PhD za heshima: Msimu wa shahada za Ikulu umeanza tena

PhD za heshima: Msimu wa shahada za Ikulu umeanza tena

Mtahuzunika saaana mnao muonea gere mama. Pia fahamuni honorary degrees ni heshima ambayo inatolewa kwa vigezo maalum.

Kuna wasomi katika vyuo vikuu watu wanajua na kuthamini uongozi wa mh rais Samia katika:
1. Kuendeleza amani nchini hasa katika kipindi cha mpito baada ya kifo cha hayati Magufuli.
2. Kupunguza heka heka na wapinzani na kuwapa nafasi ya kuendesha shughuli zao.
3.Kuendeleza na kuongeza miradi mikubwa muhimu ya miundo mbinu itakayo panua uchumi wa taifa.
4. Ajira na nyongeza za mishahara.
5. Kupanua uhusiano na nchi nje ili kuvutia uwekezaji.
6. Kuongoza juhudi za kuimarisha na kupanua sekta ya utalii..
7.Kuboresha huduma za kijamii hasa katika elimu na afya, maji na mawasiliano
8. Ni mwanamke wa kwaza kywa rais nchini na amekua mfano wa kuwainua wanawake.

Mama chapa kazi tu usipoteze muda na distractors.
Swali la msingi ni kwa nini hawampi raisi au waziri wao mkuu wanakuja kumpa mama Samia ambaye tunajua hana mchango wowote kwa India?
 
Kuna wakati tuliambiwa China walimpa u-profesa JK. Hapo ilikuwa ni baada ya kupewa PhD za heshima huku na huko! Sasa tena mambo yameanza!

La kujiuliza eti chuo kikuu cha India kinaona mchango wa Rais wa TZ ni mkumbwa kwao kuliko Waziri mkuu wao. Watu fulani wanashangilia, lakini kwa tunaojali nchi, hapo kuna jambo. Ni wepesi wa kuelewa udhaifu wa viongozi wetu.

Si mulionesha njia kwa UD kumpa rais wetu PhD ya heshima? Eti baada ya mwaka mmoja tu Chuo kikongwe cha UD kikaona huyu ni kiboko kwa mchango wa maendeleo. Ila hiyo ilikuwa kabla ya kuuza bandari zetu.

India waliona na waliskia na naamini ubalozi wao ulitoa taarifa hizo kwamba PhD ni dili kwa Ikulu yetu. Sasa PhD zitamiminika sana! LAkini tujiandae kupoteza vingi. NI sawa na biashara ya shanga na kwa dhahabu na almasi za shinyanga.
Mungu anatuwazia nini lakini?
Mbona nchi yetu imekuwa kichwa cha mwendawazimu?

Kila kinyozi anajinyolea atavyo?
 
Sijui kwanini baada ya utawala wa Kikwete PhD zimekuwa deal kwa MaRaisi wetu.

Dr Jakaya Kikwete
Dr John Magufuli
Dr Samia Suluhu
Dr .............ajaye

Mbona jambo hili la Dokta......halipo Kenya

Rais Mwai Kibaki
Rais Uhuru Kenyata
Rais William Ruto
N.k

Sisi tuna shida mahali 🙌
Mkuu hat America sijasikia, Dokta Washington, Dokta Bush wala Dokta Obama au Dokta Trump. Hata urusi hakuna Dokta Putin.Tanzania tunamaradhi ya ubongo nadhani.
 
Mkuu hat America sijasikia, Dokta Washington, Dokta Bush wala Dokta Obama au Dokta Trump. Hata urusi hakuna Dokta Putin.Tanzania tunamaradhi ya ubongo nadhani.
Ni kweli, nadhani kuna mambo ya kufanya kuondoa hii mindset
 
Mtahuzunika saaana mnao muonea gere mama. Pia fahamuni honorary degrees ni heshima ambayo inatolewa kwa vigezo maalum.

Kuna wasomi katika vyuo vikuu watu wanajua na kuthamini uongozi wa mh rais Samia katika:
1. Kuendeleza amani nchini hasa katika kipindi cha mpito baada ya kifo cha hayati Magufuli.
2. Kupunguza heka heka na wapinzani na kuwapa nafasi ya kuendesha shughuli zao.
3.Kuendeleza na kuongeza miradi mikubwa muhimu ya miundo mbinu itakayo panua uchumi wa taifa.
4. Ajira na nyongeza za mishahara.
5. Kupanua uhusiano na nchi nje ili kuvutia uwekezaji.
6. Kuongoza juhudi za kuimarisha na kupanua sekta ya utalii..
7.Kuboresha huduma za kijamii hasa katika elimu na afya, maji na mawasiliano
8. Ni mwanamke wa kwaza kywa rais nchini na amekua mfano wa kuwainua wanawake.

Mama chapa kazi tu usipoteze muda na distractors.
Kwa umri wako, umesikia mara ngapi kiongozi mkuu wa US, China, Canada, Russia, UK, Autralia, wakipewa digrii za heshima? Linganisha mendeleo ya nchi zao na hili vumbi letu hadi ikulu.
 
Hivi ukipewa hizo PhD za heshima alafu ukalataa inakuaje?
Nijuavyo kwa kiwango cha rais kupewa digrii ya aina hiyo, lazima vyombo husika vione umuhimu wa kusema ndiyo. Hiyo ni digrii ya heshima kwa rais, siyo kwa Samia. ndo maana sababu wanaozoa Wahindi ni za undandaji wa rais.

Yaonekana yeye anaamini ni Samia siyo rais maana baada ya kupewa na wahindi, hotuba yake badala ya kusema alichofanya kama rais, yeye anakumbuka maisha ya nyumbani kwao utadhani ni PhD ya kusoma kwake.
 
Nyerere nasikia alipewaga nyingi tu ila hakutaka kuitwa doctor kwa sababu alikuwa anajiamini na kichwa chake akataka aendelee kuitwa mwalimu tu.
By 1987 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM ilitangazwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa Rais wa JMT kuwa Mwalimu alikuwa na Degree za Heshima 18 kutoka vyuo vikuu maarufu tofuti hapa Duniani.
 
Aliyeongoza kwa PhD ni Mandela. Takriban PhD za heshima 64 tangu akiwa gerezani hadi kifo chake. Uzuri alikuwa safi kichwani na zingine alikuwa anatangaziwa kupewa bila hata kuhudhuria. Tena vyuo vizito!
Sisi tunapewa za India. Sawa tu!
 
Back
Top Bottom