Kuna hoja ya kuthibitisha uwepo wa Mungu, hoja ambayo imeegemea zaidi katika kutumia vitabu vya dini kama uthibitisho
Ni hoja ambayo ime base kwenye imani ya kusema Mungu amejidhihirisha uwepo wake kwa binadamu kupitia uumbaji au maandiko matakatifu.
Watu wamekua waki experience hayo maandishi kua yametoka moja kwa moja kwa mungu na kupitia experience hiyo wengi wanaamini kuwa wanawasiliana na Mungu directly.
Hiyo ni hoja ya kutoka kwenye ufunuo (argument from revelation) ambayo huusisha maandiko matakatifu (sacred text)
Kwamba
- Imekuwa inspired na Mungu
- Imeamuriwa na Mungu
- Imeandikwa na kuongozwa na Mungu
Msingi wa hoja hii
- . Maandiko yanasema Mungu yupo (Quran, Biblia)
- . Maandiko ni ya kweli kwasababu yameandikwa na Mungu au watu walio ongozwa
- . Nani aliwaongoza hao watu? (Mungu ndio alifanya hiyo kazi)
- . Mungu ndio chanzo na dhamana ya ukweli
HITIMISHO: Mungu yupo
**************
Hoja au uthibitisho wa namna hiyo haukubaliki na rational thinkers kwasababu una makando kando mengi (flaws) kuna matobo kibao kwenye hii raft ambayo umeitumia kujenga hoja yako
Tatizo la kwanza la hoja hii ni
LOGICAL PROBLEM OF FALLACY CIRCULAR ARGUMENT
Hii ni hoja ambayo inatumia assumption kwa kile inachotaka kuthibitisha na hii huchukuliwa kama moja ya hoja za kijinga na zenye udhaifu sana miongoni mwa hoja zinazojaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu
Ukiangalia hiyo misingi ya hoja hizi niliyoiweka hapo juu, namba 2 na namba 3 utaona zime contain hitimisho ndani yake
Hoja ilipaswa ikuongoze mpaka ikufikishe kwenye hitimisho na sio ku assume hitimisho ndani ya msingi wa hoja hiyo hiyo.
Kwasababu lazima ukubali kuwa kitabu hicho kimetoka kwa Mungu ili ukikubali kuwa ni cha kweli na sahihi kisha ukisha kikubali kuwa ni cha kweli na sahihi ukasoma ndani yake kuwa kuna Mungu na hivyo kuhitimisha kuwa kuna Mungu na huyo ndiye. Hicho ndicho ulichohitaji kufikiria ili kukubali kitabu hicho kuwa cha kweli na sahihi hapo awali.
Hii Circular Reasoning ya namna hii haiwezi kumshawishi rational ambaye yeye sio muumini wa Miungu/Mungu
ambulika kua ni maandiko ya kweli zaidi?
0_0
...
‘Dini ya Mtu Mweusi’ ni sehemu ya uono wa Marcus Garvey na wanamapinduzi ya kijamii wa kipindi chake cha uamsho; kwa kule kufikiri mtu mweusi hana budi ‘kumuona’ Mungu kwa jicho la mtu mweusi. Kwamba, RasTafari ni ‘Utwaaji Mwili Upya’ wa Mkombozi, Mungu katika Mtu, aliyekuja kufahamika kama Haile Selassie I, mara baada ya kupokea majukumu ya Utawala. Jambo hili, >
Mtawala Haile Selassie alilikanusha; na wakati mmoja (1967) alifanya hivi wazi wazi katika mahojiano yake kwenye luninga<… jambo ambalo linatubariki kuibaini ile adha ya Binadamu kutamani ukaribu na Mungu, hata kwa sura yoyote anayoweza kupendezwa nayo.
Kuna namna ya kuona, Urastafari, upo katikati ya ‘Ugarvey’ na ‘Uyuda’ na ‘Ukristo’. Sehemu ya huu ni
-'upinga mifumo',
-'ufuatishaji wa Imani za mambo ya dini ya Kiyahudi kama inavyodhihirishwa katika vitabu vya agano la kale la Biblia', na
- 'kiu ya ukombozi kupitia >'
nia ya Kristu'.<'
Sehemu ya upinga mifumo ndiyo tunda lake la ‘>
utamaduni-kinzanifu<’(vile wafikirifu wa kisosholojia, wenye kuzungumza kwa lugha ya kiingereza, wangelitaja kwa minajili ya >‘
counter-culture’< ama muktadha wa kupelekea maana ya kusema: ‘>
Rasta and resistance<’); uasi wa desturi katika mifumo ya kiukandamizaji na unyonyaji; hili ni sawa na ile picha ya Umarxi ulivyochochea, miongoni mwa wengi duniani, hisia za kuupinga ubepari—kwamba ubebapari ni unyonyaji--wanaotumikishwa 'wakijitambua' na halafu wakajiunga, wanaweza kujenga mshikamano kwa jitihada za uasi ama hata mapinduzi… Kwamba >
mtu yeyote mwenye kustawi katika mifumo ya kiunyonyaji ni mwenye kuipa nguvu hiyo<; hivyo na yeye ni ‘mtumwa’ ndani ya hiyo kwa kule kufuatisha mkumbo ama kuruhusu hiyo ‘imtawale’.
