Sasa Chadema huu ndo muda wenu wa kushine kama mtakuwa na akili. Nendeni kwa wananchi mjijenge. Maana ukweli sasa hii iliyopo ni serikali ya kufavor matajiri ambao ni minority hapa Tanzania.
Mkuu 'Victoire', naona umekuwa mpole!
Lakini naona bado huelewi vizuri. Ngoja nikusaidie kidogo.
Unaposema "CHADEMA waka-'shine,'" waka-'shine' kwa ajenda ipi? Huoni kuwa CCM ya Samia ndiyo CHADEMA ya Mbowe?
Labda useme kwamba CHADEMA waanze mikakati ya kujiingiza ndani ya CCM(CHADEMA) ya Samia.
Kukurahisishia zaidi ni kwamba, usione ajabu sana siasa zetu sasa zikawa kama zile za Kenya zilivyo sasa. Haya mavyama ya CCM, CHADEMA, ACT, CUF, yatakuwa ni vyombo tu vya kubeba watafuta fursa. Inapofika wakati wa kusaka uongozi, mavyama yote yanahaha kutafuta mahala pa kujibanza ili yawe kwenye ulaji. Kwa hiyo anza kutegemea , kwa mfano Muungano wa CCM na CHADEMA hapo 2025, na mambo yanakwenda 'smoothly' kama ugali na mlenda.
Umenielewa?
Jambo hili ni rahisi sana sasa kulieleza kwa wananchi, na hapo ndipo kila mtu atakapoanza kuimba 'Maza, Maza, Maza.....' , pengine hata wewe utakuwa ni kati ya hao waimbaji wa sifa za mama!
Mbowe, inawezekana tayari yupo huko Kenya (chuoni) kujifunza jinsi haya mambo yanavyofanya kazi.
Wewe na mimi hatukuwepo Mbowe alipoitwa Ikulu kujadili "mwafaka, haki, uhuru" Kuna maafikiano mazuri kuliko hayo?
Ngoja nikuache kwa sasa uyatafakari hayo.