Philip Mangula: Magufuli alitaka kujiondoa kwenye mizunguko ya kutafuta wadhamini kisa wenzake walikuwa wanatoa pesa

Philip Mangula: Magufuli alitaka kujiondoa kwenye mizunguko ya kutafuta wadhamini kisa wenzake walikuwa wanatoa pesa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Philip Mangula, amesema hayo Septemba 4, 2026, wakati akihojiwa kupitia Clouds Media.

"Magufuli alikuja nyumbani kwangu hapa Osterbay siku moja ya Jumapili, akaniambia, 'Mzee, mimi nataka kujiondoa kwenye hii mizunguko ya kutafuta wadhamini.' Nikasema, 'Kwa nini?' Akasema, 'Hapana, mimi sina pesa kabisa. Wenzangu wanatoa pesa, mimi nikienda mahali mnaongea nao, mnataka kuondoka wanasema, sasa mnatwachaje?'

Basi yeye alikwenda Iringa kutafuta wadhamini 30, kufika pale mjini akambiwa na kiongozi aliyekuwepo wakati huo, 'Bwana usipoteze muda wako hapa, wote hapa wamemshika mkono Lowassa.' Akanipigia simu, 'Mzee, hivi kweli nikose watu Iringa hapa?' Nikasema, 'Hapana, nitampigia Katibu wa Chama wa Wilaya akupeleke kwenye tawi lolote nje ya mji.'

Alipofika kule akakuta watu 50 wamemsubiri. Akaomba wadhamini 30, lakini bahati nzuri wakawa wamejaza fomu zake. Baada ya hapo anataka kutoka wanamuuliza, 'Rasi unatuachaje?' Akasema, 'Nawaacha kama nilivyowakuta.' Huyo kwenye gari akachomoka! Lakini tayari walishajaza majina ya wale wadhamini 30."

Hapo pekundu ndipo kwenye kosa, mngewaambia ukweli na dhamira yenu toka rohoni kuwa hamnunui watu ili mpate watu safi

Huu uliofanyika ni uhuni wala siyo ujanja
 
Back
Top Bottom