Basi yaja kuwa, ‘>
Mtu-Rasta<’ ni ‘>
mtu muasi<’—itikadi yake kisiasa ingalikuwa ni ‘>
mapinduzi<’; lakini wanaouishi Urastafari hujiepusha pia na ‘siasa’, ‘utengeneaji’ na ‘miundo’ kwa kuwa hivi vyote huonekana ni >
‘nguzo’ za ‘mifumo’<—na mifumo yote kufunga watu kwa ‘sheria au mila na desturi’—kufanya wachache wawatawale wengi… Mtu-Rasta, ni >
mpambanaji kwa uhuru na liberiti<, awe kama anavyopenda kuishi na kudhihirisha >
utamaduni wake juu ya jamvi la nyakati<…
Hebu tuzione maana kwa ufafanuzi wa mambo yake na alama oanifu za utamaduni wa mtu-rasta.
Mtu-Rasta ni mtu mtamaduni, na katika mila na desturi za jamii yake, vinasaba vya miundo ya jamii yake, katika muktadha wa Maisha ya ndoa yeye ajibayanisha kuwa ni mtu wa kaya ya baba, mama na watoto. Katika kaya ya Mtu-Rasta, mtu mume ni ‘Mfalme’ na mtu mke ni ‘Malkia’, na basi kila mfalme hana budi kumuona malkia wake kwa ‘jicho la nidhamu ya kimapenzi makuu’ na heshima, kama vile malkia impasavyo kumheshimu na mfalme wake kwa mapenzi ya kujitoa moyo. Lakini wote, baba, mama na uzao hujitanabaisha, kwa lugha ya Kiingereza sawia/Kijamaika, ni ‘JAH Children’—I-dren of the Most High…
JAH, ni kifupi kwa neno ‘Jehova’—'jina la Mungu aliye Juu’ kwa mujibu wa dini ya Kiyahudi; na hii ni sehemu ya utamaduni wa mtu-rasta ulio ni matokeo ya kujinasibu na Uyuda; yale mapokeo ya kuanzia kwa ‘Baba wa Taifa la Israeli’—Abraham, na kisha mbele ya wakati, kiongozi wa mapokeo na utaasisho wa mila, desturi na utamaduni wa muunganiko wa makabila kumi na mawili (12) ya Israeli—Musa. Haya yote yakitangulia kuzaliwa kwa ‘Masiha’ aliyekataliwa na Wayahudi, Yesu, mwana wa Maria na Yosefu.
Kwa hivyo mtu-Rasta katika Urastafari, kwa namna ya sura fulani, huzingatia sana mapokeo ya Musa na Utaasisho wake wa Taifa la Israeli na kumuona Mtawala Haile Selassie mahala pa ‘Masiha’. >
Marcus Garvey mwenyewe jina lake kwa ubatizo, kutokana na wazazi wake, lilikuwa ni Mosiah Garvey<, ambapo asili ya Mosiah ni Jina la ‘Musa’—nusu ‘Moses’, nusu ‘Masiha’. Musa kwa Kiswahili chetu, ni mtohoho kutoka kwenye ile tafsiri ya kichachu ya Kiarabu kwa jina lenye mzizi ule ule kwa dhana na tafsiri ya neno ‘Mashaikh’ kwa Kiebrania(lugha ya asili ya Waisraeli)—>
‘muopoaji’ ama ‘mtwaaji’, kumaanisha jambo kama vile Musa husemwa( kutoka katika moja ya vitabu vya agano la kale) aliopolewa kutoka kwenye chombo kilichokuwa kikielea kwenye maji na basi akapewa jina hilo na mwanafamilia ya kifarao wa misri< aliyekuwa akistarehe kwenye ufukwe wa mto Naili--je, basi ni la Kiebrania hasa, ama sivyo?
Ni muhimu sana kwa jamii wa Waafrika, kadri itafutavyo ‘Sura ya Utambulisho Wake’ iwe na maarifa sahihi na ya kutosha juu ya mambo ya kijamii --juu ya ufungamano wa kiutamaduni, ama sivyo >
‘ubeberu wa kiutamaduni’< utawaandama ‘isivyo bahati njema’ ule umma wa watu wake.
Utamaduni mmoja unaweza kumezwa na mwingine kwa kuwa tu ‘ufunguo wa ufunuo’ umepotea na basi jamii moja ikatawaliwa na nyingine kwa ‘hiari ya mlango wa nyuma’… Ndilo hasa linaweza kufanya watu taifa moja ‘kujiona si bora kuliko wengine’ kwa kuwa tu hao wana ‘utamaduni’ ama ‘ustaarabu’ wenye kupendeza machoni, wenye koherensia na mambo yake juu ya nyumba, makundi ya kaya, jamii, taifa, udugu, visomo, nidhamu na maadili… Kimsingi hivi ni sehemu ya jamii yoyote, lakini kwa wakati, jamii moja inaweza kuwa imekwisha nufaika mbali kuzidi nyingine kiuchumi na tawala; basi ikikutana na nyingine ’iliyo nyuma’ basi itakuwa na ‘ushawishi’ kwa mabadiliko—hasi ama chanya.
