinavyotoa PhD bila kupitia masters!
 
Kama inawezekana mbona vyuo havitangazi huo mfumo ukafahamika kwa wanaohitaji elimu ya aina hiyo kama ilivyo kwa degree zingine? Wekeni na link za hivyo vyuo vinavyotoa PhD bila kupitia masters!

Angalia prospectus ya SUA ya last year utaona hiyo kitu
 
Umeleza vizuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…