Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Philip Mangula ang'atuka nafasi ya Umakamu Mwenyekiti CCM Taifa. Abdulrahman Kinana apendekezwa na Halmashauri Kuu kuchukua nafasi yake

Ni takriban wiki moja sasa tumeona wachangiaji mbalimbali humu Jamiiforums.

Wanajaribu kutupasha kuhusu CCM kuwa na mkakati wa Abdurahman Kinana kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho huku Bara.

Kwenye kikao chao kinachoendelea huko Dodoma kuanzia leo 31/03/2022.

Abdurahman Kinana ambae alishindwa kujivua Magamba?

Kinana yuleyule wa Falcon Dry Cleaners ya Arusha na washing machine ya Mount Meru Hospital?

Yule Kinana wa Makontena ya Meno ya Tembo na meli yake kule Ughaibuni?

Kinana huyuhuyu mzee wa mtandao wa JK?

Je ni Kinana huyuhuyu ambae Simu yake na Makamba Sr pamoja na Nape,ilinaswa na kumlazimu yeye kuzira chama cha CCM?

Huku mwenzake Nape akienda Ikulu kwa miguu kuomba msamaha?

Je huko CCM hakuna hazina ya viongozi waadilifu kuweza kushika hatamu hadi muishie kulamba matapishi yenu?

Hivi CCM mmesahau jinsi mlivyokuwa mnaelekea kaburini,kabla ya JPM kuja na "CCM ya Magufuli"

Au CCM mnajipanga kuja kukomba kile mlichobakiza kabla ya kuikabidhi nchi kwa chama kingine?

UP Hapa Kazi tu hamsikiki kulikoni mnakwama wapi?
 
Mangula ameachia nafasi ya umakamu mwenyekiti CCM, kaona isiwe tabu.

Ila hii Ni Mara ya Pili mzee anawekwa pembeni, sijajua ana tatizo gani na wenzio huko.

Nafasi imechukuliwa na Kinana

Membe karudishwa CCM

===

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula leo Alhamisi Machi 31, 2022 amewasilisha katika Halmashauri Kuu ya CCM barua ya kuachia nafasi hiyo.

Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM kimependekeza jina la Katibu Mkuu wa zamani Abdulrahman Kinana kuteuliwa kupigiwa kura za kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Bara ambapo atachukua nafasi ya Philip Mangula.

Kikao hicho kimefanyika leo 31 Machi 2022 Jijini Dodoma.


Pia soma;

1). Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

2). Ukatibu Mkuu CCM: Nani anafaa kuchukua nafasi ya Daniel Chongolo? Kinana ndani


Hawa wengine walikuwa wanasikiliza simu zao kwa siri sasa wamerudi!!!!

 
Kweli kabisa.

Sasa tutafute msemo unaoendana na hizi siasa za sasa: Tuziite "Siasa za Ujanja ujanja"! Sijui kama hili lina 'rhyme' vizuri!

Hata hivyo, tofauti yake ni nini hasa kati ya hizo siasa mbili. Matokeo yake yatakuwa ni tofauti?
Hizi ni siasa za Urefu wa kamba....
 
Kwani hata kabla ya dhalimu walikuwa wanashinda kihalali? Dhalimu yeye hakuwa anaiba kura tu, bali alikuwa anapora mchakato wa uchaguzi. Yaani alikuwa mshenzi asiyevumilika.
Ahaaa.. Kwa hiyo kumbe mnapenda hiyo ya kutoshinda kihalali ila mnachukia sana hiyo ya kupora uchaguzi?,!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Wacha waingie hawa majizi wa msoga, kuliko yale majizi wauaji wa sukuma gang.
Hata hao wanauana rejea kauli ya kikwete, "CCM hatuachiani maji mezani"
Sema wao wanaua bila kuacha alama, Mwakyembe ilibaki kidogo tu
 
Kwahiyo Mangula hatakiwi kustaafu. Ni mpaka AFIE madarakani?

Hii NCHI, wanasiasa Ni tatizo. Ila wafuasi wa wanasiasa wote Ni tatizo kubwa mnoo
Mm pia najiuliza Kama ww, sipo CCM Wala sio mfuasi wa mangula. Maana pia nilishangaa unakuwaje mtu mwenye 70+ anakuwa na nafasi kubwa hivyo.
Ni Kama Sasa ilivyo kwa Kinana 70+ bado nafasi kubwa Kama hiyo
 
Mzee aliupiga mwingi wakati ule 2015 ccm imechafuka kweli kweli hata wendawazimu hawatak kuisikia,mzee akazunguka nchi nzima akatuliza hali ya hewa.

Baada ya kuhitimisha kampeni akaona Diamond anapewa bil 1,yeye hakupata kitu,akaona afanye aliyoyafanya na yeye akachota za kwake kutoka hazina ya chama,mwendazake aligundua na akamchukia sana,likawa bifu
CCM 2015 ilishinda uchaguzi? Acheni uongo
 
Back
Top Bottom