Hata mfumo wa elimu unaweza kupotoshwa kwa kule kuufananisha huo na jambo la ‘Ufunguo wa Ufunuo’; na kumbe huo bado ni ‘galasha’ la ‘mchezo’. Ufunuo ni muktadha wa ‘Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni Metafizikia ya Elimu’, ambapo ‘Elimu 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo’ ni kiungo kati yake na ‘Elimu 1.0: Kujua Kusoma na Kuandika’.
Haya yatukumbushe busara ya Mtawala Haile Selassie, maendeleo yetu hapa barani Afrika hayana budi kuwa ni ya vitu na watu; tukipuuza kimoja daima tutajikuta ni mateka wa staarabu kutoka nje; ambazo zitazotibua hata jitihada zetu za kuitafuta ‘kweli na neema ya utu wetu’ kwenye mazingira yetu.
Tukipuuza maarifa ya kiroho basi tunaweza kuyumbishwa na ile tamaa ya mapenzi ya mali na ulafi wa kimagharibi… Tukipuuza maarifa ya vitu, sayansi na uhandisi, basi tunaweza kunasibika na ‘siasa za wivu’ ama ‘jicho la husda’ kwa wengine wenye kuishi Maisha ya mali na ‘pepo ya duniani’… Tunaweza hata kupotoka na >‘akili ya kimaskini’< inayoweza kujengekea ‘akilini na mioyoni’ mwetu kutokana na mapokeo ya dini na Imani za mataifa mengine – kwa kule ‘kujihesabia haki’ katika maisha mengine yenye kudhanika ama kusadikika kuwepo mbali na dunia hii. Hili linaweza hata kutumika dhidi yetu, kiuchumi na tawala, kimfananishano wa faida za mambo na mipango – sisi wabantu tuna msemo, ‘Ukisusa, wenzio twala’…
Ni vema tuwe na hekima ya kutangamanisha mambo ya dunia na mambo ya kiroho, lakini pia tuchunguze akili na mioyo yetu wakati wote, pasi kusahau ukweli wa kwamba kila mtu kazaliwa pekee yake kabisa… na atakufa pekee yake kabisa. Yote ya ubinadamu fikra, usadikifu, uono, taasisi, mifumo na utamaduni ni mambo ya ‘wepesi’ kimaisha ya mafungamano, lakini si lazima yawe ndiyo ‘ukweli’ wa jambo juu ya uzima wote.
‘Ukweli Hasa’, daima na milele, ni jambo la ‘kuiva kwa tunda la imani katika hakika’-- ile ya mtu mmoja mmoja… Ni ‘ufunuo kamili’ katika mtu isivyokutegemea la kusikia, kuambiwa, na wala kuandikwa popote; ila basi mtu mwenyewe kufanyika ‘moja’ na ‘kweli’ yenyewe…
Kila mtu ni vema atafute ‘Kweli’ imfaaye yeye kama mtu, juu ya uzima wake na hata kupitilizia mbali ya mauti yake, huku azingatia kwamba: ikiwa ‘njia yake ya kuitafuta kweli’ inalandana na mwenzake—‘basi kheri’, ikiwa ni tofauti -- nayo pia ‘kheri’; labda kuna namna mbele ya safari njia zote huishia ‘kumoja’ -- labda ni adha ya Elimu 1.0; mtu akiwa Elimu 2.0 huanza kubaini ‘alama oanifu’ kwa ‘wasafiri’ wote – almradi tu hao kuwa kwamba ‘wameongozeka vema’ katika ‘nia na mapenzi mema juu ya wanadamu, dunia na kile ‘Kilicho ni Hasa’’?… Basi ni vema kila mtu kuwa na ‘akiba ya maneno’, kutoingiliana wala kusakamana, basi tuwe na kuheshimiana, kujaliana na Imani juu yale yote yanabeba makusudi ya upamoja wetu, kwa mfano, misingi ya nchi-taifa—kama ‘Mwanzo’…
Basi tutazame ya Urastafari kama ‘Mapito ya Safari’ lakini si kufika. Kwenye Urastafari hili lafahamika kama ‘Exodus’—'safari ya Kutoka’, Bob Marley aliimba hili kama >
‘Exodus, Movement of JAH People’ — JAH tutumie ndugu Musa mwingine<. Kwamba ‘Kutoka’, ni kuachana Babiloni na Kuelekea nchi ya ‘Baba’—kuvuka Bahari ya Shamu ilivyo ni metafo kwa hichi ‘Kipindi cha Majaribu Makuu ya Mataifa’. Dhima nyingine ya jambo hili ndiyo aliimba ‘>
Zion Train—Get on Board—Garimoshi la Sayuni—Pita Ndani’<, akihoji kana kwamba je, ni nani awezaye kumuokoa mwingine kama si kwakuithibiti nafsi yake yeye mwenyewe? Kwamba, Hekima ni bora kuliko vipande vya fedha na dhahabu, mtu asijekupata yote ya dunia lakini akaipoteza nafsi-roho yake… Aingie katika garimoshi la sayuni ili aelekeee Sayuni—Garimoshi Sayuni, ni nafsi-roho(Sonafi) ya mtu…
JAH na Sayuni ni viwili vya >
mfumo metafizikia na ontolojia< ya Stawi ya Mtu-Rasta. Sayuni ni alama metafo kwa ‘Upeo wa Wajuu wa Uono’ ambavyo watu, jamii na makabila daima yamekuwa na kule kuona >
‘Miungu yao hukaa pahala pa juu kabisa’< na kutawala mambo yao. Bob Marley analiimba hili, kwa mfano, katika wimbo >
‘Jamming’—Jamming in the name of the Lord, JAH sitteth at mount Zion, and rules all creation—Twarukaruka kwa furaha kwa jina lake Bwana, JAH aketi mlima Sayuni na kutawala Uumbaji wote<. Kama ilivyo ada, hili pia ni kutokea kwenye mapokeo ya >
kisayuni<, Uyuda.
