MUNGU YUPO , kuwepo kwa Mungu hakuthibitishi kwa maandiko ya dini yoyote ila maandiko yamemtaja Mungu, wengi kwa kuamgalia maandiko wamekuja na hoja pinzani kwani vitabu hivyo haviwezi kujibu hoja kwani vipo kuelezea hasa maisha ya mwanadamu na sio kuleta majibu ukitaka kuthibitisha Mungu kwa maandiko ya dini utakwama
Mungu ni kiswahili lakini neno halisi ni muumbaji
Kwa kizungu the creator kwa maana mtengenezaji wa ulimwengu
Kwa formula ya kisayansi hakuna kitu kinachoweza kujitengeneza chenyewe lazima awepo aliye kibuni na kuiunda
Wanadamu hawawezi kutokea tu ghafla ulimwengu umepangika kwa hesabu kamili
Wanasayansi wamechunguza mambo mengi na kugundua yamefanyika kwa hesabu kamili hivyo inatoa uthibitisho kuwa alikuwepo aliyefanya kazi hii kwa umakini zaidi yani mtengenezaji (ndio watu wanamuita Mungu)
Bila hata dini hizi zetu ambazo nyingi zimekuja huku kutoka kwa wazungu na waarabu ma Babu zetu alitambua Mungu yupo ndio wakampa jina
Karibu kila kabila lina jina la Mungu kwa rugha yake hata waleta dini waliendelea kutumia majina
Tofauti tu zizopo ni namna na taratibu za kumwabudu ndio zilitofautiana na hasa hapa ndio huwa msingi wa kitu kinaitwa imani
Imani katika dini kwa rugha nyepesi ni mtazamo wa mtu au kikundi cha watu juu ya taratibu na kanuni za namna ya kufanya katika kuabudu
Mungu yupo kwa sababu yupo na sio yupo kwa imani ,imani ni mlango wa kuwasiliana naye
Hata kama hakuna wa kumwabudu bado atabaki kuwa muumbaji
Mungu ni mkuu sana binadamu ni kama sisimizi tu mbele zake uamini usiamini kwake huwezi kumuongezea chochote
Wanadamu wanamhitaji Mungu kwa faida yako na sio Mungu kumhitaji binadamu kwani akitaka kwa sekunde moja anaweza kufuta kila kiumbe akaanza upya kama wewe unavyo weza kubomoa majengo yako ukajenga upya
Mungu yupo na anatisha kama nini huyu aliyemuumba binadamu kwa ufahamu wa hali ya juu sana ukiusoma mwili wa binadamu kuna maajabu makubwa sana jicho tu la binadamu ni sayansi ya hali ja juu bado mfumo ya moyo sensor za mwili mfumo wa ulinzi ,figo nk
Wengi kwa sababu ya kuvimbewa tu ndio uja na hoja ya hakuna Mungu ,
Wenye akili walifikili na kuja na majibu ya kwamba ni "mpumbavu tu usema moyoni hakuna Mungu"
Kama ulivyo mfumo wa mwili unafanya kazi Mungu alisha maliza mambo yote kwa sasa yupo na mengine haya unayo yaona ni kanuni tu zinatenda kazi ukiamini utaona nguvu za Mungu usipoamini utaona nguvu za shetani mambo yote yanaendelea na kubadilika kwa kwanini yeye alisha maliza hana kazi nyingine ya kufanya kwetu kama ilivyo majira ya mvua kupanda na kuvuna ndiyo yalivyo maisha yote alipanga na kumaliza