Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu

Philosophy of Religion: Uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa hoja ya Ufunuo na maandiko matakatifu

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Kuna hoja ya kuthibitisha uwepo wa Mungu, hoja ambayo imeegemea zaidi katika kutumia vitabu vya dini kama uthibitisho

Ni hoja ambayo ime base kwenye imani ya kusema Mungu amejidhihirisha uwepo wake kwa binadamu kupitia uumbaji au maandiko matakatifu.

Watu wamekua waki experience hayo maandishi kua yametoka moja kwa moja kwa mungu na kupitia experience hiyo wengi wanaamini kuwa wanawasiliana na Mungu directly.

Hiyo ni hoja ya kutoka kwenye ufunuo (argument from revelation) ambayo huusisha maandiko matakatifu (sacred text)

Kwamba
  • Imekuwa inspired na Mungu
  • Imeamuriwa na Mungu
  • Imeandikwa na kuongozwa na Mungu

Msingi wa hoja hii

  1. . Maandiko yanasema Mungu yupo (Quran, Biblia)
  2. . Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au watu walio ongozwa
  3. . Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu ndio alifanya hiyo kazi)
  4. . Mungu ndio chanzo na dhamana ya ukweli

HITIMISHO: Mungu yupo

**************
Hoja au uthibitisho wa namna hiyo haukubaliki na rational thinkers kwasababu una makando kando mengi (flaws) kuna matobo kibao kwenye hii raft ambayo umeitumia kujenga hoja yako

Tatizo la kwanza la hoja hii ni

LOGICAL PROBLEM OF FALLACY CIRCULAR ARGUMENT
Hii ni hoja ambayo inatumia assumption kwa kile inachotaka kuthibitisha na hii huchukuliwa kama moja ya hoja za kijinga na zenye udhaifu sana miongoni mwa hoja zinazojaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu

Ukiangalia hiyo misingi ya hoja hizi niliyoiweka hapo juu, namba 2 na namba 3 utaona zime contain hitimisho ndani yake

Hoja ilipaswa ikuongoze mpaka ikufikishe kwenye hitimisho na sio ku assume hitimisho ndani ya msingi wa hoja hiyo hiyo.

Kwasababu lazima ukubali kuwa kitabu hicho kimetoka kwa Mungu ili ukikubali kuwa ni cha kweli na sahihi kisha ukisha kikubali kuwa ni cha kweli na sahihi ukasoma ndani yake kuwa kuna Mungu na hivyo kuhitimisha kuwa kuna Mungu na huyo ndiye. Hicho ndicho ulichohitaji kufikiria ili kukubali kitabu hicho kuwa cha kweli na sahihi hapo awali.

Hii Circular Reasoning ya namna hii haiwezi kumshawishi rational ambaye yeye sio muumini wa Miungu/Mungu

ambulika kua ni maandiko ya kweli zaidi?
 
Tatizo lingine kwenye hoja hii ya revelation ni PSYCHOLOGICAL

leo kuna watu wengi wanaokataa kuamini kwamba maandiko ni maelezo sahihi ya matukio yaliyotokea zamani, watu wana uelewa wa psychological phenomen wa jinsi mtu anavyoweza kurudia stori na kuiongezea chumvi au kupotosha ukweli halisi wa kile kilichotokea

Kama ambavyo wewe unaamini biblia na vitabu vingine vya kale vya dini tofauti na yako vimepotoshwa kwa kuongezewa maneno ya uwongo

Hata hivyo kila kitu kina fahamika kwamba tyale yaliyochukuliwa kama maandiko matakatifu yalipigiwa kura na viongozi wa kiharakati za kidini. Yapo maandishi yaliyotengwa kwasababu fulani na mengine yakaongezwa na wale waliokuwa na uwezo wa kutangaza maandishi hayo kuwa yamevuviwa rasmi au kuandikwa na Mungu huyo.