‘Upeo wa Wajuu wa Uono’ ndiyo vile vile huingiliana na metafo ya ‘baba’; tumaini la vizazi vya Uyuda, kama >
inavyoimbwa katika Zaburi ya Daudi<, ni katika kutazama juu ya Ngome ya Mfalme; Simba wa Yuda iliyoko juu ya mlima Sayuni. Mji wa Daudi, Yerusalem (Mji salama kwa Kumuabudu Mungu wa Taifa la Israeli), si tu ni alama ya utaifa la Usayuni lakini pia kimapokea ndiyo 'lulu' ya Taifa la Israeli; inakuwa kwamba >
roho ya uhai wa taifa ni katika 'Mungu' ambaye taifa ama 'watu wake huinua macho yao kutazama juu'<...
Ndivyo basi, Urastafari huwa na alama ya utaifa iliyo ni bendera ya 'Simba wa Yuda' na pia, kuienzi ile alama ya >
'Nyota ya Daudi'<--pembe tatu zenye kuingiliana, moja ikielekea juu na nyingine ikielekea chini. Pia kujinasibu na makabila kumi na mwili ya Israeli, kama vile lile 'dhehebu' la 'Wanamakabila 12' (Vile vile kuwa kama ilivyo kwa >
alama 12 za zodiaki<) katika >
'Nyuma za Watu-Rasta'<--mengine yakiwemo 'Bobo Ashanti' na 'Nyahbinghi'.
'Nyota ya Daudi' ni moja ya >
alama za kipekee sana katika jamii za wanadamu<; ni alama ya 'nguvu' kwa metafizikia ya mambo dhahiri, na yale yasiyodhahiri, hii imefahamika kwa watu nyuma sana ya wakati, inafahamika leo na itakuja kufahamika hata kesho -- ikiwa kokote katika hizo zama ama epoki ya mwanadamu 'ukongorofu' wa mifumo umejili na 'kusahaulika kwa muda'.
Hili si hapa tu duniani, hata Sayarini kungine ambako kuna watu kama sisi wakiishi na kuandamwa na sura za kijamii, hadhi na tabia zinazofanana na za hapa duniani…
Hebu tuliangazie jambo la ‘Mungu’ na ‘Taifa’—JAH na Taifa-Urastafari; Urastafari huweka Imani kwa ‘JAH’—mtu-Rasta ni Mtu-wa-JAH, ‘JAH -man’… Dhana ya ‘JAH’ kwa mtu-Rasta, ni kuwa JAH ni ‘Kiongoza’. HIvyo mtu-Rasta ni mtu wa 'unyoofu'—ni mtu wa kutafuta ‘Baraka’ za JAH katika mapito yake. Haya ndiyo hufanya muktadha kwa ‘JAH Guide’, ‘JAH Bless’ na ‘Righteousness’—katika lugha ya kiingereza, itumikavyo na mtu-Rasta.
Taifa-Urastafari, hujinasibu na ‘Jaala’ ya ‘umoja chini ya ulinzi wa JAH’; Jamii ya mtu-Rasta hujinasibu na ‘utaifa-moja-kuendea’, hutajwa kama ‘Dest-I-nation… 'Exodus-Kutoka' ni kutekeleza ujio wa ‘Des-I-nation’. Neno la kiingereza ‘Destiny’ kwa Kiswahili ni ‘Jaala’—alichokipanga Mungu juu ya mtu, nchi ama hata mbingu. Majaaliwa ya mtu, nchi ama hata mbingu, kwa mtu wa Imani, hatima yake iko mikononi mwa Mungu -- na chochote kikingine cha ‘Mapenzi ama Nia’ ya mtu/mwanadamu—kwa maneno, matendo, tabia na mwenendo, ‘hutoa hesabu’ kwa Mungu’. Hichi ndicho Mtawala Haile Selassie ilichokuwa akimaanisha juu ya metafo ya ‘the Most High’—Aliye Juu Hasa, ‘Mungu’.
