Physics - A, chemistry - B, Hesabu - A, aende kusomea chuo gani na taaluma ipi ya Engineering ?

Physics - A, chemistry - B, Hesabu - A, aende kusomea chuo gani na taaluma ipi ya Engineering ?

Kuna mtoto wa dada yangu kapata hayo matokeo kwenye masomo ya Science,

Hataki kusikia habari za form 6, anataka kuanza safari yake ya kusomea taaluma mapema, hivyo kaamua aende chuo

Shida inakuja anapenda taaluma ya engineering ila hajui ipi aiseomee,

hofu yangu asije akaenda kusomea engineering itayompa shida kupata fursa mfano petroleum engineering, agriculture engineering, textile engineering, environment engineering, n.k.

Nimefanya research kwa kuanzia maarufu angalau kuna matumaini ni Computer Engineering, Mechanical Engineering, Electical Engineering na nyingine unaweza kunishauri

Naombeni ushauri kwa kuzingatia tatizo la ajira, aende kusomea kitu ambacho angalau kina soko, pia kuwe kuna matangazo ya ajira mara kwa mara.

Mimi nikajua ni pass za A-level;
Mwambie aache ujinga aende A- LEVEL. Masomo ya A- level ni muhimu sana na huwa yanamjenga mwanafunzi na kumpa kujiamini na hata akiamua kuja kusoma Diploma huko mbeleni ata stand out...
Soko la ajira na hata kujitegemea kwa karne hii kunahitaji zaidi ya ujuzi....Aende A- LEVEL huo ndio ushauri wangu.......SOKO LA AJIRA LINAHITAJI MTU ANAYEJIAMNI KAMA FARU JOHN
Diploma awaachie wale wenye pass za kati..
 
Mkuu kwa hali ya bongo ilivyo sioni kama ni vema kusomea kitu unachokipenda wakati hakina demand, nina rafiki alikuwa anapenda mambo ya bima akasomea insurance, kahangaika sana baada ya kuhitimu
Mi nashauri ajaribu Mechatronics Engineering inatolewa pale MUST.
 
Kama anashaurika, muambie akipata elimu ya kimataifa(world class education) ni vizuri zaidi.

Aende advance, achukue tahasusi yeyote ya STEM

Asome kwa nguvu sana, huku akitengeneza extracurriculars nzuri

Akimaliza afanye mtihani wa SAT, atafute vyuo vya nje

Napendekeza China kwasababu inapokea sana waafrika, ina ushirikiano mkubwa na Tanzania, kuna chama kabisa cha watanzania wanaosoma China(TASAFIC)

Pia itakuwa rahisi kupata ufadhili China, na hua serikali ya Tanzania inapewa sana scholarships inazitangaza

Akiweza kutengeneza extracurriculars nzuri, na akafaulu kwa viwango wa juu, anaweza kwenda kwenye vyuo vikubwa vya china(T9) akasome degree, atakuwa ametisha sana

Shida tu, ni kwamba inabidi ajikaze ajifunze kichina, na kiingereza pia kitatahiniwa

Haya ni mawazo yangu baada ya kufanya uchunguzi mrefu, kama unaona ni vizuri, tafuta wajuzi zaidi uone kama unaweza kubahatisha hizi fursa
 
Gawanya "wastani kwa idadi" utajua aende akasomee nini. Mkuu,mtoto hapangiwi akasome nini,matokeo yake ndiyo yatakayo identify kuwa akasomee nini,na kama akipangiwa course au comb tofauti na anavyotaka yeye atabadilisha mwenyewe,manake ukitaka umpangie wewe,akasome nje ya ndoto zake hapo tutakuwa tunatengeneza viongozi au watendaji wazembe,wala rushwa,wahujumu uchumi,mafisadi nk. USIINGILIE NDOTO ZA WATOTO MKUU.
 
Kuna vitu lazima umshauri mtu asomee kulingana na mazingira ya nchi, soko la ajira, fursa za kujiajiri, n.k.

huu utaratibu wa "ilimradi kuhitimu chuo" umeharibu maisha ya watu wengi sana, mtu anaenda kusomea Food science, Anthropology, Insurance, n.k. kwa Tanzania hii ni maamuzi mabovu
 
Lakin pia Tamisemi Wana utaratibu baada ya matokeo kutangazwa hua wanafungua dirisha la kuchagua upya selection zao. Kama fursa hio utakuwepo mwaka huu basi afanye kujaza technical college iwe first choice, piaa second choice iwe hio hio technical college then choice zinazobaki ataweka advance na vyuo vya afya.
Faida ya kuchaguliwa na serikali atalipiwa michango yote Hadi chakula, bima pekee na michango michache Sanaa atajilipia.
Piaa siku hizi Kuna diploma zinapewa kipaumbele kwa ajiri ya mikopo kutoka HESLB.
Engineering ni miongoni mwa hizo kozi zinazopewa kipaumbele
 
Kama anashaurika, muambie akipata elimu ya kimataifa(world class education) ni vizuri zaidi.