Kutumia maneno ambayo yamekuwa yakichukuliwa kama "maandiko matakatifu" hayaelekei kuthibitisha kwa wasio amini kwamba ni matakatifu

Kutumia maandiko kumthibitishia aiye amini kwamba kuna sacred source ambayo ili inspire waandishi wa hayo maandiko haiwezi kuwa na ushawishi pale ambapo kuna maelezo ya mbadala yanayo elezea kilicho fanyika miaka hiyo.

TATIZO KATIKA UKWELI

Ni maandiko gani matakatifu yaliyo matakatifu zaidi kuliko mengine?

Ni toleo gani la maandiko ambalo tunapaswa kulitumia? Maandiko huripoti matukio ambayo hayawezi kuwa kweli na ambayo hayawezi kuthibitishwa na ambayo yanaweza kupotosha.

Kama hoja ya ufunuo inafikiriwa kuwa ni hoja ya kukubalika basi kuna haja ya kueleza kwanini andiko moja lipingane na andiko lingine wakati yote hudaiwa kuandikwa kwa ufunuo?

  • Mungu lazima awepo kwasababu maandiko yamesema (Biblia, Quran, Vedas, Avestas, etc.)
  • Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au kwa watu walio ongozwa
  • Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu aliwaongoza)

Kwa hiyo maandiko gani kati ya hayo ni matakatifu au ya kweli zaidi kuliko mengine: Biblia agano la kale, Biblia agano jipya, Quran, Vedas, Avestas?

Toleo gani kati ya hivyo vitabu vitakatifu ambacho kinapaswa kuwa rasmi na kutambulika kua ni maandiko ya kweli zaidi?
 
Masuala ya dini ukitumia logic na facts kuya chambua utaumia kichwa mana yamejengwa kwenye stori na sumilizi ambapo kwa ulimwengu wa sasa yamebaki kuwa historia tu isiyo na ithibitisho.

Ndio mana wafuasi na viongozi wa dini hizi hawanaga majibu ya maswali magumu wanaoshi kuwa wakali na kusema unakufuru..

Kiufupi ili uziamini hizi imani inakubidi we zezeta fulani hivi uliyejitoa akili ili uwe mwamini..tofauti na hapo ni mwendo wa kupewa matumani na vitisho.

#MaendeleoHayanaChama
 
Masuala ya dini ukitumia logic na facts kuya chambua utaumia kichwa mana yamejengwa kwenye stori na sumilizi ambapo kwa ulimwengu wa sasa yamebaki kuwa historia tu isiyo na ithibitisho.
Logic kama fani pweke haina uwezo wa kutambua mambo yaliyo fichikana kadhalika ukweli wa mambo jinsi ulivyo. Huu ndiyo ukweli misingi ya logic ina udhaifu mwingi sana.

Ama kuhusu facts, labda ututolee mfano sababu dini hasa Uislamu ndiyo facts yenyewe.

Mfano kama kipi hakina uthibitisho ?
Ndio mana wafuasi na viongozi wa dini hizi hawanaga majibu ya maswali magumu wanaoshi kuwa wakali na kusema unakufuru
Naomba utuwekee maswali mawili tu magumu.
Kiufupi ili uziamini hizi imani inakubidi we zezeta fulani hivi uliyejitoa akili ili uwe mwamini..tofauti na hapo ni mwendo wa kupewa matumani na vitisho.
Siyo kweli, mfano wangu mimi na wewe tupimane kwa akili na maarifa na namna ya kufikiri tuone nani zezeta. Tusiende mbali.
 
Msingi wa hoja hii

  1. . Maandiko yanasema Mungu yupo (Quran)
  2. . Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au watu walio ongozwa
  3. . Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu ndio alifanya hiyo kazi)
  4. . Mungu ndio chanzo na dhamana ya ukweli

HITIMISHO: Mungu yupo
Huu mtiririko umeusema wewe na umeulazimisha ufate mtiririko dhaifu wa logic.

Kwanza usilo lijua ni kuwa wakana Mungu walikuwepo hata kabla ya kina Plato, wakaendelea na Mtume wetu alikutana nao. Tofauti yenu na wale wenzenu wa mwanzo kuwa wenzenu walikuwa mabingwa wa lugha na kugoji pia. Nyinyi mpo kinyume.