Kwa mtu aliyeongozwa vema, mtafuta kheri katika njia zaYe, kiasi chochote cha maarifa yake huiva na kuwa ni chachu ya hekima na busara; ndivyo basi hili ‘hufanya utashi’ katika mtu. Utashi ni kuinuliwa juu hata kuishinda ‘jaala’, kwa kuwa yuleyule anayekujalia, ndiye aweza kukupa kingine mbadala ama hata kingine cha zaida… Vile vile hili lalandani na ule usemi wetu wa Wabantu, aliyekupa wewe, ndiye aliyeninyima mimi; aliyewapa wao ndiye aliyetunyima sisi; na kinyume chake--kwa nini tuchukiane ama kuwekeana wivu? Na hapa ndipo Elimu 1.0 huwa haina msaada…
Elimu 2.0: Uono na Ufikirifu mifumo, ndiyo nasibu ya mtu yeyote wa Imani; yeye akiwa na usafi wa moyo na nia njema kweli kweli, ‘maarifa ya namna nyingine’ huanza kufanyika juu ya hili katika yeye. Kuna masuala katika maisha ya mwanadamu, adha zake haziwezi kutatuliwa kwa 'visa ama visasi' bali kwa watu 'kuinua macho yao juu' kwa kusudi la kutafuta 'kujua ilivyobora' kwa karama zaYe katika sisi.
Kwa mtu wa uono na ufikirifu mifumo, ‘Wakati’ kuingiliana na ‘Mpango wa Mungu’; namna mojawapo yaweza kuwa huu ukweli wa kwamba ‘malipo ni hapa hapa duniani’. Matukio yote tuyasabibishayo duniani sisi kama watu, kwa muktadha na nia na mapenzi yetu katika vitendo; kwa vile visa na hata mikasa, hujisawazisha kwa mema ama mabaya juu ya mtu, kaya, ukoo, taifa, ‘malaika’ na hata ‘miungu’ pahala fulani hapa hapa ama hata kungine…
Na 'wakati' basi, labda huu si kipimo cha kinachotoka nyuma Kwenda mbele, kufikiri namna hii ni ukosefu wa 'vina vya tafsiri'; kwa 'ukweli hasa' wa jambo. Wakati ni ‘siri’—katika hii, ukweli wa sonafi ya mtu umejificha katika ‘mioyo’ ya watu—Mungu yuko ndani ya mtu, lakini mtu anazinguliwa na Elimu 1.0; kusadiki chochote na vyovyote atakavyo ama kupenda; yeyote anayeishi kukosea, ataishi kujisahihisha, wakati mmoja ama mwingine, mahala hapa ama kule. Kwa kuwa, katika roho ya Mungu, iliyo ni Mungu, hili ‘siyo siri’… Sonafi ya mtu ina ‘ufunguo’ kwa >
'mwangaza'< ama ufunuo, na hii sonafi ni 'mzizi wa mizizi' katika 'nyakati zote'; kila mtu anasehemu katika yeye imeishi siku za zamani, >
inaishi leo< na itaishi kesho, >
sisi sote ni watu mistikali<, basi hakuna mtu ni mgeni hasa wa mambo ya hapa duniani—>
Je, mtu apata ujumbe<?
Hili latuleta kwenye ile picha ya Mtu-Rasta kupenda kujitambulisha kama I-Man, na kuzungumza ya matazamo wate kwa kujirejea kama I’n’I; ‘I’ kwa Kiswahili ni nafsi ya kwanza ya kauli kumaanishi ‘Ndimi’. Lakini ‘I’ ni alama… Uwima wa herufi ‘I’ ni alama ya uthabiti; nia na dhamira ya mtu Rasta ni kuwa thabiti kwa Imani katika kuyaishi Maisha ya Urastafari. Haya, kwa mtu-Rasta azungumzaye kiingereza huita ‘livity’—>
Rasta Livity<…
Pia, Liviti-Rasta ama pia tuuite 'Uisho' hubayanishwa na mtu-Rasta azungumzaye lugha ya Kiingereza kama >
'Conscious Livication'<--yale maisha ya kuwa macho kiakili, tabia na mwenendo... Hii ni kwa kuwa JAH ni mwenyekuishi kote, katika vyote na mote, Ndimi ya kwanza katika I'n'I ni ya Mtu-Rasta kama 'mtu' na ya pili ni 'JAH' katika yeye. Kwa hivyo I'n'I ni 'I in I; Lakini Mtu-Rasta humaanisha I'n'I kuwa ni Ndimi na Ndimi--yaani 'pamoja', pale arejeapo lolote lenye kuwakilisha 'watu wa imani'--'I and I'; basi yawa JAH yuko kwangu kama alivyo ndani yako na alivyo katika sisi sote... Hivi ndivyo katika wimbo wa >
'Give Thanks and Praises'<, Bob Marley aliimba juu ya udugu katika Imani...
