Philip Mpango na Selemani Jafo tokeni hadharani kuusemea muungano ukipopolewa na Lissu!

Philip Mpango na Selemani Jafo tokeni hadharani kuusemea muungano ukipopolewa na Lissu!

Wazanzibar waliopo bara ni wengi mno kiasi endapo wanarudi znz sijui watakaa wapi?, USHOGA NI MBAYA SANA, KWA SABABU UNATUMIA MAUMBILE TOFAUTI NA ILIVYOPANGWA NA MUUMBA YOU JUST GO VICEVERSA!, KATIKA KILA JAMBO!, UMOJA NI NGUVU, HUKO ULAYA WATU WANAUNGANIKA, SASA HUYO BWEGE ANASISITIZA MGAWANYIKO, A VERY STUPIDITY!
Umeona kuandika kwa herufi ndogo hatuelewi, ikabidi uongeze na herufi kubwa baada ya zile bold kutokuleta matunda pia.
Kwani ukisema kwenye Muungano tulikosea ili tuanze upya kuna kiungo mwilini kitanyofoka?
 
ukiona mtu anaandika anachanganya herufi kubwa na ndogo ujue anamatatizo ya ubongo,madhara ya ile sindano ya Jonson&Jonson
 
Masuala ya muungano nchi yamewekwa katika ofisi ya makamu wa Rais ambapo pia kuna wizara na waziri anayeshughulikia muungano na mazingira.

Sijui kwa nini serikali wameweka muungano na mazingira kama jambo moja lakini kwa sababu kuna hii wizara tayari inabadi mawaziri wake wakishirikiana na makamu wa rais wajitokeze kuutetea kwa hoja mbele ya umma wa Tanzania ili kuifanya imara zaidi kama inawezekana.

Ilipaswa kabla Kinana hajajitokeza hadharani au hata baada ya yeye kujitokeza kumjibu Lissu basi makamu wa Rais Phillip Mpango akisaidiana na Waziri Jafo wajibu pia hoja za Lissu katika majukwa mbalimbali. Jambo la kushangaza mpaka sasa wote wako kimya na wanajibu watu wengine wa mbali kabisa!

Na ikumbukwe kwamba ni wakati wa Samia akiwa Makamu wa Rais, ndipo zinazoitwa KERO ZA MUUNGANO nyingi zilishughulikiwa. Samia aliitumia sana nafasi hiyo kushughulikia maswala ya Zanzibar. Ni bahati mbaya tu kwamba watu hawataki kujikumbusha.
Lakushangaza zaidi, Magufuli upande huo wa maswala ya muungano hayakuwemo kabisa kichwani mwake; ndiyo maana Samia akawa na ujasiri wa kuyamaliza mwenyewe.
 
Kwahiyo Mpango anajua huko Zanzibar Kuna watanganyija wangapi ni wakuu wa wilaya?, au watanganyika wangapi wanaomiliki Ardhi?.
 
Taja faida 5 zitakazopatikana kwa kuvunja muungano
Hoja sio kuvunja muungano ni ama tuwe na muungano wa serikali moja au serikali tatu.
Muungano wa serikali mbili ndio unaoleta changamoto zilizopo sasa kila upande hauridhiki.
Zanzibar inahisi kupokwa madaraka yake na Tanganyika inahisi Wazanzibar wanapendelewa.
Wananchi wanahisi huu muungano ni wa viongozi na sio wananchi na unalazimishwa kuwepo.
Na ndio maana viongozi hawapendi muungano uhojiwe popote.
 
Si hadi wawe na HOJA za kujibu!!..

Swali dogo la nyongeza
Kwanini Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania,hawatambuliki Zanzibar?
 
Taja faida 5 zitakazopatikana kwa kuvunja muungano
1.Serikali ya Tanganyika itaacha kulipa Mishahara + marupurupu kwa Wabunge toka nchi jirani

2.Bunge la Bajeti litakuwa linajadiliwa kwa muda mfupi kwa kuwa tutakuwa na Wabunge wachache,tutaokoa Hela+ MUDA
3.Ushindani kwenye Ajira na watu toka nchi nyingine ya Znz ,hautokuwepo
4.Hakutokuwa na uteuzi wa nafasi za Kisiasa kwa watu toka nchi jirani ya Znz

5.Hakuyokuwa na uuzwqji wa Bandari + maaliasili za Tanzania
 
Masuala ya muungano nchi yamewekwa katika ofisi ya makamu wa Rais ambapo pia kuna wizara na waziri anayeshughulikia muungano na mazingira.

Sijui kwa nini serikali wameweka muungano na mazingira kama jambo moja lakini kwa sababu kuna hii wizara tayari inabadi mawaziri wake wakishirikiana na makamu wa rais wajitokeze kuutetea kwa hoja mbele ya umma wa Tanzania ili kuifanya imara zaidi kama inawezekana.

Ilipaswa kabla Kinana hajajitokeza hadharani au hata baada ya yeye kujitokeza kumjibu Lissu basi makamu wa Rais Phillip Mpango akisaidiana na Waziri Jafo wajibu pia hoja za Lissu katika majukwa mbalimbali. Jambo la kushangaza mpaka sasa wote wako kimya na wanajibu watu wengine wa mbali kabisa!
Wale siyo size ya ya lisu. Lisu ni mdogo sana na size yake ni Happy na wasila na wameshamjibu tayari
 
Back
Top Bottom