Katika maswali waliyokuwa wanaulizwa wakana Mungu tangu na tangu ni yale yaliyopo katika sura ya 52 aya ya 34 mpaka ya 36. Hakuna mkana Mungu yoyote aliyewahi kujibu maswali yale akapatia.

Kwahiyo hapa umetuzushia sisi watu wa dini. Sisi huwa hatuhitimishi mambo kitoto namna hii.
 
Ukiangalia hiyo misingi ya hoja hizi niliyoiweka hapo juu, namba 2 na namba 3 utaona zime contain hitimisho ndani yake
Miongoni mwa vitu vilivyo nifanya niachane na elimu ya logic ni hiki ulicho kifanya wewe, elimu hii haikuelekezi kufanya utafiti na kufikiri nje ya akili, yaani kwa logic akili ndiyo kila kitu.

Hoja namba 2 na 3 imejumuisha zaidi ya hicho ulichokidai. Hoja mbili hizo kwanza zinakulazimisha umjue huyo Mola ni nani na hao walio ongozwa ni kina nani, walifanya nini na walikutana na changamoto gani na ilikuwaje wakafanikiwa ? Kwa wewe kutokujiuliza maswali haya kuna onyesha ni kwa namna gani una uwezo mdogo wa kufikiri na kuutafuta ukweli. Unachorukia wewe ni hitimisho pasi na kujiuliza ilikuwaje wakafikia hitimisho hilo ?

Sasa viwili hivyo vyote huvijui, halafu unakuja kutuwekea mada ambayo uchambuzi wake umemili katika uongo na ujinga pamoja na uzushi wa kutuandikia mambo ambayo sisi wahusika hatuko nayo.
Hoja ilipaswa ikuongoze mpaka ikufikishe kwenye hitimisho na sio ku assume hitimisho ndani ya msingi wa hoja hiyo hiyo
Hapo nitakuuliza assumptions ziko wapi ? Wakati kila kitu kipo wazi ila wewe sababu hujui unachokijadili umerukia hitimisho na kujua hitimisho limefikiwaje ?
Kwasababu lazima ukubali kuwa kitabu hicho kimetoka kwa Mungu ili ukikubali kuwa ni cha kweli na sahihi kisha ukisha kikubali kuwa ni cha kweli na sahihi ukasoma ndani yake kuwa kuna Mungu na hivyo kuhitimisha kuwa kuna Mungu na huyo ndiye. Hicho ndicho ulichohitaji kufikiria ili kukubali kitabu hicho kuwa cha kweli na sahihi hapo awali.
Hapa umeandika uongo wazi kabisa. Nitakuuliza sharti la kukubali kwanza kitabu kimetoka kwa Mungu ni kwako wewe unayepinga au kwa sisi tunao amini hivyo ? Kama kwa sisi tunao amini hivyo si kweli sababu huanza elimu kwanza kisha imani. Tumejifunza na kuamini na kadhalika ni katika umbile letu sisi wanadamu. Ama kwenu nyinyi mnao kataa hii pia si kweli, ndiyo maana ukisoma katika Qur'aan ina wa challange kwa kuwaambia leteni hoja zenu kama nyinyi mnasema ukweli. Yaani inawataka mjenge hoja na muonyeshe ukweli wa mnayo yadai.

Ukisoma kitabu hasa Qur'aan ina kuonyesha uwepo wa Mola kwa mifano, kuhoji na kutafakari.

Hapa nahutimisha ya kuwa, umechambua jambo ambalo hulikuti katika dini, na hapa utaona udhaifu wa logic, yaani unajadili jambo ambalo huna elimu nalo na unahitimisha kwa ujinga.
 
Swali lenye najiuliza kwa muda mrefu ni kwanini Mungu asingekuwa anatuumba tunajua kila kitu kuhusu yeye tunapokuja duniani sio mpaka tuanze kufundishwa kumjua.

Kama lengo la Mungu ni sisi wanadamu tumuabudu ni kwanini tusingekuwa tunazaliwa automatic tunamjua yeye maana kama lengo lake sisi tumuabudu
kwanini mpaka tufundishwe?