Give Thanks and Praises--'Toa Shukrani na Kutukuza', Jambo hili ni 'sala' ya namna ya kuishi katika hali ya neema' kwa mtu-Rasta. Hapa ndipo ile alama ya Nyota ya Daudi inahusika...
Shukrani na Kutukuza, kwa mtu wa uono na ufikirifu mifumo ni uisho unaomkadirisha mtu na ile 'neema ya uzima'; kwamba mtu anaishi na kustawi katikati ya 'vinavyoonekana' na 'visivyoonekana'. Chini ni kwenye vinavyoonekana na Juu ni kwenye visivyoonekana... Hivi vinavyoonekana ndivyo hutajwa kama 'nchi' na visivyoonekana 'mbingu'. Katika nyota ya Daudi, pembetatu ya chini inawakilisha 'nchi' na ya juu inawakilisha 'mbingu'...
Mtu anayeishi kushukuru na kutukuza inapelekea maana ya kwamba shukrani zake huelekea ardhini—aliposimama kuwa ‘patakatifu’, na kutukuza kwake kwa fanania na tendo la kunyanyua mikono juu kana vile 'kupokea neema' ama kujazwa na 'pumzi ya roho takatifu' ya uzima wote. Neema Itokayo juu kuja chini--pia kuinua macho juu kwenye Jua, iliko ni asili ya >
mzizi wa mizizi< ya sonafi katika mtu.... lakini kiuono mfumo hili ni jambo la sayansi ya maumbo na metafizikia yake...
Kupitia fikizia ya maumbo na uono mifumo, 'Mbingu' ndiyo iletayo dhana ya 'Bwana' kwa mataifa; na pembetatu yeyote inaweza kukadirisha muktadha wa 'nchi', 'jua' na 'mbinguni'. Ambavyo inalandana na uono wa ung'amuzi kwa, Utatu Mtakatifu -- Baba, Mwana na Roho; Vitu vyote vilivyodhahiri na visivyodhahiri vimefanyika katika Roho ya Uzima wote, japo vikiwa dhahiri kuna 'mbingu' na 'nchi'. >
Uzima< katika 'unafasi, maada, nishati na wakati' hujitukiza kwa 'chembe tufe' kubwa na ndogo--moto na baridi...
Haya kuwa namna ya miili ya mbinguni, sayari na nyota, makundi ya nyota na vitovu vya falaki-->
kimoja kikizunguka kingine bila kukoma<...
Katika sayari ndivyo ambavyo 'nia na mapenzi ya kiumbe' chochote , kwa asili, vinasaba, mwili na uhai -- huwa na asili-jua (>
sonafi--mwili usiyoharibika<), ambavyo mwili wake ndiyo huwa na asili-nchi(udongo), yaani sayari(mwili wenye kuharibika). Na basi sayari yoyote yenye kukirimu viumbe, iwe dunia ndani ya mfumo wetu wa jua ama mfumo mwingine wa jua, nayo ni >
'kiumbe hai kabisa'<; na ni mama wa vyote vilivyomo ndani ama nje ya uso wa utufe wake yabisi(ardhi), wa hewa, wa maji na usumaku....
Kwa uono na ufikirifu mifumo, 'Nia' ndiyo "mhimili wa imani" kati ya ‘asili ya kiumbe sentienti’ na yale yote mambo yasiyodhahiri na tena katika mapana ya utambuzi wa mazingira yake. Ndivyo katika wimbo wa >
'Give Thanks and Praises'<, upendo wa JAH ni neema na baraka imfanyayo mtu kuwa vile anavyokuwa katika 'Wema'. HIli kwenye jamii ya mtu-Rasta ndilo hutajwa kama >
‘JAH Love’<.
Kupitia ‘JAH Love’ ndiyo katika wimbo wa >
Rastaman Vibration< ‘nguvu tetemo' za Mtu-Rasta husemwa ni ‘Chanya’… Maudhui ya kuasa na kusihi ya kwamba maisha ya mtu yawe ni ya kujiepusha na ‘nguvu tetemo hasi’, kama vile hulka za magomvi, chuki na uhasama. Hapa, kwa mtu wa uono na ufikirifu mifumo, topografu moja ya muktadha huu wa uono yawa dhahiri na kushahibiana na ingine ya kuona ambavyo ‘nia ya mtu’ yajengewa ‘fanusi mwangaza’ wa kule kutafuta kuinuka ama kuinulia. Kwamba, 'Pendo JAH' ni uweza katika kamnasibu mtu na kuinuliwa(kuwa ‘Iya-man’); kwa kule mtu kulipata ‘daraja la kiroho’ katika ‘fahamu na upeo’ ushindao migogoro ama migongano katika maisha yake ya kila siku.
