PhD za heshima: Msimu wa shahada za Ikulu umeanza tena

Aibu kubwa sn unajiita Dr/Pro huku hakuna umeme, maji, dola wala petrol
Shida ya Viongozi wetu ni kutanguliza maslahi yao binafsi kuliko matatizo ya Nchi.

Solution za mambo yote hayo tunazo kwa kutumia hizi hizi Masters na degree zilizopo. Changamoto ni kuwa kupitia ukosefu wa dollar, Umeme na Maji kuna Viongozi wananufaika.

Poor us 😒
 
Tumelaaniwa sisi
 

Punguza unafiki, PhD sio karanga kila mtu anapewa
 
Aliyenacho huongezewa asiyenacho hata kidogo kilichopo kitachukuliwa. Ukweli mbaya kuhusu maisha ya dunia hii.
 
Ukishaelewa kwamba, PhD hata ya kuitafuta kwa kuisomea mwenyewe, haina maana kama haiendani na kazi ya mtu, basi utagundua kwamba haya malalamiko ya PhD za heshima hayana maana.

Kwa sababu, malalamiko haya yanatoa picha kwamba, labda wenye PhD za kusomea wenyewe wana maana zaidi.

Wakati, kiukweli, usomi wowote wa kuoneshwa kwenye vyeti hauna maana kama elimu hiyo haionekani kwenye maisha na kazi za mtu.

Suala hapa ni kwamba elimu yoyote inayoishia kuoneshwa kwenye vyeti, bila ya kuonekana kwenye maisha na kazi za mtu, haina maana.

Ukielewa hilo, hutaona tofauti ya PhD ya heshima na ya kusomea.

Kwa sababu hutampima mtu kwa vyeti vyake, utampima kwa kazi yake.

Tatizo Watanzania wengi mnataka kupima watu kwa vyeti, badala ya kupima watu kwa kazi zao.

Ukisoma Samia alivyosaini Instruments of Full Powers kwenye IGA na DP World, utajua kuwa huyu mtu hata angekuwa na PhD ya kusomea mwenyewe, bado ni mtupu tu.

Ukimsikiliza Samia alivyoongea kuhusu "flat chested athletes" utajua tu huyu mtu hata kama angekuwa na PhD ya Harvard ya kusomea mwenyewe, inawezekana kafanyiwa, bado ni mbumbumbu tu.
 
Huyu mama abdul wa kizimkazi Hana nia njema na waTanganyika baada ya waarabu sasa kaingia kwa wahindi 😭😭😭πŸ˜ͺ

waarabu na wahindi wote wana roho mbaya na ubinafsi wa hali ya juu😭
 
ufisadi una sura nyingi mkuu...si ajabu ukasikia UAE nao wanatoa
 
Mtu analala anaamka ana PhD!


Anyway,Pongezi kwake Dr Samia
Bado wewe, maana nimeambiwa unataka kugombea Mwaka 2040 kwahiyo utaitwa Mheshimiwa Dr Saint Anne πŸ€—

Hautaweza kuibadiri political atmosphere ya Tanzania kwa sasa, maana Machawa wa kufanikisha haya wamefungua hadi Ofisi kwa kazi hii πŸ™Œ
 
Tena huku mtu akia Dr ukimuita kwa jina lake utasika AM Doctor
 
Kuna mtu aliwahi andika, " kusoma sana ni uoga wa maisha".
Mimi naandika kuwa kukubali kutunukiwa Ph.D ya heshima na kukubali kuitwa dokta ni kukubali kuwa wewe huna uwezo wa kuipata hiyo doctorate kwa kuipambania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…