Kama Mungu ana dini yake moja anayotaka tuifuate kwanini mpaka leo hakuna dini iliyoweza kusambaa duniani kwote anae bisha ili aje na uthibitisho kama kuna dini moja yenye imefika kila sehemu hapa duniani.
 
2022-03-03-20-47-12.png
 
Naanzia hapa. Kwenye ule uzi nilikupa angalizo, kwamba usiweke mada ambayo huna elimu nayo.

Nakuuliza maswali kadhaa.

1. Uthman ameandika nini katika Qur'aan na Abubakr kaandika nini ? Ambatanisha na ushahidi.

2. Qur'aan ni nini ?
Baada ya waislam wengi walio ijua Quran kufa kwenye vita ya Yomama Central Arabia ,Abu Bakr alihofia Quran ingeweza kutoweka katika uso wa dunia, vinginevyo ifanyike jitihada ya kufanya kila linalowezekana kupata Quran nyingine mpya

Abu Bakr akampa hiyo project secretary na editor wa muhammad ambaye alikuwa akiitwa Zayd ibn Thabit kufanya kazi hii nzito.

Huyu Zayd ibn Thabit alikuwa na kibarua cha kutembea maporini kutafuta collection ya maandishi kwenye mapango, kwenye ubavu wa wanyama, kwenye mawe na hata kwenye upinde wa panga na mengine alikuwa akiyachukua kwa watu ambao walidaiwa uyaifadhi maandishi kwenye vifua vyao

Kwa hiyo hii Quran ambayo tuko nayo sasa ni Quran ambayo imekuja baada ya miaka mingi kupita tangu afe muhammad

Najua kuna modern muslim scholars hawataki kukubali ukweli huu ila Wanazuoni wa Kiislamu wa miaka ya nyuma ya Uislamu walikua huru sana, walitambua kua sehemu kubwa ya Quran haikupatikana na pia walijua kwamba kuna maelfu ya utofauti ambao ilifanya isiwezekane kuzungumzia Quran

Mfano kuna mwanazuoni wa miaka hiyo As-Suyuti moja ya watu maarufu na wenye heshima katika kutoa maoni kwenye Quran

Na moja ya quote yake maarufu alisema kua " Ibn asiseme kwamba amefanikisha kuipata Quran yote, ana juaje kwamba kaipata yote?" Kiasi kikubwa cha Quran kimepotea alipaswa kusema " nimefanikisha kupata kile ambacho kimeweza kupatikana"

Lakini pia Aisha mabye alikuwa mke wa Muhammad alishawahi kusema kipindi cha muhammad Quran ilikuwa na chapter 200 lakini tangu Uthman aedit zimekuwa chapter 73

Ni historia ndefu sana ambayo ipo katika series hapo nimefanya kufupisha tu ila wapo wengi sijawataja kama binti yake Umar anayeitwa Hafsa na wengine wengi
 
Huu mtiririko umeusema wewe na umeulazimisha ufate mtiririko dhaifu wa logic.

Kwanza usilo lijua ni kuwa wakana Mungu walikuwepo hata kabla ya kina Plato, wakaendelea na Mtume wetu alikutana nao. Tofauti yenu na wale wenzenu wa mwanzo kuwa wenzenu walikuwa mabingwa wa lugha na kugoji pia. Nyinyi mpo kinyume.

Katika maswali waliyokuwa wanaulizwa wakana Mungu tangu na tangu ni yale yaliyopo katika sura ya 52 aya ya 34 mpaka ya 36. Hakuna mkana Mungu yoyote aliyewahi kujibu maswali yale akapatia.

Kwahiyo hapa umetuzushia sisi watu wa dini. Sisi huwa hatuhitimishi mambo kitoto namna hii.
Kama nimekuzushia naomba twende taratibu wala tusibishane kitoto

Umependekeza hoja ya kutumia aya za kitabu

Hizo aya ndio kwanza naziona hapa

Ili kujihakikishia naomba unithibitishie ukweli wake ili niwe na uhakika kwamba na dili na source ya namna gani
 
🤔Watu wote duniani waamini kuwa hakuna MUNGU. Itakuwa dunia ya kishenzi tu. Bora hivi. Imani na ziendelee.
 