Kwa seti ingine ya topografia ya muktadha wa uono wa jambo, kwa namna hii hii, ndiyo pia na inashahibiana na jinsi >
‘natharia migongano’< kwenye visomo sosholojia yaweza kubaini migongano kama adha za kutolandana kwa nia, vitendo na ushawishi wa taasisi moja hata ingine, ndani ya Taasisi. Tena vivyo hivyo, mtu mmoja hata mwingine, jamii moja hata ingine lakini kumbe kigezo cha haya yote ni mizania ya ‘kujisikia’ na ‘vina vya tafsiri’; katika ‘kiumbe husika’, iwe kama kwa sura ya mtu, jamii, taifa n.k… Kifanusi jamii, watu hukaa pamoja, kujiunda kijamii, kwa kuwa hawa ni wenye kushiriki hisia za raha ama furaha, na hapo hapo ni wenye kutafuta kujiepusha na machungu na huzuni yenye kuandama ‘visa ama/na mikasa’ kwa maisha yao na mazingira yao.
Mtu-Rasta, katika Pendo JAH, ni mtu wa kutafuta ‘utangamano’; hamonia kwa ‘nguvu tetemo’ za vitu, mambo, matukio, kaya na wakati. Kwa kiuono na ufikirifu mfumo, hii yaleta picha ya kukidhi sura, muktadha na kina cha tafsiri kuwa: kila kitu, jambo, tukio, muktadha wa jamii na wakati ni ‘ufungamana nguvu sawa’ wa tetemo za:-
- nia ya kimoja kujikataa na mapenzi ya JAH,
- nia ya Kimoja kujikabidhi kwa mapenzi ya JAH, na
- Mapenzi ya JAH.
Kiuono na Ufikirifu mifumo, Mapenzi ya JAH—Pendo JAH, ndiyo ‘zingara’ la ‘ulinzi’ --ulinzi kwa mtu Rasta, hii ni kupitia muktadha wa utu ama sentienti ya kiumbe kulingana na dhamira zinazoweza kuhitilafiana, kati ya kiumbe na kiumbe, juu ya muongozo wa matendo yao na tabia kwa ujumla. Vivyo hivyo, kujali na kuheshimiana ni ufunguo wa ‘tunu za utu’ ama ‘sentienti’ ambavyo ni kuona kana kwamba: mtu mwingine pia ni wewe katika mwili mwingine, kiumbe kingine pia ni wewe katika kiumbe kingine… Ndivyo basi, muktadha wa kuheshimu hoja ama fikra za mwingine katika jamii ya mtu-Rasta hutajwa kama ‘ras-pect’, kutokana na kujumuisha neno ‘Rasta’ na neno ‘Respect’—heshima.
Kwenye jamii ya mtu-Rasta, ‘Reasoning and Overstanding—Ujengaji hoja na Kusimamia ile ya Juu’ ndiyo daraja muhimu la kuhakikisha kunakuwa na ‘Umoja’ na ‘Amani’ katika taifa la Urastafari. Hili pia ndiyo ule muitikio wa fikra za busara za Mtawala Haile Selassie I juu ya ‘nguvu ya hoja’ badala ya ‘hoja ya nguvu’. Vile Bob Marley alivyopata kuimba kwenye >
‘One Drop’<: ‘
Give us the Teachings of his Majesty ‘cause we don’t want no devil philosophy —tupe mafundisho ya Mtukufu(Selassie I), kwa kuwa hatuitaki falsafa ibilisi yoyote…’
Falsafa Ibilisi… Kiuono na ufikirifu mifumo, ‘falsafa ibilisi’ ni istilahi >
‘ya kifanusi, fanusi jamii’<-- kwa mapelekeo ya kimetafo kwa ‘fanusi Ibilisi’; hii, kwa mujibu wa ile namna ya uono wa ‘ufungamano-nguvu-sawa’ (vile wenye kuzungumza katika lugha ya kiingereza wangalisema kana ‘Equilibrium of Forces within the Entire Creation’) wa ‘nguvu tetemo’ katika ususiko na ufumivo wa mambo; chochote ambacho chavuta chini nia ya mtu ama sentienti(hadhi ya kiumbe kuwa na kule kujitambua), ni matokeo ya fanusi Ibilisi. Kitu chochote ambacho chamfunga mtu na kule kuamini, sadiki, ufikirifu, mapokeo ya kitaasisi na kumfanya yeye ‘ajikatae’—asinasibike kufahamu kuwa yeye aweza kuinuka katika ‘Pendo Moja’, ilivyo ni neema ya ‘Kweli hasa’ na ‘Uzima’ wa yote—ni falsafa Ibilisi… Basi kinyume chake ni ‘fanusi Malaika’. Fanusi Malaika ni ile namna yeyote inayofanyika katika mtu na kumfanya yeye anasibike kuinuka katika ‘Pendo’ na ‘kujua ilivyobora’…
