Phillip Mpango sawa lakini Charles Kimei hapana, labda Mwigulu Nchemba

Phillip Mpango sawa lakini Charles Kimei hapana, labda Mwigulu Nchemba

Team JPM

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
1,197
Reaction score
1,826
Uteuzi wa Dkt. Philip Mpango unaweza kuwa na tafsiri nyingi, mojawapo ikiwa ni kutaka kumpenyeza Charles Kimei kuwa Waziri wa Fedha.

Mpango ni mchapakazi, mnyenyekevu na Mzalendo hivyo anafaa kwa nafasi hiyo ili kumsaidia mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Kama Mpango anamlisha Mkurugenzi mstaafu wa CRDB ambaye aliiongoza vyema Benki hiyo lakini kikawa ni kichaka cha utakatishaji, basi tuendako safari itazidi kuwa ndefu.

Mwigulu Nchemba atafaa zaidi Wizara ya Fedha maana anao uzoefu na weledi katika majukumu hayo kutokana na kufanya kazi Benki Kuu na kisha wizara ya Fedha wakati wa Serikali ya JK.
 
Kimei hawez wekwa pale hata sku1...mzee baba alimtoa pale na kumweka nsekela kwa sabab maalum....kwahyo sahau kuhusu kimei....hata huyo mwigulu hawez pewa asimamie pesa...hapo anahitajika mwenye hofu ya mungu na mwenye historia safi

Mkimweka kimei ni kina mramba walewale
 
Wizara ya Fedha iongozwe na Rais tu tujue moja maana hata wakati wa JPM Dr. Mpango alikuwepokuwepo.

Come to think of it, hii teuzi ya Mpango huenda kuna kitu kikubwa nyuma ya Pazia. Nadhani kwa Waziri wa Fedha tunaweza kuwekewa outsider (mtu kama Dorothy Gwajima) asiye na clue ili wamcontrol kwa remote
 
Back
Top Bottom