Miongoni mwa vitu vilivyo nifanya niachane na elimu ya logic ni hiki ulicho kifanya wewe, elimu hii haikuelekezi kufanya utafiti na kufikiri nje ya akili, yaani kwa logic akili ndiyo kila kitu.

Hoja namba 2 na 3 imejumuisha zaidi ya hicho ulichokidai. Hoja mbili hizo kwanza zinakulazimisha umjue huyo Mola ni nani na hao walio ongozwa ni kina nani, walifanya nini na walikutana na changamoto gani na ilikuwaje wakafanikiwa ? Kwa wewe kutokujiuliza maswali haya kuna onyesha ni kwa namna gani una uwezo mdogo wa kufikiri na kuutafuta ukweli. Unachorukia wewe ni hitimisho pasi na kujiuliza ilikuwaje wakafikia hitimisho hilo ?

Sasa viwili hivyo vyote huvijui, halafu unakuja kutuwekea mada ambayo uchambuzi wake umemili katika uongo na ujinga pamoja na uzushi wa kutuandikia mambo ambayo sisi wahusika hatuko nayo.

Hapo nitakuuliza assumptions ziko wapi ? Wakati kila kitu kipo wazi ila wewe sababu hujui unachokijadili umerukia hitimisho na kujua hitimisho limefikiwaje ?

Hapa umeandika uongo wazi kabisa. Nitakuuliza sharti la kukubali kwanza kitabu kimetoka kwa Mungu ni kwako wewe unayepinga au kwa sisi tunao amini hivyo ? Kama kwa sisi tunao amini hivyo si kweli sababu huanza elimu kwanza kisha imani. Tumejifunza na kuamini na kadhalika ni katika umbile letu sisi wanadamu. Ama kwenu nyinyi mnao kataa hii pia si kweli, ndiyo maana ukisoma katika Qur'aan ina wa challange kwa kuwaambia leteni hoja zenu kama nyinyi mnasema ukweli. Yaani inawataka mjenge hoja na muonyeshe ukweli wa mnayo yadai.

Ukisoma kitabu hasa Qur'aan ina kuonyesha uwepo wa Mola kwa mifano, kuhoji na kutafakari.

Hapa nahutimisha ya kuwa, umechambua jambo ambalo hulikuti katika dini, na hapa utaona udhaifu wa logic, yaani unajadili jambo ambalo huna elimu nalo na unahitimisha kwa ujinga.
Personal attacks za nini?

Bado naamini unaweza ukajenga hoja vizuri bila personal attacks

hoja 2&3 haina maelezo extra kama ambavyo wewe unadai, ili hoja iwe hivyo kama unavyosema ilipaswa iwe na lead na sio conclusion

Sasa hoja ina conclusion, na wewe ulichokielezea ni lead mpaka hapo unakuwa unaelezea kitu kingine tofauti na nilicho kizungumzia mimi
 
Baada ya waislam wengi walio ijua Quran kufa kwenye vita ya Yomama Central Arabia ,Abu Bakr alihofia Quran ingeweza kutoweka katika uso wa dunia, vinginevyo ifanyike jitihada ya kufanya kila linalowezekana kupata Quran nyingine mpya
Usiseme Qur'aan nyingine sema ikusanywe sehemu moja na iwe kitabu pweke sababu mpaka Mtume anafariki ilikuwa imeshakamilika. Rejea kitabu "Al-Itiqaan fi Ulumil al Qur'aan" cha Imam Suyuti.

Swahaba alihofia akaamuru hilo, ikusanywe na iwekwe kwenye kitabu. Siyo "Yomama" sahihi ni "Yamamah"

Abu Bakr akampa hiyo project secretary na editor wa muhammad ambaye alikuwa akiitwa Zayd ibn Thabit kufanya kazi hii nzito.