Kiuono na Ufikirifu mifumo, ‘Pendo Moja’ ni tunu ya utaifa ya watu kukaa pamoja na kujisikia sawasawa juu ya furaha yao, mambo yao na mustakabli wao. Bob Marley aliliimba hili katika wimbo ‘One Love—Pendo Moja’: One Love, One Heart… Lets Get Together and Feel Alright… Give Thanks and Praises to the Lord…-- Pendo Moja, Moyo Moja… Tuje Pamoja na Kujisikia sawasawa… Tutoe Shukrani na Kusifu Sifa zaYe Bwana…
Kujisikia huku furaha na moyo mkuu, kwa mtu-Rasta (Iya-man — Mtu-Aliyeinuliwa-Juu) hutajwa kama ‘Irie’(Irie I); Kujisikia ‘Irie’—Aire, Ni muktadha wa ‘nguvu tetemo’ za mtu rasta kusemwa ni ‘chanya’… Kiuno na ufikirifu mifumo, kutoa shukrani na Kusifu sifa zaYe Bwana ndiyo kwenye mapokeo ya kiimani, kutoka jamii moja hata ingine, hulingania hadhi ya ‘chumvi’ na ‘nuru’ kwa umma wake. Kwenye Imani ya Uyuda, ndiyo imeleta >
‘Zaburi ya Daudi’< na kuhimidi >
‘Haleluyah’<—kulisifu na kulihimidi jina laYe; Katika Injili ya Yesu ndiyo imeleta >
‘Sala ya Bwana’< na katika Taifa Islamu, ndiyo Tahmidi ya kusema >
‘Alhamdullilah’<; pia mlango wa Imani ilivyo ni >
‘Surah-Al Fatiha’<…
Kiuono na Ufikirifu mifumo, ‘Bwana wa Ulimwengu’, si tu ni chimbuko la mapokeo yote ya kiimani kuanzia na Uyuda; kuhusu ‘Mamlaka na Utawala’, bali pia ni ontolojia ya uumbaji wote kwa misingi ya kaya. Kwamba taasisi zote zinawezapata ‘maana’ kwa vina na tafsiri yenye kuanzia na ule ‘utatu’ wa Baba, Mama na Mtoto. Ubaba ukiwa ni ‘mboni’ ya mazingira na mustabali wa kaya, katika sura ya mapana fulani ya ‘milki’ na ‘ustawi’. Mama kuwakilisha neema, amali na fanaka ya kaya; Basi wazazi kuwa kana ni upinde na mtoto ni mshale wa muendelezo wa utaasisi wa kaya… Kupitia mtoto, mapenzi, nia na baraka za wazazi hutafuta nasibu ya ‘mema ya nyakati’ kupitia ‘kudra’ na ‘karama’ katika mwili na akili ya mtoto, kama vile hivyo imepatakuwa kwa wazazi wenyewe… Sala ya mzazi basi, ingalikuwa mapenzi mema yawe kwa mtoto, kama vile yalivyo kati ya wazazi, siku zote na milele.
‘Mboni’, kiuno na ufikirifu mifumo, ni ishara na alama hasa ya ‘Taasisi’; kwa kuwa kuna dhahiri ya kuona kwamba kudra na karama vyote, hutokea kwa mshahibiano wa ‘uweza’, ‘unasaba’ na ‘nguvu katika matendo na matokeo yake. Kadri vile mboni ya jicho huwa na ‘duara la nje’ na ‘kitovu cheusi’ cha katikati, ndivyo hiyo huwa ni dirisha la ‘siri za roho’ katika kiumbe kupitia >‘sonafi’<. Taasisi zote huwepo ndani ya taasisi nyingine, hakuna taasisi ‘inayopakana’ na nyingine zaidi ya moja…. Hili ndilo latuletea picha na dhana ya ‘usupasha’—maumbo-mazingira, nguvu za ushawishi na wakati…
Kwenye utamaduni wa Urastafari nidhamu yake mtu-Rasta ya rizoningi, ule ujengaji wa nguvu ya hoja katika mazungumzo, huwa na tunu ikiwa hoja zake zaonekana kutokana na yeye kuwa na >‘Rasta-Far-Eye ilivyo ni Rasta-Far-I’<—Jicho-Ona-Mbali katika mtu-Rasta. Miditisha ya mtu-Rasta hutajwa kama ‘I-ditation badala ya me-ditation’; kwa kuwa kiouno mfumo katika mtu-Rasta, ‘umimi’ haufai—Nia thabiti ya ‘Umoja’ na kilichohasa kati ya mtu na mtu, mtu na JAH ndicho ‘I’… Tofauti na hili, ni mtu ‘kujijaza ubatili mtupu’—kusemwa katika lugha ya kiingereza ni >
‘vexation of spirit’<… Maisha ya mtu-Rasta, ni ya Imani katika JAH na hapo hapo ni ya kutazama uumbaji kwa >
jicho la mahabuba<… Ambavyo kiingereza chake, Uumbaji hutajwa kama ‘I-ration’ badala ya ‘Creation’…
...
-_-