Aende advance, achukue tahasusi yeyote ya STEM

Asome kwa nguvu sana, huku akitengeneza extracurriculars nzuri

Akimaliza afanye mtihani wa SAT, atafute vyuo vya nje

Napendekeza China kwasababu inapokea sana waafrika, ina ushirikiano mkubwa na Tanzania, kuna chama kabisa cha watanzania wanaosoma China(TASAFIC)

Pia itakuwa rahisi kupata ufadhili China, na hua serikali ya Tanzania inapewa sana scholarships inazitangaza

Akiweza kutengeneza extracurriculars nzuri, na akafaulu kwa viwango wa juu, anaweza kwenda kwenye vyuo vikubwa vya china(T9) akasome degree, atakuwa ametisha sana

Shida tu, ni kwamba inabidi ajikaze ajifunze kichina, na kiingereza pia kitatahiniwa

Haya ni mawazo yangu baada ya kufanya uchunguzi mrefu, kama unaona ni vizuri, tafuta wajuzi zaidi uone kama unaweza kubahatisha hizi fursa
Ushauri mzuri, japo binafsi sioni umuhimu wa advance. Hivi kusoma China ni lazima mtu awe na ACSEE?
 
Hivi kusoma China ni lazima mtu awe na ACSEE?
Hichi kitu ndo sijui, bado nafuatilia

Kwasababu niliona scholarship inatanganazwa na serikali, wanasema upeleke cheti cha A-level

Ila ni vizuri kwasababu elimu ya China ni ngumu, physics na math inabidi engineer azipige kwa sana
 
Nilisoma chuo na watu waliishia F IV, hakika wale jamaa walipata shida sana chuoni. Maths na physics walikuwa wanatumia nguvu nyingi sana, na baadhi walinyanyua kwapa semester ya pili tu.

Ila kama mtu anamaliza F iV then anaenda diploma, akitoka anaweza kuingia varsity vizuri sana.
 
Kuna hii fani inaitwa BIOMEDICAL engineering,

Iko sokoni Sana Kwasasa serikalini

Graduates Wanasainishwa mikataba wakiwa huko huko field.
 
Zamani form 4 mtu anakuwa na maamuzi hata ya kupewa mke na kupewa uongozi. Ukifatilia zamani huyu wasira alianza uongozi mdogo kabia.

Sasa kama mtu amemaliza form 4 lakini bado unaona hajakuwa.Huko shule alienda kusomea ujinga???

Wenzetu wazungu( BINADAMU KAMILI) umri wa miaka 23 mtu anamaliza masters sasa hiyo hoja yako ya kwamba mtu asiende chuo kwakuwa ni mdogo kwa umri unadhani ni sahihi??
Zamani gani tena? Ni hii ambayo watoto walikuwa wanaanza shule na miaka 10 au zaidi? Unaijua background ya Wasira? Tusipoipuuza hii comment yako utaanza kufananisha mtoto wa Mwigulu na watoto wengine wa makapuku.
 
Kuna mtoto wa dada yangu kapata hayo matokeo FORM 4

Hataki kusikia habari za form 6, anataka kuanza safari yake ya kusomea taaluma mapema, hivyo kaamua aende chuo

Shida inakuja anapenda taaluma ya engineering ila hajui ipi aiseomee,

hofu yangu asije akaenda kusomea engineering itayompa shida kupata fursa mfano petroleum engineering, agriculture engineering, textile engineering, environment engineering, n.k. kuna taaluma zipo kisiasa, ni za majaribio, kuongeza mapato ya chuo, n.k. zinawaacha wahitimu wanasota

Nimefanya research nimeona angalau kuna matumaini kwenye Computer Engineering, Mechanical Engineering, Electical Engineering na nyingine unaweza kunishauri

Naombeni ushauri kwa kuzingatia tatizo la ajira, aende kusomea kitu ambacho angalau kina soko, pia kuwe kuna matangazo ya ajira mara kwa mara.
Aende kusomea ujenzi wa makaburi.., ahsante nitapokea baadae kabisa
 
Kuna jewelery and Lapidary,

Hii nayo nzuri Sana,
Kuna ambao magufuli aliwasomesha Bure (grants) na kuwasainisha kufanya KAZI serikalini punde tu watakapohitimu,Mama nae naona kafata trendi Ile Ile ya Jiwe.

Wengi wako maabara za madini na Taasisi za utafiti WA madini za serikalini na pale mgodini merelani, hasa Baada ya ule ukuta kujengwa.
 
Back
Top Bottom