Huyu Zayd ibn Thabit alikuwa na kibarua cha kutembea maporini kutafuta collection ya maandishi kwenye mapango, kwenye ubavu wa wanyama, kwenye mawe na hata kwenye upinde wa panga na mengine alikuwa akiyachukua kwa watu ambao walidaiwa uyaifadhi maandishi kwenye vifua vyao
Huu uandishi wako una mapengo sana inaonekana ulienda kugoogle hivi punde, yaani hapo kabla hukusoma kabisa ndiyo maana unakosea sana. Kwanza walikuwepo wengi walio hifadhi Qur'aan nzima, iliandikwa kwenye makaratasi. Huko maporini ni mapori gani hayo aliyo enda Swahaba wakati ardhi ya huko ni Jangwa ?
Kwa hiyo hii Quran ambayo tuko nayo sasa ni Quran ambayo imekuja baada ya miaka mingi kupita tangu afe muhammad
Si kweli, inaonekana hujasoma mpaka mwisho huko ulipo soma. Nakuuliza wewe swali, swahaba Abuu Bakr alikamilisha hilo zoezi lini na alilianza lini ? Usiseme miaka mingi kupita.
Najua kuna modern muslim scholars hawataki kukubali ukweli huu ila Wanazuoni wa Kiislamu wa miaka ya nyuma ya Uislamu walikua huru sana, walitambua kua sehemu kubwa ya Quran haikupatikana na pia walijua kwamba kuna maelfu ya utofauti ambao ilifanya isiwezekane kuzungumzia Quran
Hili hakuna msomi wa dini anae pinga, swali la uongo ni hayo madai yako unayoyaleta kwamba sehemu kubwa haikupatikana, naomba ututhibitishie hili sababu kila kitu kimehifadhiwa. Yaani unavyo andika unaonekana huijui Historia ya ukisanywaji wa Qur'aan. Hapa itabidi ujibu maswali nayo kuuliza.

Hapo mwanzo nilikutahadharisha kwamba ukianzisha mada hakikisha unaiweza mada husika.

Yaani sisi mpaka kesho haya tunafundishwa na tunayajua ila hili la wewe kudai kwamba kuna sehemu kubwa haijapatikana ndiyo unatakiwa kuthibitisha.
Mfano kuna mwanazuoni wa miaka hiyo As-Suyuti moja ya watu maarufu na wenye heshima katika kutoa maoni kwenye Quran

Na moja ya quote yake maarufu alisema kua " Ibn asiseme kwamba amefanikisha kuipata Quran yote, ana juaje kwamba kaipata yote?" Kiasi kikubwa cha Quran kimepotea alipaswa kusema " nimefanikisha kupata kile ambacho kimeweza kupatikana"
Imamu Suyuti ni wanazuoni mkubwa sana na tunamkubali na kumuheshimu sana, haya maneno tunayapata wapi yaani kayasema wapi ?
Lakini pia Aisha mabye alikuwa mke wa Muhammad alishawahi kusema kipindi cha muhammad Quran ilikuwa na chapter 200 lakini tangu Uthman aedit zimekuwa chapter 73
Haya maneno umeyatoa wapi mbona unaandika kama habari za vijiweni ? Tuwekee matrejeo.
Ni historia ndefu sana ambayo ipo katika series hapo nimefanya kufupisha tu ila wapo wengi sijawataja kama binti yake Umar anayeitwa Hafsa na wengine wengi
Hii historia umeunga unga sana na inaonekana hujaisoma kutoka katika vyanzo vya asili. Cha kukusaidia tu kijana, tafuta vitabu vyenyewe usome, na laiti kama ungesoma usingeandika huu ujinga wa kuunga unga.

Nakusaidia tu, tafuta vitabu hivi uvisome kisha uje tujadiliane hii mada.

1. Al-'Itiqaan fi Ulumil al Qur'aan cha Imam Jalaludin Suyuti

2. Muqadimma fi Usul Tafsir cha Ibn Taymiyyah

3. Mandhumat al Zamzamiy

4. Hirzi al Aman wa Wajhu tahan cha Imam Shaatibiy akielezea viraa (Namna saba za usomaji)
 
Back
Top Bottom